Said Mwema VS IGP Mangu, Nani zaidi katika Utendaji?

Said Mwema VS IGP Mangu, Nani zaidi katika Utendaji?

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,405
Reaction score
11,225
Nafikiri wote tunaweza kujadili utendaji wa IGp aliyepita Said Mwema na huyu wa sasa IGP Mangu, je ni nani anaweza kupigiwa mfano wa utendaji wa kujali taaluma ya polisi, kutatua shida za wananchi na kupunguza matukio ya ujambazi, Trafiki n.k. Nionavyo mimi huyu wa sasa baada tu kuteuliwa alienda ku-print vitabu lukuki vya NOTIFICATION/FAINI na kila trafiki akakabidhia ili jioni alete pesa kiasi kadhaa.
 
Mangu naona amekuja na mkwara wa kupata pesa kupitia faini kwa wenye magari humo barabarani ni balaa kila trafiki kapewa kitabu cha faini, zaidi si muongeaji kabisa. hata utendaji wake unatia shaka
 
Kama unauliza nani zaidi katika ile fani ya WAPIGWE TU, basi nadhani Mangu atakuwa anamzidi Mwema kwa points nyingi tu!
 
Wote sawa kwani wapo kwa ajili ya kuwaonea wapinzani na kuwalinda MAFISADI WA CCM
 
Hongera IGP Mangu kwa kazi nzuri ya kulet nidhamu katika sharia za barabarani hasa ka Dar es Salaam, sasa hivi askari wako wapo makini sana hawacheki na mtu wakikukamata (dereva) ni faini hakuna mjadala!!!!
 
IGP wa Tanzania anafanya kazi katika mazingira magumu sana. Ni sawa na kocha wa timu wa timu ya mpira anayeingiliwa kwenye suala la ufundi na kupanga timu. Wana siasa wanaingilia mno kazi za polisi.

Mi namwona Said Mwema mtu wa maana hasa alipokataa katakata kuongezewa mkataba baaada ya kustaafu. Mwingine angeendelea kukusanya pesa huku akitumiwa. Mfano mzuri ni Kova. Hana jipya. Amestaafu kapewa mkataba kama vile hamna watu wa kuchukua nafasi yake.

Suala la Amboni kule Tanga tunaishia kuangalia mashavu ya Chagonja kwenye Tv tu. Angekuwa kamanda Tossi, angekuwa kwenye mapango anafanya kazi!
 
Mangu naona amekuja na mkwara wa kupata pesa kupitia faini kwa wenye magari humo barabarani ni balaa kila trafiki kapewa kitabu cha faini, zaidi si muongeaji kabisa. hata utendaji wake unatia shaka

kwa iyo mangu yupo kipesa zaidi? dah jioni trafic anapeleka hesabu
 
SAID MWEMA ana afadhali aliliendesha jeshi kisomi kiasi pengine ile kufanya kazi INTERPOL kulimpa upeo kidogo
 
ndio kawaida mtu mzuri hajulikani mpaka aondoke ndio mnashtuka kumbe bora yule,maana hata mzee mkapa tuliombea aondoke sasa hv tunamtamani sawa na kwa said mwema kila siku tunamlaumu mara kamuweka muislam mwenzio lakini huyu matukio yanatokea hanyooshewi vidole mmenyamaza kimyaaaa
 
Back
Top Bottom