Sakata la Madini: Rais Magufuli ameagana na Nyonga?

Tufuate taratibu za kimkataba kuzuia wizi,hata TRA huwa wanatoa notice kwa mdaiwa kama wanahisi kawapunja,sisi hao Acacia mpaka leo wanasema hawajui kilichomo kwenye ripoti ya mchanga!

Mikataba ya kimataifa ina taratibu za kutatua mgogoro baina ya pande husika,tumezifuata?

Kama tumeibiwa mbona hatuendi mahakamani tumebaki kuitisha wazee wa Dar es salaam,ma-tv na kadhalika?

Hatuna wanasheria?
Kulikua kuna sababu ya kujua kuwa hii vita ni kubwa hivyo tunahitaji mbinu mpya,silaha za kisasa,wapiganaji mahiri n.k ili kushinda vita hivi.Na hivi vyote vitapatikana kwa nchi kuwaita watu wake bila kujali itikadi za kisiasa wala za kidini kukaa pamoja na kulijadili kwa kina ndipo ijulikane pa kuanzi.Watz wapo tayari lakini wametengwa na kupuuzwa kimakusudi kabisa ikijulikana watatoa mawazo ambayo hayapendwi na watawala.Mfano labda tungeanza na wazo la kuwa na katiba mpya!Labda tungepitia mikata yote ya uwekezaji mkubwa kwa upya!Labda tungejitoa kwenye mikataba ya kimataifa itakayo tubana baadae tukitaka kuwashughuikia hawa mabepari!N.k!
 
JPM AMEAGANA NA NYONGA?

Katika makala ya jana nilieleza kinagaubaga jinsi ambavyo madini na mafuta yalivyokuwa muhimu kuliko hata uhai wa binadamu (ubepari ni unyama?). Nilitoa mfano wa Patrice Lumumba mwana halali wa Afrika ambaye alitolewa uhai kwa sababu aliamua kusimama upande wa wananchi kutetea rasilimali za DR Congo. Mataifa ya Ulaya na Marekani hayawezi kuishi bila kuchukua rasilimali zetu, ndio maana wanafanya kila namna kuhakikisha wanafanikisha hilo. Kwa sasa wanatumia makampuni makubwa ya Kimataifa kufanikisha adhima yao wakisaidiwa na baadhi ya wazawa wasio wazalendo. Katika Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria, Profesa Chachage Sethy Chachage ameeleza kinagaubaga jinsi mnyororo wa unyonyaji unavyoendeshwa.

Katika vita ambavyo Magufuli ameanzisha (kama sio kuendeleza), nimetahadhalisha na kueleza kwamba ni vita ngumu. Hivyo Rais Magufuli anatakiwa kusaidiwa ili kuweza kufanikisha adhima hiyo. Ni muhimu sana wananchi kuwa nyuma ya serikali, wakati wabunge wakipata fursa ya kupitia mikataba ya madini na kufanya marekebisho kwa faida ya wananchi na makampuni yanayochimba. Kama Magufuli ameamua kwa dhati ya moyo wake kupigana vita hii, atambue kwamba anapambana na mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani. Asijidanganye kwamba anapambana na Barrick, Accasia au Ashanti Gold Mines. Ukiyagusa makampuni hayo umegusa masilahi ya nchi zao.

Je, Magufuli ameagana na nyonga? Amejipanga kupigana vita hii kwa dhati ya moyo wake? Ni pekee yake au ni vita ya serikali yake nzima? Washauri wake na watalaam mbalimbali katika sekta ya madini na mafuta na sheria wanashirikishwa jambo hili? Anajua hila za Mataifa ya Ulaya na Marekani? Amejiandaa vipi na madhara yatakayotokana na hii vita?

Maswali ni mengi sana ambayo mtu anaweza kujiuliza. Hili si suala la kufanyia propaganda, ni suala nyeti ambalo wabunge wanatakiwa kutimiza wajibu wao, watalaam wengine washauri kwa kadri ya ufahamu wao, na sisi wananchi tushauri kwa kadri tunavyojua. Hayo yote tusiyadharau. Kwa bahati mbaya sana, Taifa letu linaugua ugonjwa wa chuki. Mtu anayetoa mawazo tofauti na wewe anaonekana kama hamnazo, ana wivu na anakosa uzalendo. Hiki ni kitu kibaya sana. Watu wapate nafasi ya kupumua. Tukiwazuia tusishangae wakiwa upande wa adui.

Lengo la makala hii ni kumpa tahadhali Mhe. Rais katika vita hii ambayo ameianzisha. Patrice Lumumba, Thomas Sankara na wapigania uhuru wengi kote Afrika walifanya makossa ambayo yaliwapotezea uhai wao. Walikuwa na nia njema sana, lakini hatua ambazo walikuwa wanachukua, nyingi hazikuwa sahihi. Kwa mfano, Lumumba alijichanganya mwenyewe. Aliwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Akawa na uhusiano na USSR na Marekani kwa wakati mmoja. Alihatarisha masilahi ya Marekani ndani ya Congo na kuwapa nafasi zaidi nchi za Kijamaa, na wakati huo alitegemea kupata msaada kutoka kwa nchi zote. Hiki ni kitu kigumu.

Kuna kitu tukitegemee huko mbeleni kama vita hii itaendelezwa. Lazima tuangalie upya mahusiano yetu na nchi ambako makampuni ya madini yanakotoka. Tunachokifanya hakiwafurahishi na wakati huo huo tunategemea kupata msaada kutoka kwao. Wana mbinu nyingi sana za kuweza kutuvuruga. Siku hizi hawaji na wanajeshi kukupiga. Wanatumia makampuni ya kimataifa na wananchi wachache kupitia NGOs na vyama vya siasa. Migogoro mingi ndani ya Afrika, mfano iliyotokea Afrika Kaskazini ilipandikizwa.

Wakati tunajipanga kupigana hii vita, ni muhimu serikali ya JPM ikawa sikivu. Inawezekana ni kweli Rais ana dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha rasilimali zetu zinawanufaisha wananchi, lakini njia zinazotumika zikawa na walakini. Tuwape nafasi watalaam kushauri na watendaji kufanya kazi zao. Rais hawezi kujua kila kitu. Awaamini watendaji wake, na kuwawezesha ili wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa. Asipigane vita hii pekee yake, atashindwa. Aweke misingi endelevu ya kupambana vita hii, ili hata asipokuwepo mambo yawe yanaendelea. Rais asijijenge yeye peke yake, ajenge mfumo imara zaidi wa kupambania rasilimali zetu.

Nafasi ya vyama vya upinzani ni kubwa katika vita hii. Wanaweza kusaidia kushinda vita hii, au wanaweza kutuhujumu. Hayo yote yatategemea na jinsi tunavyowaona na kuwapa fursa. Tuache vyama vya upinzani wafanye kazi zao kwa wazi kabisa. Tukiwazuia, wanaweza kufanya hila. Vyama vya upinzani vipo kisheria. Wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, haina haja kuwazuia. Hii ni nchi ya kwetu zote, na kila mtu ana umuhimu wake. Pamoja na udhaifu wao, lakini wameibua mambo mengi sana mazuri ambayo serikali ilitakiwa kuwasikiliza. Suala la madini limezungumzwa sana na watu wa aina mbalimbali, wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani. Hoja anayokuja nayo Magufuli sio mpya ilikuwepo na pengine itaendelea kuwepo. Kuna watu makini sana na wazalendo kwenye vyama vya upinzani, tuwape nafasi, tuwasikilize maoni na mapendekezo yao, mazuri tuyafanyie kazi.
Mkuu viongozi waliotutangulia wangekuwa na mawazo kimsingi ya kijinga kama haya basi watanzania wangerudi utumwani.
Samahani lakini.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kulikua kuna sababu ya kujua kuwa hii vita ni kubwa hivyo tunahitaji mbinu mpya,silaha za kisasa,wapiganaji mahiri n.k ili kushinda vita hivi.Na hivi vyote vitapatikana kwa nchi kuwaita watu wake bila kujali itikadi za kisiasa wala za kidini kukaa pamoja na kulijadili kwa kina ndipo ijulikane pa kuanzi.Watz wapo tayari lakini wametengwa na kupuuzwa kimakusudi kabisa ikijulikana watatoa mawazo ambayo hayapendwi na watawala.Mfano labda tungeanza na wazo la kuwa na katiba mpya!Labda tungepitia mikata yote ya uwekezaji mkubwa kwa upya!Labda tungejitoa kwenye mikataba ya kimataifa itakayo tubana baadae tukitaka kuwashughuikia hawa mabepari!N.k!
Point!

Tatizo mawazo yanatoka upande mmoja,kiasi kwamba hata wabunge hawaruhusiwi kuwa laivu!
 
Makala na Uzi huu Ni mzuri Sana, Tatizo Uchama unaligharimu taifa letu
 
Vita ya ukombozi wa afrika kisiasa ilikuwa na kamati kadhaa ikiwamo OAU ya kipindi hicho,

Sasa huu ukombozi wa kiuchumi utaufanya wakati hata kusafiri nje ya nchi unaogopa?

Uhuru kenyata alitembea duniani kwa marais wote akiwataka waipinge ICC na akafanikiwa,kesi ikafutwa!

Mkuu wetu angeenda huko makao makuu ya mabepari akajenga hoja kuhusu migodi,maliasili,akaungana nguvu na mataifa mengine ambako Barrick anafanya kazi,wakawa na nguvu moja kidiplomasia

Angefanya mpango walau akapata azimio la umoja wa afrika kuhusu raslimali,ingekuwa ni major diplomatic pressure!
Tatizo hapa ni kuchukua swala hili kisiasa. hawa wanaolianzisha ndio waliolifikisha hapa. hii sio kick ya 2020. maana naona kama kwingine kote hakusomi yawezekana ni jitihada ya kupata kick
 
Harmorapa katuharibia nchi hii
 
JPM AMEAGANA NA NYONGA?

Katika makala ya jana nilieleza kinagaubaga jinsi ambavyo madini na mafuta yalivyokuwa muhimu kuliko hata uhai wa binadamu (ubepari ni unyama?). Nilitoa mfano wa Patrice Lumumba mwana halali wa Afrika ambaye alitolewa uhai kwa sababu aliamua kusimama upande wa wananchi kutetea rasilimali za DR Congo. Mataifa ya Ulaya na Marekani hayawezi kuishi bila kuchukua rasilimali zetu, ndio maana wanafanya kila namna kuhakikisha wanafanikisha hilo. Kwa sasa wanatumia makampuni makubwa ya Kimataifa kufanikisha adhima yao wakisaidiwa na baadhi ya wazawa wasio wazalendo. Katika Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria, Profesa Chachage Sethy Chachage ameeleza kinagaubaga jinsi mnyororo wa unyonyaji unavyoendeshwa.

Katika vita ambavyo Magufuli ameanzisha (kama sio kuendeleza), nimetahadhalisha na kueleza kwamba ni vita ngumu. Hivyo Rais Magufuli anatakiwa kusaidiwa ili kuweza kufanikisha adhima hiyo. Ni muhimu sana wananchi kuwa nyuma ya serikali, wakati wabunge wakipata fursa ya kupitia mikataba ya madini na kufanya marekebisho kwa faida ya wananchi na makampuni yanayochimba. Kama Magufuli ameamua kwa dhati ya moyo wake kupigana vita hii, atambue kwamba anapambana na mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani. Asijidanganye kwamba anapambana na Barrick, Accasia au Ashanti Gold Mines. Ukiyagusa makampuni hayo umegusa masilahi ya nchi zao.

Je, Magufuli ameagana na nyonga? Amejipanga kupigana vita hii kwa dhati ya moyo wake? Ni pekee yake au ni vita ya serikali yake nzima? Washauri wake na watalaam mbalimbali katika sekta ya madini na mafuta na sheria wanashirikishwa jambo hili? Anajua hila za Mataifa ya Ulaya na Marekani? Amejiandaa vipi na madhara yatakayotokana na hii vita?

Maswali ni mengi sana ambayo mtu anaweza kujiuliza. Hili si suala la kufanyia propaganda, ni suala nyeti ambalo wabunge wanatakiwa kutimiza wajibu wao, watalaam wengine washauri kwa kadri ya ufahamu wao, na sisi wananchi tushauri kwa kadri tunavyojua. Hayo yote tusiyadharau. Kwa bahati mbaya sana, Taifa letu linaugua ugonjwa wa chuki. Mtu anayetoa mawazo tofauti na wewe anaonekana kama hamnazo, ana wivu na anakosa uzalendo. Hiki ni kitu kibaya sana. Watu wapate nafasi ya kupumua. Tukiwazuia tusishangae wakiwa upande wa adui.

Lengo la makala hii ni kumpa tahadhali Mhe. Rais katika vita hii ambayo ameianzisha. Patrice Lumumba, Thomas Sankara na wapigania uhuru wengi kote Afrika walifanya makossa ambayo yaliwapotezea uhai wao. Walikuwa na nia njema sana, lakini hatua ambazo walikuwa wanachukua, nyingi hazikuwa sahihi. Kwa mfano, Lumumba alijichanganya mwenyewe. Aliwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Akawa na uhusiano na USSR na Marekani kwa wakati mmoja. Alihatarisha masilahi ya Marekani ndani ya Congo na kuwapa nafasi zaidi nchi za Kijamaa, na wakati huo alitegemea kupata msaada kutoka kwa nchi zote. Hiki ni kitu kigumu.

Kuna kitu tukitegemee huko mbeleni kama vita hii itaendelezwa. Lazima tuangalie upya mahusiano yetu na nchi ambako makampuni ya madini yanakotoka. Tunachokifanya hakiwafurahishi na wakati huo huo tunategemea kupata msaada kutoka kwao. Wana mbinu nyingi sana za kuweza kutuvuruga. Siku hizi hawaji na wanajeshi kukupiga. Wanatumia makampuni ya kimataifa na wananchi wachache kupitia NGOs na vyama vya siasa. Migogoro mingi ndani ya Afrika, mfano iliyotokea Afrika Kaskazini ilipandikizwa.

Wakati tunajipanga kupigana hii vita, ni muhimu serikali ya JPM ikawa sikivu. Inawezekana ni kweli Rais ana dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha rasilimali zetu zinawanufaisha wananchi, lakini njia zinazotumika zikawa na walakini. Tuwape nafasi watalaam kushauri na watendaji kufanya kazi zao. Rais hawezi kujua kila kitu. Awaamini watendaji wake, na kuwawezesha ili wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa. Asipigane vita hii pekee yake, atashindwa. Aweke misingi endelevu ya kupambana vita hii, ili hata asipokuwepo mambo yawe yanaendelea. Rais asijijenge yeye peke yake, ajenge mfumo imara zaidi wa kupambania rasilimali zetu.

Nafasi ya vyama vya upinzani ni kubwa katika vita hii. Wanaweza kusaidia kushinda vita hii, au wanaweza kutuhujumu. Hayo yote yatategemea na jinsi tunavyowaona na kuwapa fursa. Tuache vyama vya upinzani wafanye kazi zao kwa wazi kabisa. Tukiwazuia, wanaweza kufanya hila. Vyama vya upinzani vipo kisheria. Wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, haina haja kuwazuia. Hii ni nchi ya kwetu zote, na kila mtu ana umuhimu wake. Pamoja na udhaifu wao, lakini wameibua mambo mengi sana mazuri ambayo serikali ilitakiwa kuwasikiliza. Suala la madini limezungumzwa sana na watu wa aina mbalimbali, wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani. Hoja anayokuja nayo Magufuli sio mpya ilikuwepo na pengine itaendelea kuwepo. Kuna watu makini sana na wazalendo kwenye vyama vya upinzani, tuwape nafasi, tuwasikilize maoni na mapendekezo yao, mazuri tuyafanyie kazi.
Ulipolalia ndipo alipoamkia. Haya yote anayafahamu na anayatendea kazi. Cha msingi fahamu tu hao viongozi wa upinzani wanajijali wao zaidi ya watanzania . kwa maoni yangu wala hawapaswi kuwepo nchi hii. Tutasimama na rais wa wote na sio kiongozi wa ukoo flan. Tutapigana hadi tone la mwisho la uhai wetu. "Mali zetu au kifo" in che Guevara's voice
 
Hapa kwa taarifa yake tunapambana na marekani na Israel.Kampuni za wayahudi hizi.
 
Tunachohitaji ni collective leadership, tukae pamoja kama watanzania vyama vikae pembeni tufanye maendeleo. Hii ni ngumu kwa wengine kwa sababu ni ndumilakuwili au kichwani hamna kitu ni bendera fuata upepo
Hebu vuta picha walivyokemewa wabunge wa kijani walioenda kumsalimu lema gerezani,
Hebu fikiri yule mbuge alomgawia dk za ziada mbunge wa upinzani nini kilimtokea,
Nimekutangulizia hayo kukuandaa kupokea nnachotaka kusema,
Hawa watu wa kijani njano,wanaroho za ajabu sana kiasi unaloongea ww haliwezekani kabisa,kwao bora nchi iharikiwe kuliko kuchukua ya upande wa pili,kifupi hawa jamaa ndo adui zetu kwa Mali zetu,wao ndo washika mrija wa wanyonyaji,hawa ni majizi wenza wa wawekezaji,
Haya maneno ya eti uchungu na nchi wanayatamka tu kutaka sifa,
Wao ukiwakosoa ama kuwashauri wapo radhi kukupoteza,
Binafsi naamini wanamsaidia shetani kututesa
 
Sasa mkikaa mezani,balozi wa nchi anakutupia mezani kabrasha la madeni ya mamia ya matrilioni ambayo nchi yake inakudai,ili ulinganishe na vibilioni unavyolalamikia
Hili nalo neno,unaomba udhuru kidogo uende uani ukapunguze maji.
 
Hebu vuta picha walivyokemewa wabunge wa kijani walioenda kumsalimu lema gerezani,
Hebu fikiri yule mbuge alomgawia dk za ziada mbunge wa upinzani nini kilimtokea,
Nimekutangulizia hayo kukuandaa kupokea nnachotaka kusema,
Hawa watu wa kijani njano,wanaroho za ajabu sana kiasi unaloongea ww haliwezekani kabisa,kwao bora nchi iharikiwe kuliko kuchukua ya upande wa pili,kifupi hawa jamaa ndo adui zetu kwa Mali zetu,wao ndo washika mrija wa wanyonyaji,hawa ni majizi wenza wa wawekezaji,
Haya maneno ya eti uchungu na nchi wanayatamka tu kutaka sifa,
Wao ukiwakosoa ama kuwashauri wapo radhi kukupoteza,
Binafsi naamini wanamsaidia shetani kututesa
Kabisa umenena mkuu
 
ili hata asipokuwepo mambo yawe yanaendelea. Rais asijijenge yeye peke yake, ajenge mfumo imara zaidi wa kupambania rasilimali zetu.
Hilo lilishawashinda kitambo utakuwa unahubiria maiti,unapopeleka muswada wa dharura wa madini au mafuta na gesi bungeni ni kwa maslahi ya nani??kwa nini dharura??ndio utajua hawa jamaa wa kijani ndio shetani wetu,hao ndio wachawi wetu,Warioba na tume iliyokuwa na wajumbe wengi toka kwenye chama chao lakini waliikataa na amini hata ushauri wako huu hawawezi kuukubali.
 
TUMESHAYAVULIA MAJI NGUO LAZIMA TUYAOGE
TUAANZA VITA YA KUIKOMBOA AFICA KIUCHUMI BAADA YA DHAMIRA YA KWANZA KUAKIKISHA KILA NCHI INAKUWA NA UHURU

Unajidanganya wewe!! Dunia hii wababe wa kuwavimbia hawa mabepari walikuwa wawili tu na wote ni marehemu kwa sasa. Hawa ni Hugo Chavez wa Venezuela na Kanali Gaddafi wa Libya.
 
Hilo lilishawashinda kitambo utakuwa unahubiria maiti,unapopeleka muswada wa dharura wa madini au mafuta na gesi bungeni ni kwa maslahi ya nani??kwa nini dharura??ndio utajua hawa jamaa wa kijani ndio shetani wetu,hao ndio wachawi wetu,Warioba na tume iliyokuwa na wajumbe wengi toka kwenye chama chao lakini waliikataa na amini hata ushauri wako huu hawawezi kuukubali.
Hii nchi kwa kweli
 
Unajidanganya wewe!! Dunia hii wababe wa kuwavimbia hawa mabepari walikuwa wawili tu na wote ni marehemu kwa sasa. Hawa ni Hugo Chavez wa Venezuela na Kanali Gaddafi wa Libya.
MAGUFURI TUMEMTANGULIZA TUPO ZAIDI YA 10000000.

MWENZETU TUKUKATE MKIA.

TOKA MAJIMAJI, TIPTIP , HATUJAWAI SALITIANA NAKUSHANGAA WEWE
 
Ulipolalia ndipo alipoamkia. Haya yote anayafahamu na anayatendea kazi. Cha msingi fahamu tu hao viongozi wa upinzani wanajijali wao zaidi ya watanzania . kwa maoni yangu wala hawapaswi kuwepo nchi hii. Tutasimama na rais wa wote na sio kiongozi wa ukoo flan. Tutapigana hadi tone la mwisho la uhai wetu. "Mali zetu au kifo" in che Guevara's voice
Mimi ckuelewi hata kidogo. Juzi MTU alisaini mkataba mbovu Leo MTU huyohuyo anakuja anasema oh tinaobiwa... hee wakati unasaini mikataba watu wengi wakiwemo wanasiasa wa upinzani asasi za kiraia walipiga kelele mbona kuna harufu mbaya kwenye mikataba hii. wakapinga na kudai kuwa hapana kila kitu kiko shwari. kwangu itachukua muda sana kuwaamini kuwa kwwli hawa wana nia njema na cc
 
Back
Top Bottom