PostGE2025 Said Miraj: Lazima serikali iwajibike watu kuuawa, kupotea

PostGE2025 Said Miraj: Lazima serikali iwajibike watu kuuawa, kupotea

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mchambuzi wa masuala ya siasa na mwanasiasa mkongwe, Said Miraj, amesema serikali ina jukumu lisilopaswa kupuuzwa katika kulinda maisha ya wananchi, akisisitiza kuwa uhai wa mtu ni thamani kubwa inayolindwa na Katiba.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Force News, Miraj amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalinda haki ya kuishi, usalama wa raia na mali zao, hivyo vyombo vya dola haviwezi kuwa na visingizio linapotokea mauaji au kutoweka kwa watu.

Amesema jamii inapoendelea kushuhudia wananchi wakipotea au kuuawa kisha vyombo vya ulinzi vikashindwa kubaini wahusika kwa kisingizio cha “jarada halioneshi”, hali hiyo inadumaza imani ya wananchi kwa serikali.

“Maisha ya mtu ndiyo dhamana ya serikali. Ndio maana tunawalipa polisi walinde usalama wetu. Hakuna excuse. Watu wakifa au kupotea halafu tuseme uchunguzi haujaonesha nani kamteka, halafu iwe ndio basi — hilo halikubaliki,” amesema Miraj.

Ameongeza kuwa serikali inapaswa kuwajibika bila kujali kama wahusika wa matukio hayo ni watu waliopo ndani ya vyombo vya dola au nje ya mfumo huo, kwani jukumu la mwisho la kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani lipo mikononi mwa dola.

 
Machawa wanaendelea kuumia, wanafikiri wakileta propaganda uchawa na udini ndo watu watanyamaza. Kuua watu sio kitu cha kawaida kiasi hicho kwamba kinawezwa kupotezewa kirahisi tu.
 
Machawa wanaendelea kuumia, wanafikiri wakileta propaganda uchawa na udini ndo watu watanyamaza. Kuua watu sio kitu cha kawaida kiasi hicho kwamba kinawezwa kupotezewa kirahisi tu.
 
Ni suala la muda tu kabla mtu hajanyongwa hadharani

Machawa mpoo?

Mnatetea wauwaji? Pumbavu zenu sana!
 
Back
Top Bottom