Sakata la Escrow;Kwa nini Zito hakumgusa rais?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,242
103,943
Baada ya kamati ya PAC kusoma na kuchambua ripoti ya CAG,aliyekuwa mwenyekiti wa PAC alionyesha masikitiko makubwa jinsi fedha zilivyochotwa.Akiwasilisha report bungeni Zito Kabwe alitaja kwa majina wahusika wa sakata hilo.Walitajwa wahusika wa moja kwa moja na wale ambao walioneka kuwa negligent katika kusimamia taratibu.Mh.Zito aliwagusa pia watu wa Ikulu na akaenda mbali zaidi na kusema katika uchotwaji na utapanyaji wa pesa za Escrow ni kama "NCHI ILI-COLAPSE"!Ajabu Mh.Zito na kamati yake hawakumuhusisha popote rais na sakata hili.Najiuliza kama nchi ili-colapse,je katika mazingira gani mwananchi namba moja asihusike hata indirectly?!Pia Mh.Zito alizidi kusisitiza kuwa pesa zile zilikuwa za umma,kinyume kabisa na hotuba ya rais iliyosisitiza kuwa pesa sio za umma!Je,uliwahi kumsikia Mh.Zitto "akimkemea" na kumtaka rais awajibike??!!!MIMI NA WEWE HATUJUI
 
Hawezi kufanya hivyo kwasbbu rais ni Rafiki yake Wa pete na kidole pia Zito yuko karibu sana na usalama Wa taifa ambao pia aliwasaidia kupenyeza maneno ya chadema kwenye kasri lao, kwahiyo katu hawezi kumyaja !!
 
Mwandosya alimshauri amwache tu, kwa maslahi yake na ya chama chake, ZZK naye akakubali kusaidia chama kwa maslahi yake binafsi. Kweli uksikia mtu anajiita mzalendo TZ, omba miaka 3-5 ya kumsomea kama digrii.
 
Back
Top Bottom