Said Mwema VS IGP Mangu, Nani zaidi katika Utendaji?

Said Mwema VS IGP Mangu, Nani zaidi katika Utendaji?

Nafikiri wote tunaweza kujadili utendaji wa IGp aliyepita Said Mwema na huyu wa sasa IGP Mangu, je ni nani anaweza kupigiwa mfano wa utendaji wa kujali taaluma ya polisi, kutatua shida za wananchi na kupunguza matukio ya ujambazi, Trafiki n.k. Nionavyo mimi huyu wa sasa baada tu kuteuliwa alienda ku-print vitabu lukuki vya NOTIFICATION/FAINI na kila trafiki akakabidhia ili jioni alete pesa kiasi kadhaa.
 
Mangu naona amekuja na mkwara wa kupata pesa kupitia faini kwa wenye magari humo barabarani ni balaa kila trafiki kapewa kitabu cha faini, zaidi si muongeaji kabisa. hata utendaji wake unatia shaka
 
IGP wa Tanzania anafanya kazi katika mazingira magumu sana. Ni sawa na kocha wa timu wa timu ya mpira anayeingiliwa kwenye suala la ufundi na kupanga timu. Wana siasa wanaingilia mno kazi za polisi.

Mi namwona Said Mwema mtu wa maana hasa alipokataa katakata kuongezewa mkataba baaada ya kustaafu. Mwingine angeendelea kukusanya pesa huku akitumiwa. Mfano mzuri ni Kova. Hana jipya. Amestaafu kapewa mkataba kama vile hamna watu wa kuchukua nafasi yake.

Suala la Amboni kule Tanga tunaishia kuangalia mashavu ya Chagonja kwenye Tv tu. Angekuwa kamanda Tossi, angekuwa kwenye mapango anafanya kazi!
 
Kwa maboresho ya jeshi (miundombinu=nyumba za askari+vituo vya Polish pongezi Kwa Kamanda Mwema
 
Back
Top Bottom