quarz: hoja zako ni nzito. Lakini unategemea nini kama vijana waote mliosoma vizuri ama mnaogopa kuingia katika siasa au mnaona mlango pekee wa kuingia katika siasa ni CCM? Hii inaniumiza sana kichwa. Wewe niambie leo hii vichwa kama Mwanakijiji, Mkandara, quarz, Augustino Moshi, Kichuguu, Sam, Mzee ES n.k. vingeingia katika chama kimoja cha upinzani hasa CHADEMA, siasa zetu zingebadilika mno na tugeweza kupata mwanga katika mambo mengi yanayotusumbua. Otherwise, tutaendelea kulialia tu na wafanya maamuzi wataendelea kuwa walewale akina Nungwi. Juzi nilikutana na dada moja kutoka Ghana katika mkutano fulani London, yule dada anamjua sana JK akaniambia alishangaa aliposikia amekuwa rais. yeye anasema kama JK ameweza kuwa Rais anaamini anybody in TZ anaweza akawa president! It was really embarassing to me!