Saidi Ndemla wa Simba SC afuzu kucheza soka Sweden

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,231
103,858
Simba Sports Club
Dar es salaam
25-11-2017.

TAARIFA KWA UMMA
________

Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.

Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja.

Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko.

Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaid, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi.

Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.

Mwisho

Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa.

Imetolewa na.....

HAJI S. MANARA
Mkuu wa Habari na mawasiliano SIMBA Sports Club
 

Attachments

  • FB_IMG_1511602929811.jpg
    FB_IMG_1511602929811.jpg
    17.6 KB · Views: 264
  • FB_IMG_1511602929811.jpg
    FB_IMG_1511602929811.jpg
    17.6 KB · Views: 178
  • unnamed.jpg
    unnamed.jpg
    16.6 KB · Views: 204
Back
Top Bottom