Sakata la binti aliyejifungulia barabarani mkoani morogoro

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,076
Reaction score
34,847
SAKATA LA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.

Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki' (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume .
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.

Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.

"Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake," alisema Josephine kwa uchangamfu.

Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.

Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.

Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.

SAKATA LA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO - MPEKUZI HURU
 
Ni kutokana na huduma za afya kuwa mbali na jamii.
Pole zake sana, inasikitisha hata hivyo.
 
wabunge wetu wanasubiri kugonga meza kupisha hoja tu, tunaenda wapi tanzania? zaidi ya miak 50 hakieleweki
 
Halafu kuna mamilioni yametumika kupaga pafyumu jiji la dar wakati ndani kumeoza ili obama aje aone kunanukia
 
Nampongeza huyo Traffic Police amefanya jambo jema na la kiutu!
 
halafu ni morogoro hiyo tena kwa mbunge tajiri ABOOD
 
Muda sio mrefu ,yapata miezi miwili CCM ikiongozwa na Kinana na Nape walifanya mkutano wa hadhara hapo morogoro.Kwa kiasi kikubwa mkutano uliingolea dhihaka,matusi,vitisho na dharau dhidi ya chadema.

Pia mbunge wa morogoro kupitia ccm alipewa fursa ya kuzungumzia maendeleo yaliyoletwa na ccm hapo jimboni kwake na kama kumbukumbu zangu ziko sahihi alitaja ukarabati wa barabara za hapo morogoro kama ni mafanikio.

Mkuu wa mkoa bw bendera na yeye alipata wasaa wa kueleza wananchi juu ya mafanikio ya serikali ya ccm,katika afya alijivunia kitu kimoja ....eti kurejshwa kwa huduma za Ultra sound katika hospitali ya mkoa!

Leo hii tunashuhudia mama mjamzito akijifungulia barabarani baada ya kubebwa na bodaboda.....yawezekana uchungu ulizidishwa na mirusho na misukosuko ya toyo iliyokuwa inapita kwenye makorogesheni.

Sijui hao waliomsaidia walitumia mbinu gani ambazo zitazuia maambukizi(mfano maambukizi ya VVU) kwa mama,mtoto au wao wenyewe.

Ni aibu sana tena sana.....
HIVI TUKIKATA SHILINGI MOJA KWA KILA GRAM 1 YA MADINI YANAYOVUSHWA KWENDA NJE TUTASHINDWA KUADDRESS MATATIZO KATIKA AFYA?

Hebu nyie mabaradhuli,wanakharashi na wanaizaya tuachieni nchi yetu mapema iwezekanavyo!
 
Yale maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi?
Wananchi wananyimwa hata haki yao ya msingi ya kupata matibabu karibu na makazi yao...Miundo mbinu mibovu halafu tunajisifia uchumi wetu umekuwa sijui kwa asilimia kadhaa.....Huu kweli ni Upumbavu
.
 
SAKATA LA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.

Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki' (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume .
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.

Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.

"Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake," alisema Josephine kwa uchangamfu.

Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.

Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.

Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.

SAKATA LA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO - MPEKUZI HURU

Hongera sana Wananchi kwa ukarimu wenu tuijenge Tanzania kwa kusaidiana kama hivi, bila shaka Magufuli au Halmashauri wamejifunza kuhusu ubovu wa bara bara hiyo.
 
sasa hiyo mivulana inashangaa nini hapo? haijui kuwa ni leba hapo? au wanafikiri pana mirungi?
 
Wasamaria wema wanawake hawa!!!

Huyo mtoto huenda akaja kuwa presidaa ya Tanyangika na Gavana wa Jimbo la Morogoro miaka 40 ijayo!
 
Yale maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi?
Wananchi wananyimwa hata haki yao ya msingi ya kupata matibabu karibu na makazi yao...Miundo mbinu mibovu halafu tunajisifia uchumi wetu umekuwa sijui kwa asilimia kadhaa.....Huu kweli ni Upumbavu
.
ndio haya maisha bora...
 
Hongera jembe ingawa umezaliwa barabarani usijari safari bado ni ndefu we siunaona mdingi walivyo mchosha akina kinana
 
SAKATA LA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.

Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki' (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume .
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.

Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.

"Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake," alisema Josephine kwa uchangamfu.

Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.

Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.

Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.

SAKATA LA BINTI ALIYEJIFUNGULIA BARABARANI MKOANI MOROGORO - MPEKUZI HURU

Halafu kuna watu wasio na haya wamekazana sana kuipamba serikali yetu 'sikivu' inayowajali watu wake na hata kuthubutu kuwatambia wananchi ya kuwa ccm imewajengea 'barabara, mashule, hospitali, imewaletea bodaboda' n.k. Bila haya wala hofu ya Mungu wanadiriki kuwauliza 'CDM imewafanyia nini?' Inasikitisha sana ya kuwa miaka 51 baada ya Uhuru wa Tanganyika bado hakuna huduma nzuri za hospitali karibu na mahali wananchi wanapoishi, na pia hakuna barabara nzuri ili hata kama hospitali iko mbali usafiri wa uhakika uwepo ili wananchi waepukana na majanga kama haya. Ni bahati nzuri tu ya kwamba huyu mwanamama alizidiwa na uchungu sehemu ambayo iliwezekana kupatiwa msaada na Mungu Akamsaidia akajifungua salama. Ingekuwa hali hiyo imetokea mahali pasipokuwa na msaada angefanya nini binti wa watu, na salama ya mtoto ingekuwaje? Halafu kuna watu wanajisifu eti tumejitahidi kupunguza vifo vya mama na mtoto. Kuna mambo mengine yanatia kichefuchefu. Tanganyika yetu kwenye suala la uhai wa wananchi na haki zao za kimsingi hakuna hata moja la kujivunia! Kuisifia serikali kwa uozo uliopo miaka hamsini na moja baada ya uhuru ni sawa na kibabu cha miaka hamsini na moja ambacho ndiyo kwanza kinaanza kujifunza kusimama dede kwa kushikilia viti, halafu mzazi anajisifu mwanangu kakua si mnaona maendeleo yake, miaka ya nyuma alikuwa anatambaa huyu!
 
Traffic wa kike hongera kwa kufanya kazi kubwa na kuwa na roho ya ubinadamu. Hali bado mbaya kwa wajawazito maeneo mengi nchini. Miaka 50 ya uhuru hali bado ni tete.
 
Back
Top Bottom