Sakata la Lissu: Mawakili wa serikali wajipanga kukata rufaa kesho

These guys are not serious!!!
Kukataa rufaa mtu asipewe dhamana ambayo ni haki yake???
Au wanaendelea kutaka kuonyesha kutokujua sheria?

Kwa mwenendo huu inaonekana wao watumishi wa serikali wakishirikiana na jeshi la polisi wako mstari wa mbele kutaka matamshi ya uchochezi wanayo dai yana mdhalilisha Mh Rais yaendelee kusikika kwa kila mtu.
Kwa maana nyingine wao ndio wanao mtukanisha Mh Rais kwa sasa.
Lissu alisha ongea yakapita . Wanatakiwa waache ili upepeo upite.
Hiyo ni simple logic na ni ushauri usio hitaji malipo.
 
Serkali inatumia kodi zetu vibaya
Wanahangaika na mambo ya kijinga wakati huduma zinadorora
Lakini naona kama wanatafuta experience.
Maana kushindana na Mh Lissu na kibatala unapata vitu muhimu kisheria ambavyo hawakusoma darasani.
Kama hawajui kwamba Tanzania tunafuata sheria za Uingereza wao wanatuletea mifano ya makaburi wa Africa kusini huoni sasa wamesoma jambo hapo?
 
Kwa kweli ni vizuri serikal ikaendelea na mambo mengine kwa sababu huyu tundulisu ......anajua nini anafanya ....ifike sehemu watanzania tuache unafki
 
Mpenda sifa asiyejaribiwa anahagaika na lissu utadhani ilani yao ilisema umshughulikie lissu
Nadhani wamechanganyikiwa kwa sababu wanapeleka vitu vingi kwa wakati mmoja Mara kuhamia Dodoma,ooooh Mara watumishi hewa,Mara kutengeneza reli ya standard gauge,Mara kununua ndege,Mara sukari,Oooooh Mara ukusanyaji wa kodi sasa wanaona km wanapoteza Momentum hawajielewi waanzie wap na waishiee wap bora wapambane na Lisu kutafuta momentum tena
 
Mi nafikiri wangekaa wakaona wanafunguaje kesi juu ya mikataba tata inayoitafuna serikalini, hii habari ya kukimbizana na Lissu inawashushia hadhi zao, Tanzania tuna mambo mengi ya kufanya kuimarisha uchumi,hela yenyewe ngumu, tukodi wanakotubana Nako ndio wanamzungushia kutoka singida hadi dar.........kha!
Ikishafika hapo hutawaona, wao wanahangaika na wapinzani tu, hivi kuna faida gani ya kuwa na watu kama hawa katika taifa letu?
 
Mawakili wa Serikali washikana uchawi,wajipanga kukata rufaa kesho.

Chanzo:TanzaniaDaima la leo.

Mzalendo la jana tarehe 07/08/2016,nalo liliripoti kuwa dhamana ya Lissu kupingwa hivyo unganisha dots hapo upate habari kamili.
Mambo yasijefanana na Jaji aliye mhukumu mmiliki wa TP MAZEMBE .Jaji alilazimishwa kutoa hukumu kwa mambo ya kisiasa kitu ambacho kimesababisha Jaji kuishi mafichoni.Siasa na mambo ya kitaalamu yatachafua nchi hii.
 
Ili kupambana na Lissu kwenye sheria serikali haina budi kumkodi Masumbuko Lamwai.
...
Hata upeleke Law School yote pale wakiongozwa na Fatou Bensouda (Enough 101: Meet Fatou Bensouda, Chief Prosecutor of the International Criminal Court | Enough Project), yule mshitaki mkuu wa ICC, kuna kanuni moja rahisi sana: DAIMA ASIMAMAYE KATIKA KWELI NI MSHINDI no matter how long it will take. Kama Serikali inasimamia ukweli basi ushindi ni wake na kama Lissu yuko katika kweli ataendelea kuwa mshindi.
 
Mi nafikiri wangekaa wakaona wanafunguaje kesi juu ya mikataba tata inayoitafuna serikalini, hii habari ya kukimbizana na Lissu inawashushia hadhi zao, Tanzania tuna mambo mengi ya kufanya kuimarisha uchumi,hela yenyewe ngumu, tukodi wanakotubana Nako ndio wanamzungushia kutoka singida hadi dar.........kha!

Wana JF,
Kusema kweli kwa hali tuliyo nayo sasa Tanzania inasikitisha na ina huzunisha sana!
Huyu Magufuli anafikiri HAPA KAZI TU maana yake ni KUDHIBITI WAPINZANI!!!This is absolutely non-sense! Hii slogan ya Hapa Kazi Tu ni maigizo ambayo ukiya tazama kwa jicho la tatu ni USANII mtupu ambao ndani yake hakuna VISION wala MISSION! Badala ya kushughulikia issues za kiuchumi ili kuwaletea maendeleo Watanzania yeye ameanza kuhangaika na Wapinzani as if hiyo ndiyo ilikuwa sera au agenda ya CCM wakti akiomba kura!!!!!
Kwa akili ya Magufuli( a Chemist, who knows nothing about Politics,Economy,Business or enterprenuiship) yeye anadhani kila kitu kitaenda KWA KULAZIMISHA,MABAVU,HASIRA NA CHUKI BILA KUFUATA KATIBA,SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI HII!
Hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu ambayo enzi za Baba wa Taifa Tanzania iliungana na kusaidia vyama vya Siasa katika nchi mbalimbali Africa na dunia nzima kwa ajili ya Ukombozi wa waliokuwa wakitawaliwa na kuteseka chini ya Tawala DHALIMU,za KIDIKTETA, KIKOLONI NA KIMABAVU! Leo tumepata Rais anayetaka kuturudisha katika enzi za mkolony! Shame on JPM and his government!!!!!
 
Ukishaelewa kwamba duniani kuna watu wamejaliwa karama fulani zaidi ya wenzao, huwezi tena kujisumbua kumfuatilia mtu kama Tundu Lissu kwenye uwanja wa sheria.

Serikali inazidi kujiaibisha kama kweli itakata rufaa. Tundu Lissu sio mtu wa kawaida na hakuna mwanasheria wa serikali anaweza kwenda naye jino kwa jino. Na wanasheria wenyewe wanajuana kwamba jamaa yule hatari sema tu utakuwa ubishi wa kuwalamba makalio watawala kwamba na wao wanafanya kazi, ila hakuna lolote.
Kukata rufaa ni haki kama haki zingine hakuna cha kujiabisha wala nini.
 
Hata na mimi pia nina wasiwasi na tuendako. Miezi ya awali nili post thread hapa JF kumsifia rais anavyopambana na uzembe. Lakini sasa ananitia wasiwasi kumuona anajihusisha na mambo yasiyo na umuhimu kama kufungia mikutano ya wapinzani, kuhamia Dodoma n.k.

Halafu pia kama kweli yeye anapenda maendeleo anatakiwa amuondoe huyu "RC" wa Dar es salaam, hata sioni anachokifanya.
Nchi hii ni ya ajabu sana
Hivi inazuia mkutano ya kisiasa ili iweje?

Nimshauri magufuli akubali kukosolewa la sivyo hakuna atachofanya
 
WASICHOFAHAMU NI KWAMBA MIHIMILI IMEAMUA KUJISIMAMIA...........Amri kutoka 'juu' wamezichoka, zinadhalilisha taaluma zao...........na hapa lazima wale za uso.
BADO KIDOGO KUNA WATU TUTAUNGANA MBELE YA SAFARI. Usiombe kuona waoga wakikusanya uoga wao pamoja na kuamua kuutupa jalalani......mbaya zaidi jalala ukiwa ni wewe.
 
Back
Top Bottom