Sakata la Kampuni ya Lugumi: IGP na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani watupiana mpira

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,316
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,Ernest Mangu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani,Jaji Meja Jenerali Projest Rwegasira, wameripotiwa kutupiana mpira kuhusu kuhusu ni nini kimesababisha kutokuwasilishwa kwa mkataba huo kwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali siku ya jana.

Mangu anasema: "Iliyoagizwa ni wizara kwahiyo siwezi kuzungumza kwa niaba ya wizara na hiyo siku Katibu Mkuu alikuwepo."

Alipoulizwa kwamba,kwa upande wao wamekwishawasilisha mkataba huo wizarani alisema: "Kwani anayesaini mkataba si katibu mkuu,hivyo wasaliana na ofisi ya katibu mkuu au waziri."


Gazeti lilimtafuta Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambae alisema: "Ninaomba uwasiliane na IGP."

Baada ya kauli hiyo,Tanzania Daima lilimweleza kwamba IGP Mangu amesema atafutwe Katibu Mkuu kwani siku hiyo alikuwapo(siku walipokutana na kamati ya PAC) ambapo Rwegasira alisema: "IGP atoe maelezo siyo Katibu Mkuu,kwani hata siku hiyo tulipokwenda aliyekuwa anajibu maswali ni IGP siyo mimi."

Alipoulizwa ulipo mkataba huo,Katibu Mkuu huyo alisema: "Hata kama ofisi yetu ndiyo inasaini mkataba,lakini suala hilo lilielekezwa moja kwa moja kwa IGP ambae alikuwa anajibu."

"Mimi nategemea aliyeambiwa kupeleka ni IGP,huu ni uelewa wangu na kama alijua hana angeeleza kwamba hana ili kamati ya Bunge itoe maelezo ya jinsi ya kumsaidia kuupata." aliongeza Rwegasira.

Baada ya ufafanuzi huo wa Rwegasira,Tanzania Daima lilimtafuta kwa mara nyingine IGP Mangu ambae hakupatikana kwani simu yake ya kiganjani ilikuwaa ikiita bila kupokelewa.

Chanzo: Tanzania Daima

Bora ya yule mama!
 
Kama IGP alimsimamisha afisa manunuzi wake, mbona la kupeleka documents anasita? Au nae anamjengo mmoja kati ya hizo 40? Kwa katubu mkuu bado mgeni sana kwenye hiyo Wizara. Haelewi historia ya hicho kitu.
Kuja mambo hapo.
 
Magu kivipi tena wewe fisi wakati ngoma ipo chini ya kamati ya Bunge? Au mnataka mpewe fursa ya kusema Magu dikteta anaingilia Bunge?
Likishajadiliwa Bungeni mapendekezo/maazimio ya Bunge hupelekwa wapi kwa ajili ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na wahusika kuchukuliwa hatua?

Acha kukurupuka kama hujui kaa kimya.
 
Yale yale. Sinema imeanza....... Chezeya mwana wa mfalme. Vita vya Mafisadi ni ngumu sana kwa Magufuli. Sidhani huo mkataba utapatikana
watatupiana huo mpira wee hadi upotee.wanajua sio wao wanaotakiwa waucheze.si mnajua orodha ya waliotajwa kwenye huo ufisadi? hapa ndipo tutaona ubavu wa bunge kuwajibisha chombo cha serikali.
Kwamba, katika kupishana labda kuna aliye sahau akaondoka na mkataba kwa bahati mbaya?
 
Back
Top Bottom