Sakata la gesi ya Mtwara: Hatuchezi ngoma za mafisadi?

chicco

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
748
Reaction score
254
Kuna maswali mengi sana yananisumbua kutokana na sakata zima la gesi kwamba isafirishwe au isisafirishwe kuja Dar.Kuna wengine wanavyosema kwenye thread mbalimbali unaona kabisa kwamba hawajui kile wanachokitetea.

Kuna mmoja anasema haiwezekana mtudanganye kwamba mtajenga viwanda huku Mtwara wakati mitambo ya kuprocess hiyo gesi ambayo ndo raw materials iko Kinyerezi? Anachofahamu ni kuwa gesi yote inakuja Dar,huyu elimu tu inahitajika but sidhani kama ni makusudi au ni bahati mbaya haya makundi mawili yanaziba masikio kusikiliza hoja za upande wa pili ili kujenga maelewano.

Swali langu ni je,tunacheza ngoma za mafisadi?naamini as long as gesi inachelewa kuja Dar au kufikia maelewano mengine tutaendelea kutumia mafuta mazito kuzalisha umeme.

Huko ndiko watu wanakopiga hela ndefu kiulainiiii...maisha ni kuchagua,na kwa hili yatupasa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi,otherwise acheni tuendelee kubishana wakati twaendelea kuliwa since wajinga ndo waliwao!!!?ni mtazamo tu!!!
 
Nchi isha uzwa kwa USA, UK and China, tusubiri kuwekwa kwenye makambi kupitia vita ya wenyewe kwa wenyewe itakayo chochewa na hao wageni, mtwara wameanza.
 
Kwa hili acha tu wanaopiga Hela kiulaini kifisadi kwenye Mafuta Mazito wapige lakini Gesi isiende DSM.Viongozi wetu hawana Mawazo ya kumkomboa Mtanzania wao wanawaza madili tu.Hata hili ni Dili la watu wachache na Hela zimeshahifadhiwa Uswisi.Wanyama wanasafirishwa wazimawazima kwenda Nje ya Nchi hakuna anaejali,Tembo wanauwawa,Dhahabu,Almasi,Tanzanite na kila aina ya Maliasili zinachotwa Viongozi wakiangalia tu,sasa unataka tuendelee kuwaamini?.Naunga Mkono hoja ya Wananchi kuzuia Maliasili popote pale zilipo Mpaka tutakapopata Viongozi wenye Maono.Jiulize,toka Maliasili zetu zianze kuchotwa mbona Maisha hayaboreki?Tuwe na Msimamo kwamba zilizokwishachotwa zilitolewa kafara lakini zilizobaki tuzilinde hata ikibidi tufe kwa faida ya Watoto na Wajukuu zetu.
 
Mbona hamtuelezi athari za kiuchumi na kijamii zitakazotokea kama mtambo wa kufua umeme utajengwa mtwara na then kuingizwa kwenye grid ya taifa. Bomba lililopo sasa kutoka songo songo likatumika kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwanda vya dar?
 
kuna maswali mengi sana yananisumbua kutokana na sakata zima la gesi kwamba isafirishwe au isisafirishwe kuja dar.kuna wengine wanavyoccoment kwenye thread mbalimbali unaona kabisa kwamba hawajui kile wanachokitetea.kuna mmoja anasema haiwezekana mtuambie kuwa mtudanganye kwamba mtajenga viwanda huku mtwara wakati mitambo ya kuprocess hiyo gesi ambayo ndo raw materials iko kinyerezi?anachofahamu ni kuwa gesi yote inakuja dar,huyu elimu tu inahitajika but sidhani kama ni makusudi au ni bahati mbaya haya makundi mawili yanaziba masikio kusikiliza hoja za upande wa pili ili kujenga maelewano.swali langu ni je,tunacheza ngoma za mafisadi?naamini as long as gesi inachelewa kuja dar au kufikia maelewano mengine tutaendelea kutumia mafuta mazito kuzalisha umeme.huko ndiko watu wanakopiga hela ndefu kiulainiiii...maisha ni kuchagua,na kwa hili yatupasa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.otherwise,acheni tuendelee kubishana wakati twaendelea kuliwa since wajinga ndo waliwao!!!?ni mtazamo tu!!!

Kama vile sijakupata sawasawa!
Kitu ambacho wanakusini na watanzania wote wazalendo wa nchi hii wanachopigania ni rasilimali za taifa ziwanufaishe kweli wananchi wote hasa kuanzia pale zinakopatikana.

Kitendo cha serikali kung'ang'ania kusafirisha gesi kutoka mtwara hadi DSM, sio tu kuwa sio kitendo cha kiungwana kwa wananchi na watanzania waishio mikoa ya kusini bali pia ni kutaka kuwafanya wananchi wa huko kuwa masikini wa milele.
Ili kuichangamsha mikoa ya uko kiuchumi ni vema gesi hiyo ikachakatwa huko huko iankopatikana, ili kuwapa fursa wananchi wa huko angalau kupata ajira ambayo naamini athari yake itakuwa ni kubwa mno.

Kuchakatwa kwa gesi huko kutaifanya bandari ya mtwara kufufuka, mzunguko wa fedha kuongezeka, wawekezaji kuelekea huko na hata huduma za kijamii zitaboreka.Pia maeneo ya huko yatakua!

Lengo la serikali kuipeleka gesi DSM ni kutumika kuzalisha umeme kkule kinyerezi.Kinyerezi ni power plant mpya, ambayo inaweza kujengwa pia mtwara badala ya hapo ikiwa na lengo lile lile na hatimaye umeme huo uingizwe kwenye gridi ya taifa.Kwa nini ili linakuwa gumu kwa serikali?Hivi wanashindwa kuelewa kuwa kwa kufanya hivyo kutaokoa fedha inayotaka kutumika kujenga bomba?
Haya wanayafahamu ila tu wameamua kuzifanya ngumu shingo zao ili hatimaye lengo lao la kupiga ile dili ya 500 ifanikiwe,si vinginevyo.

Suala la ufisadi katika sekta ya nishati ni matokeo ya dili za namna hii, na kwa kuwa walifanikiwa huko Watanzania sasa wameamua kukataa ujuha wa namna hiyo katika sekta ya gesi.

Kitendo cha kusema kuwa kufanya hivyo ni kucheza ngoma ya mafisadi ili waendelee kupiga hela kwenye ununuzi wa mafuta mazito, ni kutaka kuwarudisha nyuma watanzania katiaka harakati za kuzilinda rasilimali za taifa na kupambana na mikakati ya hovyo ya serikali ya CCM ya uhujumu wa taifa letu.
Hizo ni mbinu zenu tu ili hatimaye wananchi walegee ili nyie mkamilishe dili lenu la kifisadi

GESI KWANZA!
 
Mbona hamtuelezi athari za kiuchumi na kijamii zitakazotokea kama mtambo wa kufua umeme utajengwa mtwara na then kuingizwa kwenye grid ya taifa. Bomba lililopo sasa kutoka songo songo likatumika kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwanda vya dar?

so unashauri mitambo iliyopo sasa ubungo ihamishiwe mtwara then ijengwe njia ya umeme itakayoleta huo umeme kwenye gridi ya taifa?do u think hiyo process itachukua muda gani?gharama zake kiasi gani?do we have plan B ya kuzalisha umeme wakti tunahamisha mitambo?fafanua pls
 
Kwa hili acha tu wanaopiga Hela kiulaini kifisadi kwenye Mafuta Mazito wapige lakini Gesi isiende DSM.Viongozi wetu hawana Mawazo ya kumkomboa Mtanzania wao wanawaza madili tu.Hata hili ni Dili la watu wachache na Hela zimeshahifadhiwa Uswisi.Wanyama wanasafirishwa wazimawazima kwenda Nje ya Nchi hakuna anaejali,Tembo wanauwawa,Dhahabu,Almasi,Tanzanite na kila aina ya Maliasili zinachotwa Viongozi wakiangalia tu,sasa unataka tuendelee kuwaamini?.Naunga Mkono hoja ya Wananchi kuzuia Maliasili popote pale zilipo Mpaka tutakapopata Viongozi wenye Maono.Jiulize,toka Maliasili zetu zianze kuchotwa mbona Maisha hayaboreki?Tuwe na Msimamo kwamba zilizokwishachotwa zilitolewa kafara lakini zilizobaki tuzilinde hata ikibidi tufe kwa faida ya Watoto na Wajukuu zetu.

nasapoti kulinda maliasili za taifa.pia natambua kuwa kuna makosa tayari yamefanyika,sasa je tuache tu hayo makosa yaliyofanyika yaendelee tu bila kuyarekebisha wakati yanatumika kutuhujumu?swali langu la msingi,je tuache mitambo ya symbion,iptl etc iendelee kutumia mafuta mazito wakati tayari kuna gesi?unashauri umeme uzalishwe kule mtwara then uingizwe kwenye gridi ya taifa,ipo huko mtwara?cha kushangaza ni kuwa,watu wanazungumzia ajira as if hivyo viwanda vikijengwa huko wataajiriwa tu bila kuangalia vigezo,au may be mnazungumzia vibarua?mkubali mkatae soko kubwa la gesi kwa hapa tz lipo dar so itakuja tu
 
Kuna maswali mengi sana yananisumbua kutokana na sakata zima la gesi kwamba isafirishwe au isisafirishwe kuja Dar.Kuna wengine wanavyosema kwenye thread mbalimbali unaona kabisa kwamba hawajui kile wanachokitetea.

Kuna mmoja anasema haiwezekana mtudanganye kwamba mtajenga viwanda huku Mtwara wakati mitambo ya kuprocess hiyo gesi ambayo ndo raw materials iko Kinyerezi? Anachofahamu ni kuwa gesi yote inakuja Dar,huyu elimu tu inahitajika but sidhani kama ni makusudi au ni bahati mbaya haya makundi mawili yanaziba masikio kusikiliza hoja za upande wa pili ili kujenga maelewano.

Swali langu ni je,tunacheza ngoma za mafisadi?naamini as long as gesi inachelewa kuja Dar au kufikia maelewano mengine tutaendelea kutumia mafuta mazito kuzalisha umeme.

Huko ndiko watu wanakopiga hela ndefu kiulainiiii...maisha ni kuchagua,na kwa hili yatupasa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi,otherwise acheni tuendelee kubishana wakati twaendelea kuliwa since wajinga ndo waliwao!!!?ni mtazamo tu!!!

Mimi kama ningekuwa natoka MT au Lindi ningeomba kujitoa ndani ya muungano wa TZ ili kunusuru utajiri wetu. Hii nchi inaendeshwa kiusanii sana kunufaisha watu wachache ndani ya serikali. Fika Mwadui ama Kahama Shy town (Shinyanga), kule huwezi amini kuwa wale watu ndiyo wenye alimasi na dhahabu, maji hadimu, na miji yenyewe tu iko hovyo hovyo kama Kigoma.
 
Wala usiwe na haraka ya kuanza itumia gesi ya mtwara.... Tena ni heri hata ikionekena muafaki ni wa kimagumashi hata wasitishe kabisa kwa muda... tukumbuke kuwa gesi na mafuta ndio chanzo cha mifarakano ktk nchi nyingi duniani Tuache harakaharaka na tuweke mikakati itayo tunufaisha wote
 
walisucrifice maliasili yao kwa ajili ya nchi yao.sasa ndo maana nashauri yawepo makubaliano kwamba sawa gesi inatoka sisi tunapata nini?inaweza kuwa for the time being wakapewa ruzuku or something?but kusema tusubiri hadi viwanda vijengwe huko mtwara na maendeleo yapatikane ndo gesi itoke huo ni ubinafsi uliopitiliza mipaka!!!!kwa hiyo mnatwambia watanzania wenzenu kuwa tuendelee na umeme wa mgawo kwa kutegemea mafuta mazito hadi siku mtakayojengewa viwanda na madudu mengine yote mnayotaka????selfishness inawasumbua na mtakufa na umaskini wenu!!!mbona wanamtwara hamkuchangishana pesa za kufanya utafiti wa hayo mafuta mmeacha tumetumia fedha za watanzania wote then yamepatikana ndo mnakuja kutupangia namna ya kuyatumia!!!!au na sisi tuanzishe movement kudai pesa zetu zilizotumika kuyatafiti hayo mafuta?mtatulipa?
 
kitu kimojawapo tulichofurahia upatikanaji wa gesi ni kuondokana na mgawo wa umeme.jamani gesi inakuja kuzalisha umeme ambao unatunufaisha wenyewe,kwa nini tunapinga?hayo madini wanayachukua kwenda nayo kwao kuyaprocess tumenyamaza!!!!tanzanite imeajiti wahindi wengi huko kwao,tumenyamaza!!!gesi ikija dar si bado itaajiri watanzania wakiwepo hao wamakonde?umeme si utatumika na watanzania wote?viwanda vikinufaika na mfumuko wa bei ukapungua si tutanufaika watanzania wote?so why ubinafsi huu jamani?sasa badilisheni hayo madai yenu semeni mitambo yote ya umeme iletwe huko mtwara/tanzania na mtuambie sisi wakimbizi kuwa tutapataje umeme wakati mitambo inahamishwa!!!
 
walisucrifice maliasili yao kwa ajili ya nchi yao.sasa ndo maana nashauri yawepo makubaliano kwamba sawa gesi inatoka sisi tunapata nini?inaweza kuwa for the time being wakapewa ruzuku or something?but kusema tusubiri hadi viwanda vijengwe huko mtwara na maendeleo yapatikane ndo gesi itoke huo ni ubinafsi uliopitiliza mipaka!!!!kwa hiyo mnatwambia watanzania wenzenu kuwa tuendelee na umeme wa mgawo kwa kutegemea mafuta mazito hadi siku mtakayojengewa viwanda na madudu mengine yote mnayotaka????selfishness inawasumbua na mtakufa na umaskini wenu!!!mbona wanamtwara hamkuchangishana pesa za kufanya utafiti wa hayo mafuta mmeacha tumetumia fedha za watanzania wote then yamepatikana ndo mnakuja kutupangia namna ya kuyatumia!!!!au na sisi tuanzishe movement kudai pesa zetu zilizotumika kuyatafiti hayo mafuta?mtatulipa?

Ni mali yao lazima wailinde. Pia watu wa Shinyanga ilibidi wafanye the same kuhusu alimasi na dhahabu zao, je kuna tatizo hapa? Ikumbukwe kwamba japo tunasema miradi hii ni kwa ajili ya kusaidia watanzania ni uwongo. Hili ni dili viongozi wamejiwekea ruzuku zao na vizazi vyao vya baadaye. Msishangae baada ya miaka 5 ijayo mkasikia Ridhiwani ndo waziri anayeshughulikia masuala ya gesi kwenda Kisarawe na almasi ya Mwadui kusafishwa Bagamoyo. Subirini tu.
 
kama ulivyo sema ..... sekta ya madini tunachakachuliwa live live... unataka na hii ya mafuta iwe kama ya madini? Unaweza shangaa tukaanza zalisha hayo mafuta na bado bei ilawa haishikiki.... Tujipange ankooo.... Hawa mafisadi watatutafuna wazima wazima chicco
 
Last edited by a moderator:
nasapoti kulinda maliasili za taifa.pia natambua kuwa kuna makosa tayari yamefanyika,sasa je tuache tu hayo makosa yaliyofanyika yaendelee tu bila kuyarekebisha wakati yanatumika kutuhujumu?swali langu la msingi,je tuache mitambo ya symbion,iptl etc iendelee kutumia mafuta mazito wakati tayari kuna gesi?unashauri umeme uzalishwe kule mtwara then uingizwe kwenye gridi ya taifa,ipo huko mtwara?cha kushangaza ni kuwa,watu wanazungumzia ajira as if hivyo viwanda vikijengwa huko wataajiriwa tu bila kuangalia vigezo,au may be mnazungumzia vibarua?mkubali mkatae soko kubwa la gesi kwa hapa tz lipo dar so itakuja tu

Bw,Chicco Makosa yaliyokwisha fanyika hayawezi kurekebishwa harakaharaka kama unavyofikiri na hasa ukiangalia aina ya viongozi tulionao.Cha Msingi ni Kudhibiti Maliasili ambayo haijafisadiwa na baadaye ndio tupambane kwenye hizo zilizochukuliwa.Sio vizuri kupambana Vita Mbili kwa wakati Mmoja.Kuhusu Mitambo ya Symbion,IPTL etc,Kwanza hii Mitambo ni ya Kifisadi haifai kabisa kuendelea kutumika Nchini,Siungi mkono aina yoyote ya kuifanya iendelee kuwepo.Kuhusu Mitambo kutokuwepo Mtwara ni swala la Ujenzi tu.Kama vile mlivyoamua kujenga Mitambo Kinyerezi(DSM) na Mtwara inaweza kujengwa vilevile.Ama kuhusu Ajira hilo halina tatizo,Watu watoke popote pale hata nje ya Nchi waje kuajiriwa.Ni sawa tu na DSM watu wanatoka sehemu mbalimbali kuja kutafuta ajira.Watu wa Mtwara watafaidika kwa kitu kinachoitwa "MULTIPLIER EFFECT".Viwanda mbalimbali vitavutia vingine,Nyumba za kupangisha zitapata soko zaidi,Sehemu za Burudani zitaongezeka,Ajira zisizo za kitaalamu zitaongezeka mf.saluni,mama lishe,grocery,ulinzi etc.Kwa ujumla faida ni nyingi mno kuliko hasara.
 
kama ulivyo sema ..... sekta ya madini tunachakachuliwa live live... unataka na hii ya mafuta iwe kama ya madini? Unaweza shangaa tukaanza zalisha hayo mafuta na bado bei ilawa haishikiki.... Tujipange ankooo.... Hawa mafisadi watatutafuna wazima wazima chicco

nakubaliana na wewe mkuu.labda hamjanielewa,shida yangu ni plan ya muda mfupi huu tulionao,tunatatuaje tatizo la upungufu wa umeme/mgao wa umeme na wakati huo huo kuondokana na kutumia mafuta mazito ambayo ni gharama kubwa?ni haki kwa nchi kuendelea na gharama hizo eti tu hadi wanamtwara wajengewe viwanda?upotoshaji mwingine,kinyerezi ipo kama kituo cha kufikishia gesi kwa ajili ya mitambo ambayo ipo tayari kama symbion na iptl,sawa ni plant mpya lakini utofauti wake na hiyo wanayosema ijengwe mtwara ni kuwa dar mitambo ipo tayari wakati mtwara utatakiwa kujenga plant pamoja na mitambo.
 
Last edited by a moderator:
Ni mali yao lazima wailinde. Pia watu wa Shinyanga ilibidi wafanye the same kuhusu alimasi na dhahabu zao, je kuna tatizo hapa? Ikumbukwe kwamba japo tunasema miradi hii ni kwa ajili ya kusaidia watanzania ni uwongo. Hili ni dili viongozi wamejiwekea ruzuku zao na vizazi vyao vya baadaye. Msishangae baada ya miaka 5 ijayo mkasikia Ridhiwani ndo waziri anayeshughulikia masuala ya gesi kwenda Kisarawe na almasi ya Mwadui kusafishwa Bagamoyo. Subirini tu.

mkuu watz karibia wote ni wezi,tunatofautiana viwango nenda maofisini huko ndo utalitambua hili.hv nchi ikiingia kwenye mgao wa umeme anaathirika nani zaid?huyo riz atawasha genereta wewe mwenzangu na mie?au haukuwepo wakati wa mgao mkali wa umeme?msipinge tu tuambieni watz tunaondokaje kwenye mgao wa umeme kwa sasa?
 
Kama vile sijakupata sawasawa!
Kitu ambacho wanakusini na watanzania wote wazalendo wa nchi hii wanachopigania ni rasilimali za taifa ziwanufaishe kweli wananchi wote hasa kuanzia pale zinakopatikana.

Kitendo cha serikali kung'ang'ania kusafirisha gesi kutoka mtwara hadi DSM, sio tu kuwa sio kitendo cha kiungwana kwa wananchi na watanzania waishio mikoa ya kusini bali pia ni kutaka kuwafanya wananchi wa huko kuwa masikini wa milele.
Ili kuichangamsha mikoa ya uko kiuchumi ni vema gesi hiyo ikachakatwa huko huko iankopatikana, ili kuwapa fursa wananchi wa huko angalau kupata ajira ambayo naamini athari yake itakuwa ni kubwa mno.

Kuchakatwa kwa gesi huko kutaifanya bandari ya mtwara kufufuka, mzunguko wa fedha kuongezeka, wawekezaji kuelekea huko na hata huduma za kijamii zitaboreka.Pia maeneo ya huko yatakua!

Lengo la serikali kuipeleka gesi DSM ni kutumika kuzalisha umeme kkule kinyerezi.Kinyerezi ni power plant mpya, ambayo inaweza kujengwa pia mtwara badala ya hapo ikiwa na lengo lile lile na hatimaye umeme huo uingizwe kwenye gridi ya taifa.Kwa nini ili linakuwa gumu kwa serikali?Hivi wanashindwa kuelewa kuwa kwa kufanya hivyo kutaokoa fedha inayotaka kutumika kujenga bomba?
Haya wanayafahamu ila tu wameamua kuzifanya ngumu shingo zao ili hatimaye lengo lao la kupiga ile dili ya 500 ifanikiwe,si vinginevyo.

Suala la ufisadi katika sekta ya nishati ni matokeo ya dili za namna hii, na kwa kuwa walifanikiwa huko Watanzania sasa wameamua kukataa ujuha wa namna hiyo katika sekta ya gesi.

Kitendo cha kusema kuwa kufanya hivyo ni kucheza ngoma ya mafisadi ili waendelee kupiga hela kwenye ununuzi wa mafuta mazito, ni kutaka kuwarudisha nyuma watanzania katiaka harakati za kuzilinda rasilimali za taifa na kupambana na mikakati ya hovyo ya serikali ya CCM ya uhujumu wa taifa letu.
Hizo ni mbinu zenu tu ili hatimaye wananchi walegee ili nyie mkamilishe dili lenu la kifisadi

GESI KWANZA!

Nimesoma hii article Jamie forum
 
mkuu watz karibia wote ni wezi,tunatofautiana viwango nenda maofisini huko ndo utalitambua hili.hv nchi ikiingia kwenye mgao wa umeme anaathirika nani zaid?huyo riz atawasha genereta wewe mwenzangu na mie?au haukuwepo wakati wa mgao mkali wa umeme?msipinge tu tuambieni watz tunaondokaje kwenye mgao wa umeme kwa sasa?

Mgao wa umeme ni dili la viongozi wa Tanesco kwani wanakula dili ili genereta zao zinunuliwe na kujinufaisha wao wenyewe na familia zao. Hii nchi ingekuwa na kiongozi makini anayefunga/kunyonga viongozi waadilifu mbona tungekuwa mbali. Oneni Kagame anavyofanya Rwanda, sie raisi wetu anatuchekea tu kila kukicha. Mgao wa umeme ni makusudio ya vigogo wa tanesco lile ni dili linaloeleweka. Wana Mtwara washikilie tu mali yao.
 
Back
Top Bottom