Said Mwamba Kizota has comeback to life as Kibu Dennis and Mohamed Mwameja has comeback to the pitch as Djigui Diarra.

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,121
27,128
Said Mwamba Kizota ni nani? Said Mwamba Kizota ni mchezaji bora kabisa wa wakati wote, wa mpira wa miguu kutoka Tanzania.


Nikiambiwa nimtaje mchezaji mmoja alie wapi kucheza mpira wa Tanzania ambae ndio bora kabisa kuliko wachezaji wote basi kwa haraka sana nitamtaja Said Mwamba Nassoro Kizota. Hayo si maneno yangu. Ni maneno ya Mahamoud Zubeir ( Bin Zubeir) wa Azam Tv. Kwangu huyu ni expert number moja wa mpira wa Tanzania.


Maneno ya Bin Zubeir yanaungwa mkono na Haji Manara a.k.a Shareef El Buggati a.k.a Shareef Matrophy. Maneno haya aliyataja wakati huo akiwa msemaji wa Simba.

Asilimia kubwa ya Wapenzi wa mpira wa Tanzania wanaofuatilia mpira wa Tanzania kuanzia miaka ya sabini watathibitisha kauli hii kuhusu Said Mwamba.

Said Mwamba aliyajibu kwa ufasaha maswali yote ambayo mpira wa miguu ulimuuliza. Ndio maana aliitwa Kizota.


Mwameja Mohamed Mwameja ni nani? Ni moja kati ya makipa bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu wa Tanzania. Kwa kizazi chake na kizazi kilicho fuatia baada yake hakujawahi kutokea kipa mwenye kufanana nae.

Mwamba huyu ambae anatajwa kuwa na mapenzi makubwa sana na klabu ya Yanga tangu utoto wake ( ingawa hakuwahi kuichezea/mwaka 93 alisaini Yanga ukatokea mgogoro hadi Rais Mwingi akaingilia kati) aliyezaliwq pale Mwakidila Tanga kutoka Mzee Mohamed Mwameja ( Mnazi wa Yanga) alikuwa hafungiki.

Ili kumfunga Mwameja ( anasema mdau mmoja wa Soka la bongo) ilibidi Abbas Gulamali atoe bahasha ndio kina Lunyamila watikise nyavu za Simba.


1. I see a lot of Said Mwamba in Kibu Dennis. It is as if Said Mwamba has come back to life as Kibu Dennis.


2. I look at Jiji Ziara ( Djugui Diarra) and see how Mwameja used to be on pitch.
 
Kwa lugha nyepesi ya kibantu kichwa cha mada kinasema Said Mwamba Kizota amerudi akifanishwa na Kibu Dennis pamoja na Mohamed Mwameja akifananishwa na Djigui Diarra
 
Miaka yao walikuwepo wachezaji wengi wenye vipaji kama wakina Hamis Thobias Gaga,Stiven Mussa,Athuman China,Mao Nkami,James Tungaraza,Peter Tino,Innocent Haule,Michael Paul (Nyron),Ramadhan Lenny,George Lucas,Fumo Felician,Nteze John,Abubakar Salum,Gebo Peter,Ken Mkapa,Mbui Yondani,Celestine Sikinde Mbunga,Zamoyoni Mogellah,Said Swed,Dua Said hawa ni baadhi tu ya watu wenye vipaji vya mpira tulivyowahi kuviona pamoja na Said Mwamba (Kizota) kutoka Tabora...
 
Miaka yao walikuwepo wachezaji wengi wenye vipaji kama wakina Hamis Thobias Gaga,Stiven Mussa,Athuman China,Mao Nkami,James Tungaraza,Peter Tino,Innocent Haule,Michael Paul (Nyron),Ramadhan Lenny,George Lucas,Fumo Felician,Nteze John,Abubakar Salum,Gebo Peter,Ken Mkapa,Mbui Yondani,Celestine Sikinde Mbunga,Zamoyoni Mogellah,Said Swed,Dua Said hawa ni baadhi tu ya watu wenye vipaji vya mpira tulivyowahi kuviona pamoja na Said Mwamba (Kizota) kutoka Tabora...

Hapo kwa Zamoyoni Mogella umenikumbusha kuna mchagga mmoja alikuwa anamkubali Zamoyoni Mogella hadi akamuita mtoto wake jina Zamoyoni.

Mchagga anaitwa Massawe so mtoto wake anaitwa " ZAMOYONI MASSAWE"


Jina la kizaramo /kiluguri + jina la kichagga
 
Back
Top Bottom