Sakata la Dkt Mwaka, hapa serikali imekurupuka

Sakata la Dkt Mwaka, hapa serikali imekurupuka

Aventus

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2013
Posts
2,011
Reaction score
2,176
Dr MWAKA NA SERIKALI WA KULAUMIWA NANI?

Kuna mjadala mzito unaoendelea karibu kila kona ya nchi hii, huki mitandaoni ndipo ulipooenea zaidi, mjadala huo unamuhusu Dr aliyejinasibu kwamba yeye ni tabibu bingwa kupitia Kliniki yake iitwayo Fore Plan iliyopo pale Ilala Bungoni jijini Dar.
Nimejaribu kuufatilia mjadala huo bado sijauona ukijadiliwa kimuonekano unaopaswa kutazamwa na kwamba ni nini tatizo na hatma yake

Nikijiuliza
1. Kuna herbal clinic ngapi Tanzania?
2. Kwa nini aanze na ForePlan?
3. Kulikuwa na doubts zipi hata mpaka aanzie pale?

Ebu tukae tufikiri kwanza Tusikute Tumeanzisha serikali ya visirani, kukomoana, hujuma na kulipa visasi?
Tafadhalini watanzania Tanzania yetu ni ile ile itikadi za vyama na dini waka tofauti zetu zingine zozote ziwe za ukabila na hata ukanda zisitugawe tukausahau utanzania wetu, tukumbuke hakuna amani pasipo Haki Tusipelekwe tu puta na hawa wanasiasa tukumbuke pamoja na yote mwisho wa siku wanasiasa ni watafuta pesa kama watu wengine hivyo wasijifanye wao ni malaika kila mahali wako sawa

Ni nani kati yetu imemuingia akilini Clinic iliyoanzishwa tangu October 2010 tabibu wake apate kijicheti tena cha kuattend clinic moja huko Guanzhou mwaka jana?
(na tena kuna taarifa kuwa zile machine ukizinunua ni lazima uattend training ya kuzitumia na huenda ndio hiyo ya mwaka)

Sasa tujiulize ilikuaje mtu akawepo muda wote huo?
Waziri wa Afya where were you?
Msajili wa Clinic za tiba mbadala huyu jamaa alikuonesha vyeti vipi hata ukampa ruhusa ya kutibu dada zetu na Mama zetu?
Je mliwahi kumfuatilia utendaji kazi wake na kama kweli wagonjwa wake wanapona ama ikikuwa kiini macho?
Hizi lawama atupiwe nani, Dr Mwaka au Serikali?
Kwani serikali ni nani?
Kwa nini tunawaza hapa hapa tusiwaze kule mbali kuangalia majambo kwa upana wake?
Hii elimu yetu imepika watu wenye ufahamu wa aina gani au na mpishi wa wasomi wetu nae mbumbumbu kawalisha watu elimu mbichi?

Tunakimbilia tu kumlaumu Mwaka! Mwaka! Mwaka! Tunasahau alikuwapo pale kisheria, wengine utawasikia wakiuliza eti kwa nini akimbie?
Hivi kukimbia kuna husiana vipi na uhalali wa udaktari wake?
Au labda hatukumbuki kamati ya Bunge ilipozuru halmashauri ya Jiji la Mwanza maofisa wote walizikimbia ofisi zao, Ina maana nao hawakuwa maofisa?
Why don't we think a little bit more hence judging from point to point and disagree where necessary?

Kwa nini hata tuliache suala kubwa lililosababisha tukimbilie kisababishwa?
Kama Mwaka si tabibu na serikali yetu ingekuwa makini huu mjadala usingekuwepo leo sasa kutokana na udhaifu wa serikali kuna Dr Mwaka leo tunaacha kujadili udhaifu huo ambao ndio point ya msingi tunamsonta huyu Mwaka ambae ni minor point.
To me, it is fallacy to lament on Mwaka neglect the government silly on making sure its people are safe

Tena hili ni suala pana mno ilitupasa tuungane sote kwa pamoja na kuishtaki serikali kwa uzembe huu ambao pengine umepelekea watu wengi kupoteza maisha endapo itathibitika tabibu Mwaka ni tapeli na wala sio kumzodoa
Kama Mwaka sio Dr kaishitakini serikali yenu kwa uzembe uliohatarisha maisha yenu acheni kunong'ona nong'ona na kuongelea matumboni

Mimi nikajua watanzania tumeshabadilika kumbe yule mzee hakuwa mjinga kusema ELIMU ELIMU ELIMU
Naona kweli inahitajika ELIMU ELIMU ELIMU kuwaelekeza maana manakariri tu hamuelewi na mkielewa hamuelewi inavyopaswa kueleweka

Sio kwamba namtetea MWAKA hapana nachotaka tufikirie kuna nini nyuma ya pazia hata iwe hivi tusikurupuke tu kutupa mawe upande tusiouona tutawalenga wasiohusika, Sisi tulipaswa kukaa na kusubiri kuisikia serikali inatoa tamko gani juu ya tabibu huyu na ituambie ilimruhusu vipi na ikiwa kuna watu waliathirika na huduma zake itawajibika vipi?
Tuwe tunawaza sawasawa kule Uingereza kuna kijana alianguka kwenye sink la barabarani akaishtaki manispaa akalipwa na kuitoza faini kubwa kwa kutokuwa makini Je hapa sisi hatuoni ni muda wa HapaKudaiTu?

Kinachonisikitisha zaidi ni watu aliokuwa akiwahudumia Dr Huyu na kama mjuavyo tatizo kama kutokupata mtoto linawafanya wanandoa kuwa desperate sana yaani hata akiwa muislamu ukamwambia dawa yake ni Kula kinyesi cha Nguruwe basi atakula tu sasa kama alikuwa akiwachezea kiini macho serikali inapaswa iwajibike katika hilo

Tusiwe watu wa kulalamika tu Kulikuwa na mkuu wa wilaya pale hakuwahi kuzuru pale mpaka aje NW au yeye kazi yake ni WEKA NDANI TU?

Sikatai kama hatokuwa daktari wa kweli basi huenda aliwalaghai wengi mno hasa wale aliowasema wana matatizo ya ugumba nahisi wazi labda kutokana na Dada zetu kuanza mapenzi wakiwa bado wadogo na kutumia njia za uzazi wa mpango pasipo ushauri wa kitabibu ukute ilimsababishia mtu hormanal disorder au hormonal imbalance amehangaika kupata mtoto hajapata akaenda pale akapewa list ya matunda na dawa za kubalance hormone tu akawa sawa na kujiona kapona ugumba

Lakini hili suala la madaktari feki si la leo kuna yule aliyekamatwa Manyara, kuna yule Bingwa wa Moyo jina namuhifadhi lakini ni mtu wa Morogoro, kuna na wengine wengi tumewahi kuhabarishwa mtu aliyefanyiwa operation ya kichwa kimakosa hii yote inatokana na nini?
Kwa nini tunacheza na uhai wa watanzania hawa?
Kwa nini tunayaweka maisha ya watanzania hawa rehani kiasi hiki?
Kwa nini tumlaumu mbwa kumng'ata mpita njia tuache kumlaumu anayemfuga mbwa huyo akamuacha azurure hovyo?
Serikali mnalikwepaje hili?

Nilitegemea madaktari wa tiba mbadala pamoja na chama chao wangeingilia kati suala hili lakini bado nadhani wanaweza kufanya hivyo, inapaswa ikithibitika MWAKA hana sifa za kuwa tabibu waishtaki serikali kwa kuishushia wasifu taaluma yao na kwa kuwa kutokana na kashfa kubwa kama hii basi huenda kukawa na wimbi kubwa la watu watakaoathirika kisaikolojia na kuwaona watabibu mbadala ni waongo na makanjanja na hata sector hiyo kukosa soko tena wakati wengi walishaanza kuiamini mno

MWISHO niiombe serikali huu uwe mwanzo tu waendelee kuna udanganyifu mkubwa na uvunjifu wa sheria mkubwa hata huku mitaani tu kwa mfano kwenye basi aweza kupanda mtu from nowhere akaanza kuuza dawa za miti shamba na nyingine za kichina wao kama serikali hili hawalijui hata walizuie?
Wasisahau kutoa taarifa za Babu wa Loliondo huenda pia kuna watu wengi waliathirika ama kufa kutokana na dawa yake almaarufu kikombe watuambie yeye walimchukulia hatua gani au kwa kuwa nao walipata kikombe basi kifo cha wengi harusi?
 
Dr MWAKA NA SERIKALI WA KULAUMIWA NANI?

Nikijiuliza
1. Kuna herbal clinic ngapi Tanzania?
2. Kwa nini aanze na ForePlan?
3. Kulikuwa na doubts zipi hata mpaka aanzie pale?

Akiishia hapo nitaona kweli kuna tatizo, ila kuanzia hapo sioni tatizo.
 
Umeandika vizuri ila hilo la kuanzia kwa mini ulitaka waanze na nani kila kt kina mwanzo wake bahati mbaya imekuwa kwake .lakini umeeleweka hongera sana
 
Kuibadili tz ni ngumu sana labda serikali iwekeze kwenye kizazi kipya ila hiki cha zamani kinasumbuliwa na Stockholm syndrome
 
Hii serikali ina miujiza na viongozi wengi wivu umewajaa, walijenga barabara kwenda Loliondo kwa babu na viongozi wengi walikwenda kunywa mpaka rais Magufuli alikunywa kikombe cha babu, dawa ya babu ilikuwa na masharti haibebeki unakunywa pale imepimwa kwa mkono wake una sepa mpaka leo hawajamfungia, why Dr. Mwaka ambae dawa zake unabeba, TFD wanajua yupo maana hafanyi siri kwa nini kumsumbua? Kuna jambo si bure.
 
Back
Top Bottom