Sakata la kufukuzwa watanzania katika machimbo nchini Msumbiji

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,590
3,626
Zimekuwepo taarifa za kufukuzwa kwa Watanzani ambao ni sehemu ya WACHIMBAJI wadogo wadogo katika mgodi...

Zilikuwepo taarifa za matendo yanayofanywa na Raia (hasa wa Kitanzania) wakituhumiwa kuendesha matukio ya kihalifu kama uporaji, ubakaji na hata mauaji dhidi ya Raia wengine toka nchi mbalimbali...

Wanaelezwa g mauaji hata pale mtanzania mwenzao anapotokea kupata kipande cha MADINI...

Ni baada ya Mauaji ya na vurugu za muda mrefu wanazo fanya dhidi ya RAIA toka nchi kama Zambia, Uganda, Ethiopia na hata kwa wazawa, jambo lililo onesha kuwa SERIKALI ya Mozambique wameshindwa kuchukua hatua SITAHIKI kumlinda mchimbaji mkubwa (MZUNGU)...

Kulikuwepo malalamiko na ushauri wa muda mrefu toka kwa MUEKEZAJI/MCHIMBAJI mkubwa akiomba kuondoa wachimbaji wote wadogo na kuwaunga pamoja wachimbaji wenzao jambo ambalo lingewapelekea kujipatia ajira na kuingia katika payroll...

Ziliibuka vurugu kubwa za mapigano kati ya wachimbaji wadogo na wale wa MUEKEZAJI hatua iliyopelekea ASKARI kuingilia kati na kuanza zoezi la KAMATA KAMATA....

Katika dhahama hiyo walikamatwa wachimbaji wote wasio RASMI wakiwemo ETHOPIANS kwa wingi na WATANZANIA ambao ndio kama walikuwa walengwa wakubwa.....

Ni kweli wengi wao hakuna aliepita nyumbani kuaga...yalitumika magari ya machimboni, yale yanayotumika kubeba mchanga katika zoezi la kuwakusanya na kuwapeleka wahusika wote MPAKANI.....

Kilichoniuma ni kuona uvunjifu wa haki za binaadamu, udhalilishaji na kupelekea kukosekana uvumilivu wa DIPLOMASIA uliofanywa na hawa ASKARI wa MSUMBIJI......

Ningetoa wito kwa viongozi na hasa BALOZI wa Tanzania MOZAMBIQUE kufuatilia swala hili na kuweza kusaidia wale walionyanganywa mali, fedha na hati zao za kusafiria walau waweze kusaidiwa kwani naamini wengi wao watakuwa wamekwama MPAKANI....

Huu ni wito wangu...
 
1487019347795.jpg
 
Nlijua hii kitu itatokea na kuwa tatizo kubwa...Mimi binafsi nshatemeshwa hela huko sidadi

Ova
 
Nchi zote zina Shelia zake za kuishi kufanya Kazi lkn akuna MTU mwenye kibari cha kuchimba madini waludi waje kujipanga watanzania wengine wanaendelea kuishi km kawaida maeneo mengine
 
Zimekuwepo taarifa za kufukuzwa kwa Watanzani ambao ni sehemu ya WACHIMBAJI wadogo wadogo katika mgodi...

Zilikuwepo taarifa za matendo yanayofanywa na Raia (hasa wa Kitanzania) wakituhumiwa kuendesha matukio ya kihalifu kama uporaji, ubakaji na hata mauaji dhidi ya Raia wengine toka nchi mbalimbali...

Wanaelezwa g mauaji hata pale mtanzania mwenzao anapotokea kupata kipande cha MADINI...

Ni baada ya Mauaji ya na vurugu za muda mrefu wanazo fanya dhidi ya RAIA toka nchi kama Zambia, Uganda, Ethiopia na hata kwa wazawa, jambo lililo onesha kuwa SERIKALI ya Mozambique wameshindwa kuchukua hatua SITAHIKI kumlinda mchimbaji mkubwa (MZUNGU)...

Kulikuwepo malalamiko na ushauri wa muda mrefu toka kwa MUEKEZAJI/MCHIMBAJI mkubwa akiomba kuondoa wachimbaji wote wadogo na kuwaunga pamoja wachimbaji wenzao jambo ambalo lingewapelekea kujipatia ajira na kuingia katika payroll...

Ziliibuka vurugu kubwa za mapigano kati ya wachimbaji wadogo na wale wa MUEKEZAJI hatua iliyopelekea ASKARI kuingilia kati na kuanza zoezi la KAMATA KAMATA....

Katika dhahama hiyo walikamatwa wachimbaji wote wasio RASMI wakiwemo ETHOPIANS kwa wingi na WATANZANIA ambao ndio kama walikuwa walengwa wakubwa.....

Ni kweli wengi wao hakuna aliepita nyumbani kuaga...yalitumika magari ya machimboni, yale yanayotumika kubeba mchanga katika zoezi la kuwakusanya na kuwapeleka wahusika wote MPAKANI.....

Kilichoniuma ni kuona uvunjifu wa haki za binaadamu, udhalilishaji na kupelekea kukosekana uvumilivu wa DIPLOMASIA uliofanywa na hawa ASKARI wa MSUMBIJI......

Ningetoa wito kwa viongozi na hasa BALOZI wa Tanzania MOZAMBIQUE kufuatilia swala hili na kuweza kusaidia wale walionyanganywa mali, fedha na hati zao za kusafiria walau waweze kusaidiwa kwani naamini wengi wao watakuwa wamekwama MPAKANI....

Huu ni wito wangu...
Hii habari nimeipenda kwa kiasi fulani ila mleta mada ungeiongezea nyama kidogo ikiwemo source ya hiyo habari kuliko kuleta nusunusu
 
mtoa habari kaleta habari ya uongo, watanzania hawafanyi matukio unayo yasema wewe hiyo co kweli Nina ushahidi na hicho kitu
 
Hii habari nimeipenda kwa kiasi fulani ila mleta mada ungeiongezea nyama kidogo ikiwemo source ya hiyo habari kuliko kuleta nusunusu
SOURCE....Mimi ni moja ya shuhuda...na kwa taarifa zaidi wasiliana na Afisa mkuu uhamiaji kizuizi cha MTWARA (namaanisha mpaka wa Tanzania na Msumbiji)

Kwa kifupi nimepishana na hiyo OPERATION....

Sikutoa hii habari kumfurahisha mtu, ila ni baada ya kuiona MICHUZI BLOG imetolewa kwa MAPUNGUFU....
 
Ni kweli watanzania wanafanya uhalifu na sio kwa raia wengine tu bali wanafanyiana hata wao kwa wao, warudi tu ili tulinde mahusiano mazuri ya nchi zetu
 
Tatizo wanalazimisha sheria ifuate wanavyotaka wao kwani kila Nchi ina sheria na taratibu zake
Wao ni wachimbaji wadogowadogo wa Madini hilo eneo wanalo ng'ang'ania lipo chini ya mwekezaji halali ambaye amekabidhiwa na Serikali kwahiyo wao wanalazimisha kuchimba eneo hilo hilo
Kwani huko Tanzania hakuna migodi?
Nendeni Bulyamhuru mukachimbe musitake kutuharibia sisi huku tupo na tunaishi kama vile Tuko Nyumbani TANZANIA
 
Waache ujinga,warudi kwa mashetani wenzao,Kwanini wanakimbia kuishi kama mashetani.
 
Jana kupitia vyombo vya habari niliona watanzania waliokuwa wanaishi nchini Msumbiji wakiwa wamefukuzwa na kurudishwa nchini huku wengi wao wakiwa wamenyang'anywa hati zao za kusafiria na kila kitu walicho nacho.

Kwa namna ambavyo kiongozi wa Idara ya uhamiaji wa tanzania alielezea tukio lile, ni kuwa utaratibu haukufuatwa na majirani zetu hao wa Msumbiji.

Mimi binafsi sikutegemea hata siku moja kuwa nchi ya Msumbiji ingeruhusu lile litokee kutokana na ukweli kuwa watatanzia tumekuwa wenye mchango mkubwa wa kuwepo kwa taifa la msumbiji.

Watanzania tunakila sababu ya kutafakari aina ya siasa zetu pamoja na mahusiano na majirani zetu, inawezekana majirani zetu hawaelewi siasa zetu za miaka hii.

Inawezekana watanzania tunatatizo ambalo hatujaligundua au hatutaki kuligundua. Wiki zilizopita watanzania kadhaa walikamatwa nchini Malawi kwa kile kilichoelezwa kuwa wameingia kupeleleza pamoja na sababu nyingi nzuri zilizoelezwa na kituo cha kutetea haki za binadamu lakini Tanzania sasa tujue wazi kuwa kuna kitu na hatuko vizuri na majirani zetu.

Ni vizuri tujitathmini mapema ili chokochoko hizi zisije zikatuingiza kwenye hatari.
 
Kwakweli hata mi nimeshangaa sana,umeongea vyema tujitazame upya kuna kitu hakiko sawa
 
Nahisi itakuwa ni hii biashara haramu. Watz tumenuka duniani
 
TUJIREKEBISHE KWA STYLES TUNAYOCHAGUA KUISHI ,PIA HATA KUJIVUA NGUO HADHARANI SISI WENYEWE KWA MATENDO YETU YA NDANI NI SABABU.NDIO MAANA NAMPONGEZA SANA RAIS JPM KUMTEUA KAMISHNA KTK TUME YA MADAWA YA KULEVYA.
LEO HII TAARIFA ZETU WENYEWE TULIZOTOA KWA VYOMBO VYETU NA VYOMBO VYA NJE, ZINATUDHURU!
MTAMBUE KILA NCHI INALO TATIZO HILI,LAKINI BUSARA HUTUMIKA KTK KULIMALIZA KWA MITINDO AMBAYO HAITANIATHIRI SANA TAIFA AU HAITATIA DOA HESHIMA YA NCHI.
LEO TUNAONEKANA SIO WATANZANIA WALE WAJAMAA WALIOKUWA WAKATI WA MWL NYERERE ENZI ZA MAPAMBANO YA UHURU BALI WATANZANIA MABEPARI.
(Tujitathmini upya kama TAIFA )
 
Tatizo lingine watanzania hatuna mazoea ya kuheshimu sheria na taratibu. Utaona mtu mzima na elimu yake lakini bado hataki kufuata utaratibu au sheria. Sasa tukienda nchi za nje tunapata matatizo kutokana na mazoea. Nitatoa mfano, kuna nchi kama Rwanda mtu yeyote hata awe mgeni haruhusiwi kupita eneo lililopandwa majani aina ya ukoka. Nilazima upite eneo la njia ya miguu. Sasa watanzania tumezoea kukatisha hata maeneo yaliyopandwa maua na ni vigumu watu kuacha tabia. Tulienda Rwanda tulikamatwa kwa kuvuka barabara eneo lililopandwa majani na maua ikawa aibu. Sasa nchi nyingine wakiona ni wageni msioelewa wanapata sababu ya kuwatimua
 
Back
Top Bottom