Sakata la Ben Saanane; Swali kwa Jeshi la Polisi nchini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Gazeti la mwananchi la leo linaripoti kuwa Jeshi la Polisi nchini limeomba msaada kutoka kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa Ben Saanane.

Binafsi nalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hii hata hivyo nina swali lifuatalo kwa Jeshi hili.

Kwakuwa Tundu Lissu alitoa namba ya simu ya mtu aliemtumia Ben ujumbe wa vitisho,ni kwanini basi Jeshi la Polisi lisitafute details za mmiliki wa namba hiyo ya simu kutoka kampuni husika ya simu na kisha kuzitangaza taarifa hizo kwenye vyombo vya habari ili wananchi wasaidie upelelezi wa sakati hili?

Ushauri kwa Jeshi la Polisi na chama chake cha CHADEMA kuhusiana na kupotea kwa Ben Saanane.

Ili kusaidi upelelezi/kupatikana kwa ndugu yetu bwana Ben Saanane, nazishauri taasisi hizi mbili hasa Jeshi la Polisi litangaze zawadi nono ya fedha taslimu kwa mtu yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa ndugu yetu huyu
.

Nashauri hivi kwasababu jambo hili kwa sasa limeshakuwa na public interest hivyo ni bora likapewa uzito unaostahili.

Ni ushauri tu.
 
Kabla ya Polisi, Mbowe amjibu Baba Ben.

SAKATA la kupotea ghafla kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bernard Saanane, limechukua sura mpya, baada ya familia yake kumjia juu mwajiri wake, Chadema, kwa kile inachodai chama hicho kimeshindwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kumtafuta.

Akizungumza na MTANZANIA jana, baba mzazi wa Saanane, Focus Saanane, alisema anashangazwa na hatua ya Chadema kushindwa kujitokeza hadharani kumtafuta mwanae ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Tangu mwanangu Ben amepotea, hatujawahi kumuona (Freeman) Mbowe ambaye ndiye mwajiri wake kama amechukua hatua yoyote ya kukutana na familia yangu, tukashauriana namna ya kumtafuta. Ukimya huu umenistajabisha mno.

“Nilitegemea angekuwa mtu wa kwanza kuja kwangu, tuone njia gani ambayo tunaweza kutumia kumpata Ben. Naumia mno ndugu yangu,” alisema Focus.

Alimtaka Mbowe ajitokeze na kuipa familia taarifa za mahali alipo Ben, kwani wao wametawaliwa na hofu kubwa kutokana na kijana wao kutoweka akiwa mikononi mwake.

“Ninamtaka Mbowe aniletee mwanangu Ben akiwa mzima, nashindwa kujua yupo wapi na nini kinaendelea mpaka sasa kati yake na Ben, haiwezekani mwajiri ashindwe kujua mfanyakazi wake alipo mpaka sasa… bado haliniingii akilini mwangu… suala hili halileti taswira nzuri kwa jamii kama anaendelea kukaa kimya na hazungumzi chochote, si haki,” alisema.

Akizungumza kwa jazba, Focus aliiomba Serikali na vyombo vyake vya dola isaidie kumtafuta Ben kwa nguvu zote kutokana na juhudi za familia kugonga mwamba.

Pia alikanusha vikali taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, kuwa Ben amefariki dunia. Kwamba familia yake imeitwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwenda kutambua maiti moja iliyochomwa moto maeneo ya Uru Ongoma. Kata ya Uru Kaskazini wilayani Moshi.

CHADEMA

Akijibu malalamiko hayo, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alisema si kweli kama Mbowe ameamua kukaa kimya, bali wao wameiachia Serikali kufanya uchunguzi wa kina na kutoa taarifa.

“Wakati jambo hili linatokea, mwenyekiti wetu (Mbowe) alikuwa nje ya nchi, naelewa presha aliyonayo mzazi wa Ben katika suala hili, tunaendelea kuhangaika nalo na kutaka vyombo vya dola vichukue hatua.

“Tunaitaka Serikali ifanyie kazi mambo matatu ambayo yako ndani ya uwezo wake, iseme wapi alipo Ben, mara ya mwisho aliongea kwa simu yake na nani na wapi na itumie kila aina ya uwezo wa kumleta kwa sababu si mtuhumiwa,” alisema Makene.

RPC

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana, kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kuhusu mwili uliookotwa eneo la Uru Ogoma, si wa Ben kama ambavyo iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

“Uchunguzi uliofanywa umebaini aliyefariki ni Steven Kimario (55), mkazi wa Sanya Juu wilayani Siha, ambaye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira, baada ya kukutwa akifanya jaribio la kubaka mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka tisa.
 
Hii habari haitasaidia kitu tuwaze nje ya hapo.
 
Elewa wajibu wa kila mmoja pamoja na mipaka yao!! Wajibu mkubwa wanao polisi!! Kwa sababu hata huo upuuzi unaoueneza ya kuwa Mbowe anajua aliko Ben ulitakiwa uripoti pale pale ambapo Familia yake,chama chake,pamoja na wadau wengine waliporipoti! Ulitaka chama kifanye msako wa nyumba kwa nyumba?
 
Naona hili Suala lingepelwkwa kwanza kwa Watu wake wa karibu yaani waajiri, rejea kifo cha Yule Askari wa wanyama pori kule Arusha muuwaji au mtuhumiwa ni mke wake akisaidiwa na mfanyakazi wao.
Sasa hapa je kazini alionekana Mara ya mwisho lini?? Je mwajiri alitoa taarifa kokote kule kupotea kwa mfanyakazi wake na lini?? Je gazeti pendeza la Chama Mara ya kwanza ku report kupotea kwa Ben ni lini ? Siku ngapi baada ya tukio ?? Na liliendeleza kampeni Hiyo ya kutaka kujua alipo Ben. Je waajiri wameshikilia na vipi na familia ya Ben ktk kumtafuta au wao waajiri Hilo Suala haliwagusi. Baada ya hapo ndipo tutakwenda hatua ya pili ya kuichunguza utendaji wa polisi
 
Hapa ninapata mashaka sasa na Dola kwa uadilifu wenu wa kazi, hamko serious na Maisha yetu wananchi.
Very simple like that eti tunaomba msaada mmefanya juhudi gani kwanza za kumtafuta Ben kabla ya Kuanza kuabisha Jeshi la Polisi maana hii ni aibu mnataka kutuletea Taifa letu kuwa Chombo husika na chenye dhamana ya Kulinda raia na mali zao eti mmeshindwa wajibu wenu.
Nadhani kama kweli itakuwa mmeshindwa kufanya wajibu wenu Waziri mwenye dhamana,IGP,na Jeshi lote linapaswa kuvunjwa lianzishwe upya pamoja na Wizara Husika.
Sitaki kuamini majibu mepesi mnayotaka kutueleza Polisi,Waziri na Sekta zenu zote husika kuwa eti mmeshindwa kumpata Ben, mna vyanzo vingi vya Usalama na Tz. inasifika kwa Amani na Ulinzi wa Taifa sasa mnataka kutuambia na kuambia Ulimwengu nini kuhusu eti kupotea kwa Ben na Maiti 7 kule Ruvu??????????????????????????
MY Take: Waziri,IGP na Sekta zote za usalama wa nchi yetu tunaomba muokoe Taifa letu na aibu hii maana hii itakuwa ni aibu sasa na kama ikishindikana kwa sote, basi Dola muombe nchi za nje zilizo piga hatua au kuendelea ila nayo itakuwa aibu tena eti kupotea kw Mtu, maiti 7 kule Ruvu...no no...no..haingii akilini hasa kwa mtimilifu wa akili.
 
dangerous-fish.png
 
Dawa ni kufuta jeshi la polisi la sasa na kuliunda upya , jeshi ambalo linaweza kutumwa hata na mjumbe wa nyumba 10 wa ccm kufanya lolote ni hatari mno .
 
Je Tundu L alipeleka namba hiyo polisi kama ya kusaidia kupotea kwake au aliandika kwenye mitandao?
 
Kwakuwa Tundu Lissu alitoa namba ya simu ya mtu aliemtumia Ben ujumbe wa vitisho,ni kwanini basi Jeshi la Polisi lisitafute details za mmiliki wa namba hiyo ya simu kutoka kampuni husika ya simu na kisha kuzitangaza taarifa hizo kwenye vyombo vya habari ili wananchi wasaidie upelelezi wa sakati hili?
lissu mropokaji na msaka umaarufu sidhani ata kama hiyo sms ilikuwepo, after all alikamatwa jana kwa mahojiano na jeshi la polis
 
Back
Top Bottom