Sakata la Makontena: Makonda azua balaa bandarini

Sakata la Makontena: Makonda azua balaa bandarini

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,983
Makontena aliyoingiza nchini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, yameleta ‘shida sana’ bandarini na sasa mfumo wa kutoa na kuingiza makontena kwenda kwenye ICD utabadilishwa, JAMHURI limebaini.

“Kwa kweli hapa tulikuwa tunaangalia bill of lading na taarifa za mzigo (cargo manifest). Lakini pia kule TICTS walikuwa bado wanaweza kutoa makontena kwenda kwenye ICDs (Bandari Kavu) bila kutushirikisha.

“Hata haya makontena ya Makonda kwenda DICD yalipitia TICTS. Sasa kwa kweli utaratibu huu tumeona hapana. Sisi Bandari tayari sheria imebadilishwa na kutuongezea madaraka, hivyo kuanzia sasa tutatoa utaratibu utakaomtaka kila mteja kuorodhesha mali au bidhaa zilizomo kwenye kontena.

“Utaratibu wa sasa unaweza kukuta tunaingiza hadi mabomu bila kujua, maana scanner huwezi kufahamu kama zinatumika vilivyo. Mkurugenzi Mkuu [Deusdedit] Kakoko amekuwa akisema mara zote na sasa naona hili litatekelezwa kwa jinsi alivyo
mkali.

“Baadhi ya watu aliowakuta hapa bandarini walikuwa wanasema analeta utaratibu mpya usiokubalika, hautafanya kazi, lakini angalia mapato ya bandari yalivyopanda. Tunahitaji fikra mpya, hivyo hata hii akitaka vitu vyote viorodheshwe kimoja baada ya kingine vilivyomo ndani ya kontena lazima ifanyike.

“Sasa si umeona kwa makontena ya Makonda tunaambiwa ni viti vya shule kumbe kuna hadi masofa kama alivyosema Mheshimiwa Rais [John] Magufuli. Hii ni hatari, inabidi orodha ya bidhaa kwenye kontena itolewe,” kimesema chanzo chetu.

JAMHURI limemtafuta Injinia Kakoko kufahamu utaratibu huu mpya utaanza kutekelezwa lini, akasema: “Hili ni muhimu, ila nakwenda safari, ngoja nikirudi tutalizungumza kwa kina. Lazima bandari zetu ziwe salama na muda wote nimekuwa nikibana ninapobaini ulegevu,” amesema Injinia Kakoko.

Wiki iliyopita Gazeti la JAMHURI lilichapisha habari kuhusu Rais Magufuli akimkemea Makonda na kumtaka alipe kodi kwa maelezo kuwa serikali haijaomba msaada wa viti kwa walimu. Rais Magufuli alisema ndani ya makontena taarifa alizonazo kuna hadi masofa, ambayo hayawezi kuwa vifaa vya walimu.

Fikra hizi za Bandari zinakuja siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kuzulu eneo la kuhifadhia makontena – Bandari Kavu Dar es Salaam(DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kisha akaiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya serikali inayokadiriwa kufikia Sh bilioni 1.2.

Hata hivyo makontena hayo kwa wiki tatu mfululizo sasa yamekosa wateja, huku Makonda akitoa tishio kuwa yeyote atakayeyanunua Mungu atamlaani.

Dk. Mpango alisema kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba
amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na mkuu huyo wa mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakayenunua mzigo huo atalaaniwa.

“Sheria za nchi hazichagui sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilichoapa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyopewa. Kwa hiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba,” alisisitiza Dk. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Forodha, Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliyeagiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahiki na asipolipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

“Napenda niwaombe viongozi wenzangu serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii?” alieleza kwa masikitiko Dk. Mpango.

Dk. Mpango alitoa wito kwa Watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama ofisini kama vile viti, meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.
 
Ndugu wakigombana shika jembe ukalime....
 
Yaan mkuu wa mkoa anafanya udanganyifu "false declaration" lakini.anaachwa? Dah hii ngumu sana..ila masikini.akifika bandari na kigari chake anaminywa mpaka tone.la.mwisho la damu
 
Nchi hii ngumu sana , people are very corrupted.
Wanatuchanganya: kila kasha linapoingia lazima bandari wajue kilichomo ndani ndo maana wana print manifest inayoonesha aina ya bidhaa iliyopo ili mamlaka za udhibiti zifanye kazi yake
 
Back
Top Bottom