Juzi bunge lilimaliza mjadala wa kujadili sakata ambalo limetikisa nchi la escrow.
Mjadala huu umeiacha tanzania ikiwa uchi bila nguo kutokana na yaliyojiri katika mjadala. uchi huu unatokana na mambo yafuatayo.
1. Kitendo cha mahakama kukubali hoja ya kuzuia bunge kujadili hoja hiyo na kutoa amri ya kutosikilizwa kwa shauri kinatudhalilisha watanzania. hii ilikuwa kesi ndogo sana ambayo hata wanafunzi wa shule za msingi wangeweza kuitolea hukumu kwa kuangalia haki iko wapi na kama wote mlalamikaji na mlalamikiwa wana haki ni haki gani inatawala nyingine baina ya haki ya wengi na wachache.
2. Kitendo cha baadhi ya wabunge na mawaziri kusimama kutetea vitendo vilivyofanywa inazua maswali na kutufedhehesha watanzania. Mbali na ukweli kuwa yawezekana walikuwa kulikuwa na msukumo wao kufanya hivyo kwani inasemekana kuna kuna mgao wa fedha umegawiwa kwa watu walioficha majina sasa kweli kuna haja ya kujiuliza hawa ni kina nani au mjadala wenyewe umewaweka wazi. mjadala ulibainisha kila aliyejadili yuko upande gani kama ni wa wananchi kutetea mali zao au ni wa mafisadi kutetea wanaoiba mali za umma. hivi hawa viongozi walikuwa bungeni au kama ni waziri amekuwa waziri kwa tiketi gani? je anajitambua au tumejenga mifumo ya watu kupewa madaraka bila kujua wanamtumikia nani.
Waziri anasimama amekasirika kabisa mpaka anatukana kisa eti mtu aliyeghushi nyaraka, aliyekwepa kodi, aliyechukua pesa ambayo si yake kwa maana bila kufanya ukokotoaji upya na kubaini kama kama fedha yake yeye ni kiasi gani ndiyo hiyo tu achukue na kabla ya hilo fedha hiyo si yake wanataka apelekwe mahakamani.
Waziri anasimama na kudai kumpeleka mtu huyu mahakamani kwa makosa ya kufoji nyaraka, kukwepa kodi, kushiriki katika vitendo ambavyo vinaashiria kuwapa rushwa watendaji wa serikali lazima isubiri mapitio ya kesi ya madai alifunguliwa mtuhumiwa na hivyo matokeo ya kesi hiyo ndiyo serikali itaamua cha kufanya.
Hivyo yawezekana matokeo hayo ingawa hayahusu makosa haya ya jinai lakini akishinda kesi ya madai basi ni kusafishwa pia makosa ya jinai haya ambayo inatakiwa apelekwe mahakamani na mahakama ndio ikadhibitishe kama ana hatia na imhukumu.
Waziri anawaagiza watu waliopokea fedha ambazo bado zinaashiria kuwa fedha haramu kama rushwa kulipa kodi. Hivi kweli na rushwa inalipa kodi au kwanza tuchunguze kama ni fedha halali na kama ni halali ndio ilipe kodi na kama ni haramu hawa hawatakiwi kulipa kodi bali washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Lakini kukimbia kulipia kodi fedha hizi yaweza kuwa njia ya kutakatisha fedha hizi na tukajikuta tunaendeleza kufanya kitu ambacho tunakipiga vita.
Nashindwa kutambua haswa hapa tatizo ni nini lakini mambo kadhaa yawezekana.
1. Rushwa yaweza kusababisha mkanganyiko huu. Lakini 2 hii yaweza kuwa taswila ya elimu yetu.
Ukichukua mijadala ya debate zetu za sekondari za upande unaopinga na upande unaotetea kwa maana kama uko upande unaopinga mada husika haijalishi kinachoongolewa kina ukweli kiasi gani utabaki kupinga tu hivyo wapo yawezekana ambao wanadhani hoja ni serikali kujitetea hivyo watatafuta jinsi ya kufanya utetezi wa kuwa against bunge.
Hivyo walijadili mada wakidhani kuna pande mbili kwa maana ya bunge na serikali. Mimi nasema waliojadili kwa mantiki hii hawafai kuwa viongozi na najiuliza walipataje uongozi kwa maana kiukweli hapa kulikuwa na makundi mawili mafisadi na wananchi ambao wananchi walikuwa wakitetewa na vyombo vyao viwili yaani serikali na bunge.
Serikali ina wajibu wa kufanya lakini inaposhindwa kufanya ni bunge sasa kuhihoji hapa umefanya nini ? kwa nini huyu amefanya hivi na ukakaa kimya kama ni tatizo dogo unamuagiza akampige kibao aliyehusika lakini kama ni tatizo kubwa ni bunge kuwajibisha serikali nzima.
Lakini hapa ni wazi tuna watendaji wasiotambua kuwa wanatumikia wananchi hivyo wanafanana watoto wengi wanaokaa na walezi wao, mara nyingi unakuta watoto hawa au ndugu wanakaa nyumbani wanahudumiwa kila kitu lakini fadhila zao ni kwenda kukaa na majirani kuwasema vibaya walezi wao. Unajiuliza huyu unayekaa naye kumsema mlezi wako anakusaidia nini wakati nyumbani unakula na kunywa na kulala.
Kama jamii tunawajibu wa kuwakumbusha hawa majukumu yao na kwangu mimi nafikiri ni jukumu la tume ya maadili pia kuwachukulia hatua watumishi wa umma na viongozi wanaoonyesha misimamo ya wazi ya kutetea maovu katika jamii.
Kwa naibu waziri wa fedha msimamo wake ulikuwa sahihi yeye alisema swala linalomhusu la kodi ila kila waziri anayehusika alitakiwa kutoa kauli ya wizara yake kuhusu swala hili.
Waziri wa sheria au mwanasheria mkuu wa serikali walitakiwa kutoa kauli zao kuhusu mtizamo wa sheria kuhusu swala hili na nini kifanyike.
Hatuwezi kuwalazimisha waseme nini ila wanachokisema ndicho kinaweza kuwabainisha wako kwetu wananchi au kwa mafidi na ama tuwaunge mkono kwa mapendekezo yao au tuwawajibishe kwa misimamo yao.
3. kitendo cha bunge kutotambua mamlaka yake mpaka wakavutana mda mrefu ni cha kufedhehesha.
4. kitendo cha serikali kutunga maneno ya maagizo wanayotakiwa kuagizwa na bunge ni cha kusikitisha.
5. kitendo cha watuhumiwa kutumika kutunga maamuzi ya bunge ya kuwawajibisha kinachekesha kama sio kuwaacha wananchi mdomo wazi.
Yote haya yanajumuisha swali moja tu kuwa hivi utumishi wa umma Tanzania kweli kuna maadili yake? Na maadili haya tunayalindaje au tunayasimamia vipi?
Kimsingi sakata hili linaonyesha tuko uchi kabisa tunahitaji kuvaa nguo.