Sakata La Madini...je ni funika kombe mwanaharamu apite?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,269
23,205
Barrick Meets With Government of Tanzania to Commence Negotiations

TORONTO, June 14, 2017 — Barrick Gold Corporation Executive Chairman John L. Thornton met today with the President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Dr. John P. Magufuli, to discuss issues pertaining to Acacia Mining plc (“Acacia”), and the country’s current ban on mineral concentrate exports.

The meeting was constructive and open, with the parties agreeing to enter into negotiations to seek a resolution that is in the best interests of all stakeholders, including Tanzania, Barrick, and Acacia

Ifuatayo ni kauli ya Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton baada ya kukutana na Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kama nilivyojitahidi kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili...(natanguliza samahani kama kama kuna makosa)

Prof. John L. Thornton.

"Tumekuwa na majadiliano yenye mafanikio kuhusu tuhuma zinazoikabili kampuni ya ACACIA. Nimekuja hapa ili kusaidia kutatua tatizo na kumhakikishia Rais kwamba tuna nia ya kukaa chini na kutafuta azimio litakaloleta ushindi kwa wadau wote (ushindi kwa Tanzania, ushindi kwa Barrick na kampuni yetu tanzu ya ACACIA).

Baada ya kufanya mazungumzo hayo ya kina ninayo matumaini makubwa ya kufikia azimio hilo la ushindi na kuwataka wateuliwa wa kila upande (wa Rais na wa kwetu) wakae chini haraka kupitia kwa undani zaidi taarifa zote na najisikia vizuri sana kuhusu hatua tuliyopiga na maendeleo tuliyoyafikia hivi leo."

Maswali...

  1. Kwa nini tunajadiliana?
  2. Je lengo la majadiliano ni mashauriano, maridhiano au mapatano?
Ongezea na wewe sali kama unalo...
 
Swali...

Kwa nini tunajadiliana?
Wanawasahaulisha watanzania juu ya kibiti, Bajeti wizara ya fedha pia vyeti vya Daud Bashite mpaka ununuzi wa ndege na ujenzi wa reli na uwanja wa ndege chato.hawataki mkumbuke huko wameandaa skendo kibao zitatoka kadri wanavyoona moja imepoa wanaibua mpya mpaka ifike 2020 skendo bado zipo na zinaendelea kuibuliwa.
 
magufuli ni mwanasiasa na anajua akili za watz maskini watanzania kila ngoma ipigwayo wao wanakatika. hahahah ati juzi anajifanya kutaka kulia leo anacheka nao only in africa
Watanzania jambo likifanywa na Rais hulishabikia sana hata kama hilo jambo limewahi kufanywa na wengine mara 100, wapo tayari kusahau vilio vya Wapinzani tokea miaka ya 90 lakini wameshabikia uamuzi wa mwaka 2017 wakati walipaswa kuzuia mapema.wana CCM wengi IQ zao ni ndogo kama wabunge wao wa ndiyoooooo....
 
Hivi ni waliambiwa walipe au wakae mezani wapitie taarifa zote?
Wajinga ni walioshangilia juzi.

Jamani...haya mambo hayaendeshwi kwa siasa bali facts.
Na facts ni kwamba tulishasaini nao mikataba mibovu.
Nini kifanyike sasa? Ilitakiwa bunge libadili vifungu vibovu na kandamizi vya sheria ya madini kabla ya serikali na viongozi wake wakuu kutuletea hili sinema.

Mnaotegemea Noah sijui nini sahauni,hakuna trillions 100+ zitakazolipwa wala nini.
 
Migodi haijataifishwa na hakuna ishu za kupelekana mahakamani. Kwa hiyo makubaliano ilikuwa ni mojawapo ya Azimio kutokana na taarifa ya pili ya Tume iliyoongozwa na Prof Ossoro. Kuna tofauti zimegundulika hivyo lazima zitapatiwe ufumbuzi. Bila Magufuli kuunda hizo Tume hawa Mabeberu wangeendelea kutupiga na kamwe wasingetuambia kama wanatupiga.

Kitendo cha Barick kukubali kukaa mezani ni hatua kubwa kwetu baada ya kuwastukia na kuwachana live bila chenga. Acacia /Barrick wamekubali fasta makubaliano ili kulinda hisa zao zisizidi kuporomoka.

Serikali inatakiwa kupitia Sakata hili isiwaonee haya Makampuni Nyonyaji na inabidi Sheria na Mikataba ipelekwe Bungeni ili kuondoa vipengele vilivyowekwa kuyafaidisha haya Makampuni na badala yake Bunge letu Tukufu lipitishe vipengele vyenye maslahi mapana ya Taifa na hapa Political Ideology zetu tuziweke pembeni kwa muda.
 
Nyie ndo maana mliitwa WAPUMBAVU na MALOFA,yule Mzungu Proff John katoa na mfano wa Dominican Republic na Saudi Arabia ambapo kampuni zao zililalamikiwa kimikataba na wanaenda wakalipana na kuweka mikataba ya 50℅ by 50℅,hamkusikia?,

akaendelea mbele na kusema kama iliwezekana huko inashindikana nini hapa?,hata tusipolipwa fidia ila tukawa tunapata 50℅ mnajua tutapata fedha nyingi kiasi gani?,haki ya Mungu mkiendelea kupinga kila kitu 2020 mtachemka vibaya sana,wananchi sio wajinga kama mnavyodhani,2020 hazungushi mtu mikono hewani kinyumbu nyumbu.
 
Hivi ni waliambiwa walipe au wakae mezani wapitie taarifa zote?
Wajinga ni walioshangilia juzi.

Jamani...haya mambo hayaendeshwi kwa siasa bali facts.
Na facts ni kwamba tulishasaini nao mikataba mibovu.
Nini kifanyike sasa? Ilitakiwa bunge libadili vifungu vibovu na kandamizi vya sheria ya madini kabla ya serikali na viongozi wake wakuu kutuletea hili sinema.

Mnaotegemea Noah sijui nini sahauni,hakuna trillions 100+ zitakazolipwa wala nini.
Hulali? Au unavutavuta mida ya Daku? Nimetuma salamu kwa shemeji kule kwenye Uzi wake mpya operation za kijasusi zilizofanikiwa, umepata?
 
Nyie ndo maana mliitwa WAPUMBAVU na MALOFA,yule Mzungu Proff John katoa na mfano wa Dominican Republic na Saudi Arabia ambapo kampuni zao zililalamikiwa kimikataba na wanaenda wakalipana na kuweka mikataba ya 50℅ by 50℅,hamkusikia?,akaendelea mbele na kusema kama iliwezekana huko inashindikana nini hapa?,hata tusipolipwa fidia ila tukawa tunapata 50℅ mnajua tutapata fedha nyingi kiasi gani?,haki ya Mungu mkiendelea kupinga kila kitu 2020 mtachemka vibaya sana,wananchi sio wajinga kama mnavyodhani,2020 hazungushi mtu mikono hewani kinyumbu nyumbu.

..50/50 leo wakati wameshaiba kwa miaka 15++.

..halafu kuna mgodi unafungwa ndani ya miaka 3.

..wananchi watawahukumu 2020 kwa kukubali kujadiliana na wezi wa rasilimali zao.
 
Migodi haijataifishwa na hakuna ishu za kupelekana mahakamani. Kwa hiyo makubaliano ilikuwa ni mojawapo ya Azimio kutokana na taarifa ya pili ya Tume iliyoongozwa na Prof Ossoro. Kuna tofauti zimegundulika hivyo lazima zitapatiwe ufumbuzi. Bila Magufuli kuunda hizo Tume hawa Mabeberu wangeendelea kutupiga na kamwe wasingetuambia kama wanatupiga.
Naambiwa hii si tume ya kwanza kutoa pendekezo linalofanana na hili.
Kitendo cha Barick kukubali kukaa mezani ni hatua kubwa kwetu baada ya kuwastukia na kuwachana live bila chenga. Acacia /Barrick wamekubali fasta makubaliano ili kulinda hisa zao zisizidi kuporomoka.
Hivi tuliingia nao kwenye mkataba bila kukaa nao mezani! Samahani sana, nilikuwa sijui hili.
Serikali inatakiwa kupitia Sakata hili isiwaonee haya Makampuni Nyonyaji na inabidi Sheria na Mikataba ipelekwe Bungeni ili kuondoa vipengele vilivyowekwa kuyafaidisha haya Makampuni na badala yake Bunge letu Tukufu lipitishe vipengele vyenye maslahi mapana ya Taifa na hapa Political Ideology zetu tuziweke pembeni kwa muda.
Bunge lipi ndugu yangu, hili hili au tusubiri Bunge lijalo!
 
Jambo la msingi ni kuwa maendeleo ya yatakayokuwa yanajili mezani tuhabarishwe na muafaka ukifikia pia tujulishwe kama ilivyokuwa kwenye kutoa taarifa za makinikia kwa kuombwa tuangalie na kusikia kwenye luninga na internet.
 
magufuli ni mwanasiasa na anajua akili za watz maskini watanzania kila ngoma ipigwayo wao wanakatika. hahahah ati juzi anajifanya kutaka kulia leo anacheka nao only in africa

Hampendi.kuona watu wakipatana.
Kwa heri.
 
Naambiwa hii si tume ya kwanza kutoa pendekezo linalofanana na hili.

Hivi tuliingia nao kwenye mkataba bila kukaa nao mezani! Samahani sana, nilikuwa sijui hili.

Bunge lipi ndugu yangu, hili hili au tusubiri Bunge lijalo!
Kitu cha msingi ni utekelezaji wa mapendekezo ya Tume na kama Tume za awali walitoa pendekezo hilo basi waliona umuhimu wake sababu tunahitaji wawekezaji lakini iwe win to win. Mkuu watu waliokaa mezani na kufanya makubaliano hapo awali walitanguliza maslahi yao binafsi na maslahi ya Mabeberu badala ya maslahi ya Taifa.

Makubaliano ni hatua ya kwanza kuondoa utata ikishindikana ni kupelekana mahakamani.

Kama JPM katoa ahadi ya kupeleka Sheria na Mikataba Bungeni ili ipitiwe upya anamaanisha kweli atapeleka sababu ni mtu ambaye akisema ni lazima atatekeleza. Sasa kama ni bunge hili la Bajeti au bunge lijalo hilo ni suala la muda.
 
..50/50 leo wakati wameshaiba kwa miaka 15++.
Hapana, walikuwa hawaibi, walikuwa wanachukua kwa ruhusa yetu ila sasa tumezinduka! Walioapa kutulinda na mali zetu tumeamua na sisi kuwalinda na waliofaidi tunatafuta muafaka nao...ujanja kupata si kuwahi!
..halafu kuna mgodi unafungwa ndani ya miaka 3.
Usisahau ule msemo wa watu kutafuta shuka wakati kumekucha...kwa Watanzania hii si ajabu, ndivyo tulivyo.
..wananchi watawahukumu 2020 kwa kukubali kujadiliana na wezi wa rasilimali zao.
Thubutu! Wananchi wa wapi, Tanzania? Hawa wanaopiga vigelegele serikali ikitafuta maridhiano na wezi wanaodai kuwaibia, hiyo sahau. Unakumbuka tulivyowabembeleza wezi wa EPA? Kikwete aliwalilia akiwaomba warudishe japo kidogo walichoiba akitoa ahadi ya kuwasamehe na kweli mwaka 2010 tukamzawadia Kikwete awamu ya pili!
 
Taarifa ya Ikulu; 'wamekubali kulipa na wamekubali kujenga kiwanda cha kuchengua (smelter)
Wao Barrick wanasema walikuja kusaidi kuweka mambo ya mazungumzo sawa!

Nina shaka sana na kinachoendelea, muda utatuambia
 
..50/50 leo wakati wameshaiba kwa miaka 15++.

..halafu kuna mgodi unafungwa ndani ya miaka 3.

..wananchi watawahukumu 2020 kwa kukubali kujadiliana na wezi wa rasilimali zao.
Magufuli angeonekana mjanja angeenda kwenye mafuta na gesi.
Ila huku alipogusa ataondoka na fedheha.
Hakuna atakaemlipa hata trilion 1.
 
Back
Top Bottom