Sakata la DC Mstaafu kumshambulia mkewe lachukua sura mpya

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Sakata la aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Peter Toima Kiroya kudaiwa kumshambulia mkewe, Philomena Toima na kumsababishia maumivu makali mwilini limechukua sura mpya baada ya polisi kumwita na kisha kumhoji kiongozi huyo mstaafu.

Toima aliitwa jana katika kituo cha polisi cha Orkesmet wilayani Simanjiro mkoani Manyara na kuhojiwa kuhusu madai ya kumshambulia mkewe.

Toima, ambaye hivi Karibuni alituhumiwa na mkewe, Philomena Toima kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali mpaka kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu alihojiwa jana wilayani Simanjiro.

Akiongozana na watoto wake wawili Toima alihojiwa kuhusu madai ya kumpiga mkewe, kumnyanyasa na kumtishia silaha mara kwa mara huku akitoa Utetezi wake mbalimbali kwamba suala hilo liko mikononi mwa wazee wa ukoo.

Mara baada ya kuhojiwa ndipo mkewe na yeye aliyekuwa kituoni hapo aliitwa na kuhojiwa kuhusu sakata hilo ambapo alishikilia msimamo wa kutaka suala hilo lifike mbele ya mahakama ili apate haki zake.

Hata hivyo, mwanamke huyo aliliomba jeshi la kumpatia ulinzi kwa kuwa amekuwa akipokea vitisho sehemu mbalimbali huku akasisitiza kwamba Kamwe harudi nyuma katika kudai haki zake.

Mbali na madai hayo mwanamke huyo amemtuhumu mume wake kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao baada ya kuchepuka na binti mwenye umri wa Kati ya miaka 30-32 aitwaye Scolla Mollel huku akidaiwa kuwa binti huyo amekuwa akivuruga ndoa yake mpaka kufikia hatua ya kupigana na mtoto wake wa kike.

Tutaendelea kuwapa kile kinachojiri katika sakata hili hatua kwa hatua mpaka mwisho.
 
Ndio ujue hawa ndo tunawaita wenyeviti wa Ulinzi na usalama wilaya wasitaafu!

Just imagine asingekuwa amepitia UDC angekuwa Malaya kiasi gan!

Kwani sheria hazijui? alipokuwa DC kafungisha ndoa za watu wangapi?
 
dmkali, Dc anawakilisha wananchi,na kuna wananchi wengi tu wanachepuka,a good leader must act with a reflection of his people
 
Kumbe kisa mke hataki uke wenza!!! Kama hataki asingekubali kuolewa na mmasai, una mwita mke mwenzako mchepuko! Mnafanyiana fujo lazma mtakosana na mumeo
 
...mume wake kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao baada ya kuchepuka na binti mwenye umri wa Kati ya miaka 30-32 aitwaye Scolla Mollel huku akidaiwa kuwa binti huyo amekuwa akivuruga ndoa yake mpaka kufikia hatua ya kupigana na mtoto wake wa kike.

Zamani walikuwa wanausingizia ulimi kuwa ni kiungo kidogo lakini madhara yake makubwa, ukweli ni kwamba tuytendee haki ulimi viungo hatari kabisa kuwahi kutokea ni hicho kilichoko kwa Scola Mollel
 
Back
Top Bottom