Sakata la escrow laanika uchi wa Tanzania

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
Juzi bunge lilimaliza mjadala wa kujadili sakata ambalo limetikisa nchi la escrow.

Mjadala huu umeiacha tanzania ikiwa uchi bila nguo kutokana na yaliyojiri katika mjadala. uchi huu unatokana na mambo yafuatayo.

1. Kitendo cha mahakama kukubali hoja ya kuzuia bunge kujadili hoja hiyo na kutoa amri ya kutosikilizwa kwa shauri kinatudhalilisha watanzania. hii ilikuwa kesi ndogo sana ambayo hata wanafunzi wa shule za msingi wangeweza kuitolea hukumu kwa kuangalia haki iko wapi na kama wote mlalamikaji na mlalamikiwa wana haki ni haki gani inatawala nyingine baina ya haki ya wengi na wachache.

2. Kitendo cha baadhi ya wabunge na mawaziri kusimama kutetea vitendo vilivyofanywa inazua maswali na kutufedhehesha watanzania. Mbali na ukweli kuwa yawezekana walikuwa kulikuwa na msukumo wao kufanya hivyo kwani inasemekana kuna kuna mgao wa fedha umegawiwa kwa watu walioficha majina sasa kweli kuna haja ya kujiuliza hawa ni kina nani au mjadala wenyewe umewaweka wazi. mjadala ulibainisha kila aliyejadili yuko upande gani kama ni wa wananchi kutetea mali zao au ni wa mafisadi kutetea wanaoiba mali za umma. hivi hawa viongozi walikuwa bungeni au kama ni waziri amekuwa waziri kwa tiketi gani? je anajitambua au tumejenga mifumo ya watu kupewa madaraka bila kujua wanamtumikia nani.

Waziri anasimama amekasirika kabisa mpaka anatukana kisa eti mtu aliyeghushi nyaraka, aliyekwepa kodi, aliyechukua pesa ambayo si yake kwa maana bila kufanya ukokotoaji upya na kubaini kama kama fedha yake yeye ni kiasi gani ndiyo hiyo tu achukue na kabla ya hilo fedha hiyo si yake wanataka apelekwe mahakamani.

Waziri anasimama na kudai kumpeleka mtu huyu mahakamani kwa makosa ya kufoji nyaraka, kukwepa kodi, kushiriki katika vitendo ambavyo vinaashiria kuwapa rushwa watendaji wa serikali lazima isubiri mapitio ya kesi ya madai alifunguliwa mtuhumiwa na hivyo matokeo ya kesi hiyo ndiyo serikali itaamua cha kufanya.

Hivyo yawezekana matokeo hayo ingawa hayahusu makosa haya ya jinai lakini akishinda kesi ya madai basi ni kusafishwa pia makosa ya jinai haya ambayo inatakiwa apelekwe mahakamani na mahakama ndio ikadhibitishe kama ana hatia na imhukumu.

Waziri anawaagiza watu waliopokea fedha ambazo bado zinaashiria kuwa fedha haramu kama rushwa kulipa kodi. Hivi kweli na rushwa inalipa kodi au kwanza tuchunguze kama ni fedha halali na kama ni halali ndio ilipe kodi na kama ni haramu hawa hawatakiwi kulipa kodi bali washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukimbia kulipia kodi fedha hizi yaweza kuwa njia ya kutakatisha fedha hizi na tukajikuta tunaendeleza kufanya kitu ambacho tunakipiga vita.

Nashindwa kutambua haswa hapa tatizo ni nini lakini mambo kadhaa yawezekana.

1. Rushwa yaweza kusababisha mkanganyiko huu. Lakini 2 hii yaweza kuwa taswila ya elimu yetu.

Ukichukua mijadala ya debate zetu za sekondari za upande unaopinga na upande unaotetea kwa maana kama uko upande unaopinga mada husika haijalishi kinachoongolewa kina ukweli kiasi gani utabaki kupinga tu hivyo wapo yawezekana ambao wanadhani hoja ni serikali kujitetea hivyo watatafuta jinsi ya kufanya utetezi wa kuwa against bunge.

Hivyo walijadili mada wakidhani kuna pande mbili kwa maana ya bunge na serikali. Mimi nasema waliojadili kwa mantiki hii hawafai kuwa viongozi na najiuliza walipataje uongozi kwa maana kiukweli hapa kulikuwa na makundi mawili mafisadi na wananchi ambao wananchi walikuwa wakitetewa na vyombo vyao viwili yaani serikali na bunge.

Serikali ina wajibu wa kufanya lakini inaposhindwa kufanya ni bunge sasa kuhihoji hapa umefanya nini ? kwa nini huyu amefanya hivi na ukakaa kimya kama ni tatizo dogo unamuagiza akampige kibao aliyehusika lakini kama ni tatizo kubwa ni bunge kuwajibisha serikali nzima.

Lakini hapa ni wazi tuna watendaji wasiotambua kuwa wanatumikia wananchi hivyo wanafanana watoto wengi wanaokaa na walezi wao, mara nyingi unakuta watoto hawa au ndugu wanakaa nyumbani wanahudumiwa kila kitu lakini fadhila zao ni kwenda kukaa na majirani kuwasema vibaya walezi wao. Unajiuliza huyu unayekaa naye kumsema mlezi wako anakusaidia nini wakati nyumbani unakula na kunywa na kulala.

Kama jamii tunawajibu wa kuwakumbusha hawa majukumu yao na kwangu mimi nafikiri ni jukumu la tume ya maadili pia kuwachukulia hatua watumishi wa umma na viongozi wanaoonyesha misimamo ya wazi ya kutetea maovu katika jamii.

Kwa naibu waziri wa fedha msimamo wake ulikuwa sahihi yeye alisema swala linalomhusu la kodi ila kila waziri anayehusika alitakiwa kutoa kauli ya wizara yake kuhusu swala hili.

Waziri wa sheria au mwanasheria mkuu wa serikali walitakiwa kutoa kauli zao kuhusu mtizamo wa sheria kuhusu swala hili na nini kifanyike.

Hatuwezi kuwalazimisha waseme nini ila wanachokisema ndicho kinaweza kuwabainisha wako kwetu wananchi au kwa mafidi na ama tuwaunge mkono kwa mapendekezo yao au tuwawajibishe kwa misimamo yao.

3. kitendo cha bunge kutotambua mamlaka yake mpaka wakavutana mda mrefu ni cha kufedhehesha.

4. kitendo cha serikali kutunga maneno ya maagizo wanayotakiwa kuagizwa na bunge ni cha kusikitisha.

5. kitendo cha watuhumiwa kutumika kutunga maamuzi ya bunge ya kuwawajibisha kinachekesha kama sio kuwaacha wananchi mdomo wazi.

Yote haya yanajumuisha swali moja tu kuwa hivi utumishi wa umma Tanzania kweli kuna maadili yake? Na maadili haya tunayalindaje au tunayasimamia vipi?

Kimsingi sakata hili linaonyesha tuko uchi kabisa tunahitaji kuvaa nguo.
 
Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,826
2,000
Suala la kuruhusu serikali itoe mapendekezo dhidi ya yale ya kamati ya PAC in udhaifu wa Spika. Tangu lini anayeagizwa kazi ya kufanya akajipangia kazi ya kufanya? tukisema bunge la Tanzania sio huru tutakuwa tunakosea?
 
kimtizamo mimi nadhani ilikuwa ni sahihi pengine serikali kupewa nafasi ya kutoa maoni yao. lakini walichokifanya ni upuuzi ambao kwa mtizamo wangu aliyeleta mapendekezo haya na yeye alitakiwa kuwajibishwa mara moja.

swala la aibu limefanyika, baadhi ya watendaji wa serikali wamehusika badala ya serikali kuonyesha u seriousness na kuonekana kukazia mapendekezo ya kamati na kuonyesha kama walipitiwa na watendaji wachache wakafanya hayo. bado serikali wakaonyesha kilichofanyika ndio msimamo wa serikali na wakawa wanapindisha mapendekezo ya kamati kwa maana badala ya kukazia wakawa wanaregeza mapendekezo ya kamati.

hivi kweli hawa wako serious?
 
Kipoporu

JF-Expert Member
May 2, 2013
351
170
Suala la kuruhusu serikali itoe mapendekezo dhidi ya yale ya kamati ya PAC in udhaifu wa Spika. Tangu lini anayeagizwa kazi ya kufanya akajipangia kazi ya kufanya? tukisema bunge la Tanzania sio huru tutakuwa tunakosea?

All in all Bi Mkora ameonesha umahiri wa kuwakutanisha CCM na Ukawa na kutoka na solution kuliko alivyofanya Mbulumundu Samwel SITTA. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpe
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,210
2,000
Watu waovu, wezi wamejipenyeza na kukabidhiwa madaraka makubwa katika mihimili mikuu ya dola, serikalini, mahakamani na hata bungeni.
Kusafisha uozo huu siyo kazi rahisi, hata hivyo inawezekana kama wananchi walio wengi watawachukia na kupambana na mafisadi!
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
All in all Bi Mkora ameonesha umahiri wa kuwakutanisha CCM na Ukawa na kutoka na solution kuliko alivyofanya Mbulumundu Samwel SITTA. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpe

hapa lazima ujue historia ya jambo hili, swala hili lilisemwa mda mrefu lakini halikukubalika kwa maana kwetu tanzania halikuwa tatizo. uchumi wa watanzania unategemea kwa kiasi kikubwa ufisadi au dili lakini lilikuwa tatizo pale tu wafadhili walipogoma kutoa fedha na hivyo msimamo hapa ulikuwa ni kuhakikisha kunapatikana hoja ya kuwaridhisha wafadhili.

alafu kesho tunawalaumu wafadhili hao kuwa wanatupa masharti! kwa mwendo huu kweli sisi ni wa kulaumu au kushukuru wafadhili kutumia misaada kusimamia maadili yetu
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,473
2,000
Kama ni uchi, si wa tanzania. Ni uchi wa CCM inayounda serikali!.

Ccm ndiyo imeshindwa kusimamia na kutetea maslahi ya taifa.

Ccm ndiyo imekuwa ya kifisadi na kuongozwa na mfumo fisadi

Ccm ndiyo inayounda serikali ambayo watendaji wake wote kuanzia raisi hawajui majukumu na mipaka yao.

Ccm ndiyo iliyoiba fedha za Escrow kuanzia mwenyekiti hadi watendaji wake.

Ccm ndiyo inayoongozwa kwa misingi ya rushwa. Hakuna kiongozi ccm bila rushwa anzia kwa mwenyekiti wao.

Ccm ndiyo inayounda serikali iliyotunga majibu ya utetezi wa uwongo.

Ccm ndiyo yenye wabunge waliokaa vikao na kupewa rushwa ili watee majizi na wakafanya hivyo.

Ccm ndiyo yenye PM na team yake waliokuwa wakifanya hila kuzuia mjadala wa escrow bungeni.

Ccm ndiyo yenye wabunge mazezeta wasiokuwa na hoja bungeni zaidi ya kuimba taarabu, mipasho kama mashoga na kusubiri kupiga kura. Kura ambazo ni za ccm ndizo zilikuwa zikitetea wizi na majizi.

Ccm ndiyo yenye speaker aliyekuwa anajaribu kupotosha hukumu kwa kujifanya hatakiwi kuiambia serikali nini cha kufanya. Lengo la pretense hii ni kulinda maharamia na interests zake.

Ccm ndiyo waliokuwa wakiongea pumba na uozo kiasi cha ku extend bunge.

AIBU YOTE INAIENDEA CCM BILA UBIA NA MTU YEYOTE!.
 
Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
24,004
2,000
suala la kuruhusu serikali itoe mapendekezo dhidi ya yale ya kamati ya pac in udhaifu wa spika. Tangu lini anayeagizwa kazi ya kufanya akajipangia kazi ya kufanya? Tukisema bunge la tanzania sio huru tutakuwa tunakosea?
kweli mkuu.....
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
Kama ni uchi, si wa tanzania. Ni uchi wa CCM inayounda serikali!.

Ccm ndiyo imeshindwa kusimamia na kutetea maslahi ya taifa.

Ccm ndiyo imekuwa ya kifisadi na kuongozwa na mfumo fisadi

Ccm ndiyo inayounda serikali ambayo watendaji wake wote kuanzia raisi hawajui majukumu na mipaka yao.

Ccm ndiyo iliyoiba fedha za Escrow kuanzia mwenyekiti hadi watendaji wake.

Ccm ndiyo inayoongozwa kwa misingi ya rushwa. Hakuna kiongozi ccm bila rushwa anzia kwa mwenyekiti wao.

Ccm ndiyo inayounda serikali iliyotunga majibu ya utetezi wa uwongo.

Ccm ndiyo yenye wabunge waliokaa vikao na kupewa rushwa ili watee majizi na wakafanya hivyo.

Ccm ndiyo yenye PM na team yake waliokuwa wakifanya hila kuzuia mjadala wa escrow bungeni.

Ccm ndiyo yenye wabunge mazezeta wasiokuwa na hoja bungeni zaidi ya kuimba taarabu, mipasho kama mashoga na kusubiri kupiga kura. Kura ambazo ni za ccm ndizo zilikuwa zikitetea wizi na majizi.

Ccm ndiyo yenye speaker aliyekuwa anajaribu kupotosha hukumu kwa kujifanya hatakiwi kuiambia serikali nini cha kufanya. Lengo la pretense hii ni kulinda maharamia na interests zake.

Ccm ndiyo waliokuwa wakiongea pumba na uozo kiasi cha ku extend bunge.

AIBU YOTE INAIENDEA CCM BILA UBIA NA MTU YEYOTE!.

jamani watanzania tunahitaji kujitambua, yanayofanywa na bunge ni yetu sote watanzania, yanayofanywa na serikali ni yetu sote watanzania.

hapa ni kutafuta dawa ya kutibu. ila kinachonitia shaka katika haya yanayotendeka kama CCM bado wanazidi kukubalika nadhani yanayofanywa ndio hulka yetu kwa maana wapinzani hawataki kuyaanika haya kwa kuhofia kukata miti wanayotegemea kuchuma matunda.

siwahukumu ila napenda sana hoja hizi ndizo zitawale kampeni zetu kama chama mnajipanga vipi kusimamia maadili ya umma, kama chama mnamipango gani ya kuendeleza uchumi, kama chama mna mipango gani ya kulinda rasilimali na maslahi za watanzania.

ila wapo wanaodhani kwa hoja hizi siasa zinakuwa hazilipi hivyo kuzibeba hizo hoja ni bora wao kuacha siasa.

ni jukumu letu wananchi kulazimisha hizi kuwa ajenda za siasa na si majina ya watu kuambiwa majina fulani watagombea, si matusi na vijembe na wala si rangi na mbwembwe za vyama.

tuchague siasa zenye tija
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
Watu waovu, wezi wamejipenyeza na kukabidhiwa madaraka makubwa katika mihimili mikuu ya dola, serikalini, mahakamani na hata bungeni.
Kusafisha uozo huu siyo kazi rahisi, hata hivyo inawezekana kama wananchi walio wengi watawachukia na kupambana na mafisadi!

watu wakiambiwa madaraka ya raisi ni makubwa na yanaweza kumfanya raisi awe dikiteta mambo yenyewe ndiyo haya. tunapendekeza katiba mpya kwa raisi kuteua kila kitu mahakama, mawaziri, wakurugenzi na kadhalika. matokeo yake watu wanaunda mitandao ya uraisi wakipata wanateuana wanashika sekita zote mwisho wa siku hakuna anayemsimamia mwenzake kokote utakokwenda watu walewale wanalindana.
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,473
2,000
ego; umesema sahihi.

Pamoja na hayo, tunahitaji kutambua pia kwamba kinachoongoza nchi ni mifumo. Ukitazama, pamoja na kwamba kikwete hakuwa na sifa za uraisi, lakini mwanzoni alionyesha nia njema. Lakini licha tu ya kukosa support, kwa kuchagua team mbovu ya utendaji, chama chake kimemvuta na kumwondoa kwenye misingi ya uraisi wa Nchi. Completely kikwete hana uwezo wa kuamua na hata akiamua hana uwezo wa kufanya jambo lolote lisiloridhiwa na ccm.

Chama kilichothibitika kwa kuimarisha udanganyifu, rushwa, ufisadi na dharau kwa wananchi, hakina sifa ya kuongoza nchi. Hata kaam kinalazimisha, hakina uwezo wala vigezo vya kutoa kiongozi bora. Hata kingeweka sera na agenda za kampeni, itakuwa ni kuwahadaa Watanzania kwa lengo la kujipati akura na hatimaye kuwatelekeza na kuwaibia kama ilivyo sasa.

Ukiwalazimisha watengeneze agenda, watatengeneza na kila kitu safi, lakini ni nini kitawalazimisha watekeleze hayo wanayoyanadi?

Ni dhahiri mamo makuu mawili, "Utashi" na "Katiba".

Ccm tayari, wala haina mjadala kwamba utashi wa kuleta maendeleo kwa nchi hawana. Hata wakisema, zitakuwa ni nyimbo za kampeni lakini kila mtu ameshafahamu ccm haina nia njema na taifa ndiyo maana wanaua elimu, wanajenga mfumo wa kifalme, wanahamisha raslimali zetu bil auchungu, wanajilimbikizia mali nje ya nchi, uchumi wote mikononi mwa wageni kiasi hata cha kutubeza kwamba tutaishia kuwa madalali hakuna hata mtu wa kukemea uovu huu, pamoj an akuendekeza rushwa na ufisadi.

Ccm, kwa kufanikisha malengo yao hayo, wamechakachua katiba na kuondoa maadili ya viongozi, na kutokutilia maanani maslahi ya taifa kiasi hata cha kuzuia haki za msingi zisihojiwe mahala popote. Hata kama wakiimba ngojera kwenye kampeni, ni nini kitawafanya wawajibike ikiwa katia imeachwa na matundu makubwa makusudi?

Siamini kwamba wapinzani hawataki kuyasema maovu ili nao waje wafuate mkondo uleule. Hapa si kweli hata wewe unajua hilo.

Mara ngapi wapinzani wametishiwa mauti na ccm ka sababu ya kufichua maovu? Mara ngapi wametukanwa kwamba ni waongo, tumbili n.k kwa sabbu tu wanasema wanayoyajua?

Kama wangetaka kuleta utaratibu fisadi ili uwasaidie mbeleni, ni kwa nini hawakuridhia katiba ya kifisadi iendelee ili nao siku moja waje wavune?

Ninaona tofauti kubwa sana kati ya ccm na ukawa. si sahihi kuwajumuuisha wote watanzania hawawezi kujenga nchi, eti kwa kuwa ccm imeshindwa. Si kweli.

Ccm imehsindwa, tuwape wengine waongoze nchi. Nchi ni yetu sote na wala si ya ccm.

Kama mfumo ccm umeoza, bado tuna mifumo mingine inayoweza kuleta mageuzi. ccm wakae kando.

Lakini jambo kubwa tutengeneza katiba itakayolinda maslahi ya taifa si hii inayopendekezwa iliyojaa hila na kinga kwa mafisadi na watawala.

BILA KATIBA SAHIHI, MAENDELEO NI VIGUMU SANA KUPATIKANA. RUSHWA NA UFISADI HAUTAKOMA, DHURUMA UTASHAMIRI NA UMASKINI UTAENDELEA KUTAMALAKI SIKU ZOTE.

jamani watanzania tunahitaji kujitambua, yaonayofanywa na bunge ni yetu sote watanzania, yanayofanywa na serikali ni yetu sote watanzania.

hapa ni kutafuta dawa ya kutibu. ila kinachonitia shaka katika haya yanayotendeka kama CCM bado wanazidi kukubalika nadhani yanayofanywa ndio hulka yetu kwa maana wapinzani hawataki kuyaanika haya kwa kuhofia kukata miti wanayotegemea kuchuma matunda.

siwahukumu ila napenda sana hoja hizi ndizo zitawale kampeni zetu kama chama mnajipanga vipi kusimamia maadili ya umma, kama chama mnamipango gani ya kuendeleza uchumi, kama chama mna mipango gani ya kulinda rasilimali na maslahi za watanzania.

ila wapo wanaodhani kwa hoja hizi siasa zinakuwa hazilipi hivyo kuzibeba hizo hoja ni bora wao kuacha siasa.

ni jukumu letu wananchi kulazimisha hizi kuwa ajenda za siasa na si majina ya watu kuambiwa majina fulani watagombea, si matusi na vijembe na wala si rangi na mbwembwe za vyama.

tuchague siasa zenye tija
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,325
2,000
Watu waovu, wezi wamejipenyeza na kukabidhiwa madaraka makubwa katika mihimili mikuu ya dola, serikalini, mahakamani na hata bungeni.
Kusafisha uozo huu siyo kazi rahisi, hata hivyo inawezekana kama wananchi walio wengi watawachukia na kupambana na mafisadi!

Mkuu lebabu11, ni kweli kwamba mihimili yote ya dola imeonyesha udhaifu mkubwa kwenye sakata la escrow! Pia wanasiasa wetu wameamua kufanya maridhiano ambayo kimsingi ni ya "kufunika kombe mwanaharamu apite"! Kinachohitajika ni kwa wale wananchi wenye uchungu wa kweli na nchi hii na wana access ya data zinaweza kuthibitisha "uhusika" wa "wahusika wa sakata hili" kuzimwaga hadharani kwenye mitandao ya kijamii kwa namna itakayolinda bado usalama wao. Kwa njia hii wataweza "kufunua kombe ili mwanaharamu asipite" kwani atakuwa anaonekana na kila mmoja kwamba ni haramu!
 
sansiro12

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
259
225
Suala la kuruhusu serikali itoe mapendekezo dhidi ya yale ya kamati ya PAC in udhaifu wa Spika. Tangu lini anayeagizwa kazi ya kufanya akajipangia kazi ya kufanya? tukisema bunge la Tanzania sio huru tutakuwa tunakosea?
Hapo tume ya Warioba ilikuwa sahihi. Kugenganisha mihimili ya dora, Mawaziri wasiwe wabunge na Spika asiwe mbunge (kutoa mambo ya niwe wa nani?) na bunge to vet appointment muhimu.
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
Mkuu lebabu11, ni kweli kwamba mihimili yote ya dola imeonyesha udhaifu mkubwa kwenye sakata la escrow! Pia wanasiasa wetu wameamua kufanya maridhiano ambayo kimsingi ni ya "kufunika kombe mwanaharamu apite"! Kinachohitajika ni kwa wale wananchi wenye uchungu wa kweli na nchi hii na wana access ya data zinaweza kuthibitisha "uhusika" wa "wahusika wa sakata hili" kuzimwaga hadharani kwenye mitandao ya kijamii kwa namna itakayolinda bado usalama wao. Kwa njia hii wataweza "kufunua kombe ili mwanaharamu asipite" kwani atakuwa anaonekana na kila mmoja kwamba ni haramu!

hapa naunga mkono kabisa na tunahitaji wanasiasa wa kubeba hoja hizi kwa makini kwa maana wananchi vijijini ukiwaambia akaunti ya escrow hawatakuelewa bali waeleze jinsi nchi inavyopata hasara kwa tunaowatuma kusimamia mali zetu wanavyohongwa na wageni na wakishaonga jinsi tunavyowasaidia kuwaibia wananchi rasilimali, kupandisha gharama za miradi ya maendeleo na kuwafanunulia jinsi ambavyo wizi huu unavyowasababishia umasikini kwani kama umelima mazao wewe ni mkulima wezi kila siku wanaingia shambani wanaiba unadhani wewe mkulima utapata nini?

lakini kama umemuweka ama mlinzi, au msimamizi wa shamba ukagundua nahusika kufanya dili na wezi utamfanya nini? na bila kudhibiti wezi uwaulize kama wanadhani maisha ya wakulima yataboreka? ukifika kwa wafanya biashara hivyo hivyo uwaeleze kwa mifano ya duka ambalo kila siku wezi wanavunja wanaiba kama mwenye duka anaweza kupata faida,

lakini wasisahau kuweka mipango ya ukishazuia wezi utafanya nini ili mali zetu zitunufaishe,

nina uhakika huo ndio ukombozi kwa watanzania, wapatiwe elimu, wapatiwe mipango ya kweli na waamue wenyewe
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
ego; umesema sahihi.

Pamoja na hayo, tunahitaji kutambua pia kwamba kinachoongoza nchi ni mifumo.

kimsingi nchi inatakiwa kuongozwa kwa mifumo, hoja ni mifumo ipi?

mifumo inayotakiwa kuongoza nchi ni mifumo ya kulinda uchumi wa nchi, mifumo ya kulinda maadili ya watendaji wa umma na kila mtu anayeishi katika nchi, mifumo inajenga ustawi wa taifa na wananachi wake.

kwetu sisi tulisinzia wahuni wakaweka mifumo yao ya kifisadi, huwezi kupata uongozi kwa kuwa unafaa bali unapata uongozi kwa sababu unajuana na nani, kila mtu akipata mradi wa kusimamia ni kuhangaika kuweka maslahi yake, kupata huduma za serikali lazima utoe kidogo kama ni fedha aya kama kumruhusu aguse nguo zako za ndani haya.

yote haya hayana tija katika utendaji wa kazi bali kuongeza ufisadi
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,473
2,000
Ninachokiona, katiba yetu ya 1977, ilikuwa mno trusting and dependent on nature. Tuliamini kwamba viongozi wote watakuwa kama Mwalimu na kwamba watu wote watakuwa proactively responsible, honest, accountable and dependable. Tuliposema ujamaa ni imani, tukaamini watanzania wote wanaamini katika misingi ya ujamaa na kwamba hawahitaji kiranja wa kuwahimiza wala chombo chochote cha compliance kama vile mtu anayeamini katika Mungu vile anajitahidi Kuomba kwa Mungu hata akiwa peke yake bila shuruti.

Maadamu dunia imetu prove wrong, ili tufike huko ambako mimi na wewe tunakusema, kwenye uwajibikaji wa kujituma, uadilifu sahihi na uaminifu usio sukumwa kwa nguvu nyingi, tunatakiwa tuanze na katiba.

Tuwe na katiba inayojenga mifumo inayosimamia, kulazimisha na kulinda maendeleo ya uchumi wa nchi, maadili ya watendaji wa umma na umma wa watanzania, ikiwa ni pamoja na ustawi wa taifa zima katika nyanja zote.

Kwa umoja wetu kama watanzania, tukizingatia utaifa na maslahi yetu na vizazi vyetu vijavyo, bila kujali itikadi za vyama, wala dini zetu, wala ukabila ama chochote kinachotutofautisha, kwa pamoja tuachane kabisa na katiba hii pendekezwa ambayo imeandaliwa na inalazimishwa kupita kwa hila. Katiba hii haitufikish popote zaidi ya kuimarisha matatizo ya watanzania.

Rasiimu ya Judge warioba tuiache kama ilivyo,

Tufumue muundo wa bunge la katiba, ili kuwa na bunge lenye watu walio na mchanganyiko bila domination ya kundi lolote. Kwa maana vyama vya siasa viwakilishwe na watu kwa idadi sawa na makundi mengine. Wawakilishwi wa makundi wachaguliwe na makundi husika na kuwe na chombo huru cha kuidhinisha wawakilishi hao na si raisi. Waingie bungeni. Na hawa watu wawekewe sheria kama ya kenya kwamba hawaruhusiwi kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa kisiasa kwa miaka kadhaa.

Wajumbe wa tume ya kukusanya maoni wawe sehemu ya bunge.

Bunge hilo ndilo lianze upya kuchambua rasimu na kutengeneza katiba inayoona, na inayolazimisha compliance kwenye uwajibikaji, uadilifu na uaminifu hata kama mtu binafsi hana utashi.

Ninashindwa kabisa kupata picha ninapoona ccm wakiimba nyimbo za uadilifu na misingi bora ya uongozi, na kujifanya wanalaani ufisadi na rushwa wakati hata kwenye katiba yao wameonyesha kwamba masuala hayo si muhimu kwao.

Tuanze na katiba kwanza ili atakayekwenda kinyume, katiba imbaini kwamba amekiuka katiba na sheria ifanye kazi ya kurekebisha hizo tabia mbofu mbofu!.

kimsingi nchi inatakiwa kuongozwa kwa mifumo, hoja ni mifumo ipi?

mifumo inayotakiwa kuongoza nchi ni mifumo ya kulinda uchumi wa nchi, mifumo ya kulinda maadili ya watendaji wa umma na kila mtu anayeishi katika nchi, mifumo inajenga ustawi wa taifa na wananachi wake.

kwetu sisi tulisinzia wahuni wakaweka mifumo yao ya kifisadi, huwezi kupata uongozi kwa kuwa unafaa bali unapata uongozi kwa sababu unajuana na nani, kila mtu akipata mradi wa kusimamia ni kuhangaika kuweka maslahi yake, kupata huduma za serikali lazima utoe kidogo kama ni fedha aya kama kumruhusu aguse nguo zako za ndani haya.

yote haya hayana tija katika utendaji wa kazi bali kuongeza ufisadi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom