Saida karoli Tunakuelewa wachache tu.

Saida karoli Tunakuelewa wachache tu.

baest

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
273
Reaction score
171
Ni siku ya pili mama huyu ameachia video yake ya kichaka ambayo ndani yake Kuna belle 9, na Gnako.

maudhui yake ni mahaba/ mapenzi lakini picha zake zimejawa na mavazi ya kiasili na vitenge ...safi sana.

Nimevuta taswira kama diamond au alikiba kama angeachia video kama ile.

Kama tu wanasiasa na baadhi ya waimbaji wa injili walishindwa kujizuia kutoa ya mioyo yao juu ya nyimbo za "mafahali" hao wawili.

nimekuja kubaini kuwa ...muziki ni hisia, hulazimishwi kupenda kama hujashawishika.

Ila cha ziada kwa hapa bongo, lazima uwe na bifu au utafute kiki.

Simaanishi mama utafute kiki kwa msanii unayemuweza, la hasha, ila tunakutia moyo kuwa muziki wako una ladha ambayo ni sisi wachache labda "wa kizamani" tunapenda.

Hongera....mama/shangazi

Doubt is a liar
 
Kweli, atafute hata kaserengeti boy ka miaka 19, apige nacho picha kwenye kitanda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom