Sakata la Lissu "Handle with care"

Sakata la Lissu "Handle with care"

Feedback

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Posts
7,988
Reaction score
4,514
Tumeshuhudia siku za hivi karibuni polisi imekuwa ikihangaika na matamshi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu kuwa rais Magufuli ni "dikteta uchwara".

Hebu tujiulize nini hasa lengo la hili sakata kwa pande zote zinazovutana.

Haiwezekani mtu unakamatwa/shitakiwa kwa kosa fulani halafu unarudi kutenda kosa lilelile tena nje tu ya jengo la mahakama.

Binafsi naona ni kama kuna mtego fulani kwa chama tawala utakaohitimishwa September 1, chini ya Operation UKUTA.

Nafikiri nia hasa ya Chadema ni ama Lissu afungwe au awekwe ndani ipatikane sababu ya kufanikisha operation hiyo.

Lengo lingine nafikiri ni kukiweka chama kwenye headline kwa muda mrefu na kufifisha ziara za mtukufu rais zinazoendelea. Kumbuka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Mh. Mbowe alisema wanauwezo wa kufanya siasa ndani na nje ya bunge.

Lengo lingine "nafikiri" ni mkakati wa kumuandaa mtu atakayeaminiwa na kuonewa huruma na jamii (Mandela style) ili labda baadaye aje kugombea cheo kikubwa ndani au nje ya chama.

Lengo lingine nafikiri ni kuionyesha dunia na watanzania kwa ujumla kuwa serikali ya Magufuli ni ya kidikteta inayovunja katiba yake ili kuthibitisha maneno ambayo yamekuwa yakisemwa na chama hicho.

Serikali ijue Chadema ni chama kikubwa kina uzoefu mkubwa kina wanasiasa wazoefu na wakongwe, hivyo kina mikakati yake na mbinu mbalimbali za kujiimarisha. Hivyo, serikali isilichukulie sakata la Lissu kama jambo dogo, should handle this issue with care.

Kumbuka moto huanza na cheche moja baadaye husambaa na kuunguza msitu mzima.

Haya ni mawazo yangu binafsi.
 
Huwa wanamuita Mbowe kwa kebehi kuwa ni DJ, lakini ukweli ni kuwa kama ni DJ basi ni wa ukweli kwani kila muziki anaouweka Ccm wanaucheza na serikali wananengua mpaka basi.

Kamusi iko wazi kuhusu neno Dikteta jee wanashindwa kulisoma na kujua tafsiri yake kuwa sio matusi?

DJ Mbowe shusha CD za kutosha kwa mtindo wa bandika bandua wacheze mpaka nyonga zifyatuke.

Leo ni Lissu, kesho CD nyingine, hivyo hivyo hadi sept1 hapo ndio unashusha remix
 
Tumeshuhudia siku za hivi karibuni polisi imekuwa ikihangaika na matamshi ya Mbunge wa Iramba Mashariki Mh. Tundu Lissu kuwa rais Magufuli ni "dikteta uchwara".

Hebu tujiulize nini hasa lengo la hili sakata kwa pande zote zinazovutana.

Haiwezekani mtu unakamatwa/shitakiwa kwa kosa fulani halafu unarudi kutenda kosa lilelile tena nje tu ya jengo la mahakama.

Binafsi naona ni kama kuna mtego fulani kwa chama tawala utakaohitimishwa September 1, chini ya Operation UKUTA.

Nafikiri nia hasa ya Chadema ni ama Lissu afungwe au awekwe ndani ipatikane sababu ya kufanikisha operation hiyo.

Lengo lingine nafikiri ni kukiweka chama kwenye headline kwa muda mrefu na kufifisha ziara za mtukufu rais zinazoendelea. Kumbuka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Mh. Mbowe alisema wanauwezo wa kufanya siasa ndani na nje ya bunge.

Lengo lingine "nafikiri" ni mkakati wa kumuandaa mtu atakayeaminiwa na kuonewa huruma na jamii (Mandela style) ili labda baadaye aje kugombea cheo kikubwa ndani au nje ya chama.

Lengo lingine nafikiri ni kuionyesha dunia na watanzania kwa ujumla kuwa serikali ya Magufuli ni ya kidikteta inayovunja katiba yake ili kuthibitisha maneno ambayo yamekuwa yakisemwa na chama hicho.

Serikali ijue Chadema ni chama kikubwa kina uzoefu mkubwa kina wanasiasa wazoefu na wakongwe, hivyo kina mikakati yake na mbinu mbalimbali za kujiimarisha. Hivyo, serikali isilichukulie sakata la Lissu kama jambo dogo, should handle this issue with care.

Kumbuka moto huanza na cheche moja baadaye husambaa na kuunguza msitu mzima.

Haya ni mawazo yangu binafsi.

hivi lisu ndo nani mbona mna mpa kiki bure , ndo maana hata media hazimpi umaarufu wowote KUTOA habari zake
 
Shiiiiii....acha usiwaamshe!! Siasa ni mchezo mchafu, ni mbinu, ni "sawa na system with high dynamics" and wasipotumia akili watakuwa busy kuzuia maandamano na kutumia hela nyingi kwa mambo ambayo hayana tija. Na wahashindwa kuelewa kwenye huu mchezo wana CCM pia wamo...tena wanafadhili kwa nguvu zote chini kwa chini.
 
Wacha wacheze. Hata gadafi alianza ivi ivi na mwisho wake ulikuwa mbaya. Damu zinazomwagwa kila mwaka zinamlilia Mungu mbele ya kiti chake cha enzi. Ipo siku ghadhabu ya Mungu itawaka na hakuna atakae zuia na waonevu wote watalia na kusaga meno
Fafanua ni damu gani zinazomwaga kila mwaka chini ya utawala wa Magufuli.
 
Wapinzani wanasema mikutano na maandamano ni haki yao kikatiba na kisheria. Sasa rais angetuambia yeye anazuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa kwa sheria ipi?
Kuna kitu kinaitwa Presidential Decree.
 
Back
Top Bottom