mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
JPM AMEAGANA NA NYONGA?
Katika makala ya jana nilieleza kinagaubaga jinsi ambavyo madini na mafuta yalivyokuwa muhimu kuliko hata uhai wa binadamu (ubepari ni unyama?). Nilitoa mfano wa Patrice Lumumba mwana halali wa Afrika ambaye alitolewa uhai kwa sababu aliamua kusimama upande wa wananchi kutetea rasilimali za DR Congo. Mataifa ya Ulaya na Marekani hayawezi kuishi bila kuchukua rasilimali zetu, ndio maana wanafanya kila namna kuhakikisha wanafanikisha hilo. Kwa sasa wanatumia makampuni makubwa ya Kimataifa kufanikisha adhima yao wakisaidiwa na baadhi ya wazawa wasio wazalendo. Katika Riwaya ya Makuwadi wa Soko Huria, Profesa Chachage Sethy Chachage ameeleza kinagaubaga jinsi mnyororo wa unyonyaji unavyoendeshwa.
Katika vita ambavyo Magufuli ameanzisha (kama sio kuendeleza), nimetahadhalisha na kueleza kwamba ni vita ngumu. Hivyo Rais Magufuli anatakiwa kusaidiwa ili kuweza kufanikisha adhima hiyo. Ni muhimu sana wananchi kuwa nyuma ya serikali, wakati wabunge wakipata fursa ya kupitia mikataba ya madini na kufanya marekebisho kwa faida ya wananchi na makampuni yanayochimba. Kama Magufuli ameamua kwa dhati ya moyo wake kupigana vita hii, atambue kwamba anapambana na mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani. Asijidanganye kwamba anapambana na Barrick, Accasia au Ashanti Gold Mines. Ukiyagusa makampuni hayo umegusa masilahi ya nchi zao.
Je, Magufuli ameagana na nyonga? Amejipanga kupigana vita hii kwa dhati ya moyo wake? Ni pekee yake au ni vita ya serikali yake nzima? Washauri wake na watalaam mbalimbali katika sekta ya madini na mafuta na sheria wanashirikishwa jambo hili? Anajua hila za Mataifa ya Ulaya na Marekani? Amejiandaa vipi na madhara yatakayotokana na hii vita?
Maswali ni mengi sana ambayo mtu anaweza kujiuliza. Hili si suala la kufanyia propaganda, ni suala nyeti ambalo wabunge wanatakiwa kutimiza wajibu wao, watalaam wengine washauri kwa kadri ya ufahamu wao, na sisi wananchi tushauri kwa kadri tunavyojua. Hayo yote tusiyadharau. Kwa bahati mbaya sana, Taifa letu linaugua ugonjwa wa chuki. Mtu anayetoa mawazo tofauti na wewe anaonekana kama hamnazo, ana wivu na anakosa uzalendo. Hiki ni kitu kibaya sana. Watu wapate nafasi ya kupumua. Tukiwazuia tusishangae wakiwa upande wa adui.
Lengo la makala hii ni kumpa tahadhali Mhe. Rais katika vita hii ambayo ameianzisha. Patrice Lumumba, Thomas Sankara na wapigania uhuru wengi kote Afrika walifanya makossa ambayo yaliwapotezea uhai wao. Walikuwa na nia njema sana, lakini hatua ambazo walikuwa wanachukua, nyingi hazikuwa sahihi. Kwa mfano, Lumumba alijichanganya mwenyewe. Aliwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Akawa na uhusiano na USSR na Marekani kwa wakati mmoja. Alihatarisha masilahi ya Marekani ndani ya Congo na kuwapa nafasi zaidi nchi za Kijamaa, na wakati huo alitegemea kupata msaada kutoka kwa nchi zote. Hiki ni kitu kigumu.
Kuna kitu tukitegemee huko mbeleni kama vita hii itaendelezwa. Lazima tuangalie upya mahusiano yetu na nchi ambako makampuni ya madini yanakotoka. Tunachokifanya hakiwafurahishi na wakati huo huo tunategemea kupata msaada kutoka kwao. Wana mbinu nyingi sana za kuweza kutuvuruga. Siku hizi hawaji na wanajeshi kukupiga. Wanatumia makampuni ya kimataifa na wananchi wachache kupitia NGOs na vyama vya siasa. Migogoro mingi ndani ya Afrika, mfano iliyotokea Afrika Kaskazini ilipandikizwa.
Wakati tunajipanga kupigana hii vita, ni muhimu serikali ya JPM ikawa sikivu. Inawezekana ni kweli Rais ana dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha rasilimali zetu zinawanufaisha wananchi, lakini njia zinazotumika zikawa na walakini. Tuwape nafasi watalaam kushauri na watendaji kufanya kazi zao. Rais hawezi kujua kila kitu. Awaamini watendaji wake, na kuwawezesha ili wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa. Asipigane vita hii pekee yake, atashindwa. Aweke misingi endelevu ya kupambana vita hii, ili hata asipokuwepo mambo yawe yanaendelea. Rais asijijenge yeye peke yake, ajenge mfumo imara zaidi wa kupambania rasilimali zetu.
Nafasi ya vyama vya upinzani ni kubwa katika vita hii. Wanaweza kusaidia kushinda vita hii, au wanaweza kutuhujumu. Hayo yote yatategemea na jinsi tunavyowaona na kuwapa fursa. Tuache vyama vya upinzani wafanye kazi zao kwa wazi kabisa. Tukiwazuia, wanaweza kufanya hila. Vyama vya upinzani vipo kisheria. Wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, haina haja kuwazuia. Hii ni nchi ya kwetu zote, na kila mtu ana umuhimu wake. Pamoja na udhaifu wao, lakini wameibua mambo mengi sana mazuri ambayo serikali ilitakiwa kuwasikiliza. Suala la madini limezungumzwa sana na watu wa aina mbalimbali, wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani. Hoja anayokuja nayo Magufuli sio mpya ilikuwepo na pengine itaendelea kuwepo. Kuna watu makini sana na wazalendo kwenye vyama vya upinzani, tuwape nafasi, tuwasikilize maoni na mapendekezo yao, mazuri tuyafanyie kazi.