Martini Am
Member
- Mar 7, 2016
- 9
- 6
Kwa majuma kadhaa sasa, baadhi ya Wanasiasa wamekuwa na hoja ya kuhusu Mkataba Tata wa Lugumi .
Kwa namna ambavyo walikuwa wakizungumza ni kana kwamba tayari wana uhakika kwamba kampuni ya Lugumi haikutekeleza mkataba. Baadhi ya watu walidai kwamba kampuni ya Lugumi ilipata Tenda kinyume na sheria.
Jana kupitia Taarifa ya Habari ya Clouds Tv niliona habari kwamba PAC imeunda kamati ya watu tisa kwa ajili ya kuzunguka nchi nzima kufanya Uchunguzi ili kubaini kama Lugumi hakutekeleza Mkataba.
Hii inaonyesha kwamba;
1. Kampuni ya Lugumi ilifuata kanuni na sheria zote kupata Tenda hiyo. Kama ingekuwa hawajafuata sheria, kusingekuwa na haja ya kufuatilia utekelezaji wa wa mkataba huo ( ingekuwa ni kitendo cha kuchukua hatua dhidi ya waliohusika katika Mkataba huo )
2. haikuwa sahihi kwa baadhi ya wajumbe kutoka PAC na wanasiasa wengine kutangaza kwamba "watakula sahani moja na Lugumi". Kula sahani moja ina maana walikuwa na ushahidi tayari ; kama ni hivyo kazi ya uchunguzi wa siku 30 kuanzia kesho ina mantiki gani?