Said Mwaipopo anaudanganya umma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Said Mwaipopo anaudanganya umma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mkweremkwere, Jul 11, 2012.

 1. m

  mkweremkwere New Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipata matumaini makubwa sana ya kupata usuluhishi wa mgogoro kati ya madaktari na Serikali hasa baada ya Waliojiita Viongozi wa dini walipojiingiza katika Suala hili.

  Binafsi namheshimu sana mtu anayetaja jina la Mungu lakini pia namdharau sana mtu ambaye anatumia jina la Mungu ili kujipatia umaarufu au Kutimiza malengo yake binafsi na watu wanaomzunguka.

  Said Mwaipopo aliyekuwa msemaji mkuu katika kikao kati ya Madaktari wana harakati na 'Viongozi wa dini' pale hotel Travetine Jumamosi iliyopita. Japo nilipata wasiwasi nilipoona haop waliojiita wa dini, hasa kwa kuwa ni watu wa chini katika ngazi za kiuongozi za kidini kitaifa, nilipata imani kubwa pale niliposoma Tamko ambalo lilipambwa kwa lugha ya hosu kwa Serikali na makalipio ya unyanyaswaji wa Dr. Ulimboka...Kumbe Unafiki Mtupu!

  Mwaipopo alionyesha Umahili mkubwa sana katika kujibu maswali hasa mwandishi mmoja alipo muuliza, n' Viongozi wa dini mtafanya nini iwapo Rais atakataa wito wenu wa kuonana nanyi?' naya akajibu 'Kama Yesu alivyonawa mikono nasi tutanawa'

  Kwa kauli hiyo, baada ya Ikulu kukataa ombi lao, nilitegemea hao wanaojiita viongozi 'WATANAWA MIKONO'


  LAKINI Basi...
  Said Mwaipopo ameendelea kupiga makelee katika vyombo vya habari ,mara leo akisema watawashitaki madaktari...Unafiki Mtupu!
  Kulingana na Kiongozi mmoja wa Madaktari, wakati viongozi hao wakisubiri majibu ya maandishi kutoka Ikulu baada ya Vyombo vya habari kutoa taarifa kuwa ikulu imekataa ombi lao, inasemekana kuna mtu mmoja aliyejitambulisha kama AFISA WA IKULU alimpigia Mwaipopo simu akisema Rais atakutana na Madaktari Iwapo wataomba Msamaha Mbele zkwa Rais na kwa Umma! Hata Hivyo Viongozi wa Madaktari walitaka waambiwe jambo hilo kwa Maandishi na Mwaipopo akaahidi kufuatilia Barua ya Ikulu inayowataka madaktari waaombe msamaha!
  Kwa mujibu wa Madaktari Suala la Msamaha ni MUENDELEZO wa Propaganda na Ubabe wa Serikali na Kujikosha kwa Kikwete kwa WANANCHI!
  Taarifa toka kwa Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na Said Mwaipopo zinaonyesha kuwa Mwaipopo alikaripiwa na Viongozi wa ngazi za juu kwa kuandaa Tamko lile, na ili kulinda nafasi yake kidini, ameamua kuzusha kuwa wamekubaliana na madaktari kuhusu kuomba msamaha jambo ambalo si kweli...Madaktari wanamsubiri MWAIPOPO Apeleke barua kutoka Ikulu inayowataka Madaktari KUOMBA msamaha kama Sharti la Kuongea na Kikwete>>barua ambayo hana na hawezi kuipata!

  KWA NINI AMEIBUKA NA MADAI YA KUWASHITAKI MADAKTARI?

  Mwaipopo hajui kuwa Wananchi hawana Mkataba wowote na Madaktari na kwamba Wananchi wanapaswa kuibana Serikali na si Madaktari. Anaposema WAMESOMESHWA KWA KODI ZA wANANCHI, mwaipopo hajui KUWA Meals and ACCOMODATION ZA MADAKTARI NI MKOPO ambao wanadaiwa, Hajui kuwa aday ya Takribani 8,000,000/= ambayo wamelipiwa na Serikali inatokana na Kodi za Wazazi wao na wanaukoo wao. Daktari mmoja anakadiria kuwa na wanaukoo na ndugu kati ya 50 hadi 300 ambao kodi zao toka enzi za kodi ya Kichwa hadi kwenye bidhaa zingeweza kusomesha madaktari wengine hata 10 wasio wanaukoo...

  Swali Je Mwaipopo amelipa kodi kiasi gani iliyomsomesha Daktari?
  Watoto wa mwaipopo wanatibiwa wapi( KAMA ANAO)?


  KWA NINI ANAONGEA KWA uCCHUNGU NA KUUPOTOSHA UMMA?
  • KWANZA INASEMEKANA ALITISHWA NA VIONGOZI WA JUU KWA kuandaa kikao na KUSOMA tAMKO AMBALO HALIKUWA NA BARAKA ZA viongoZI wote wa kitaifa
  • Pili, anajikosha Kwa Kikwete baada ya Kugundua Ameharibu
  • Tatu, anataka Umaarufu kwa Jamii
  Mwisho, Watu kama akina Mwaipopo si wa Kuamini kabisa
  Kama angekuwa Mchungaji si mtu wa kusali kanisani kwake

  Ni Mnafiki mkubwa na Mpotoshaji wa Umma kwa Manufaa yake Binafsi
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  elimu yake ikoje huyo mwaipopo?huyo ni mchumia tumbo asikupotezee muda
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu huyu mtu ni mnafiki,tapeli na mfitini mkubwa.Anasababisha watu wauchukie uislam bila sababu.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo Said Mwaipopo kasomesha wanawe? Si ajabu ukute hajasomesha hata mmoja!
   
 5. v

  vngenge JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Na sisi waislam tutamshtaki kwa kusema maneno ambayo hatujamtuma
   
 6. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Mwislam wa wapi wewe acha unafiki
   
 7. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Mwaipopo Mswahili tu yule, ni mchonganishi sana kwenye nyanja za kidini! Kuna mdau mmoja anafanya investigative journalism kuhusu Mwaipopo muda si mrefu ataanikwa!
   
 8. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Atufanyie na ya KIBABU KIBACHELA na ya Ndugu Makengeza
   
Loading...