Moronight walker
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 3,105
- 4,640
- Thread starter
- #21
Kuna mwingine akiona unampenda Sana kiasi unashidwa kujizuia anaweza akaitumia hio mpenyo kwa faida yake yeye mwenyewe, na hata kukuendesha vyovyote vile anavyotaka.... huu upuuzi wa mwanamke kujua umempenda kupitiliza wanaume inabidi tuuache, jamaa anaonesha hakuwa anajiamini kwa huyo mwanamke na mwanamke alijua wazi kutojiamini kwake na hakuwa na uwezo wa kuja kuachwa kitu ambacho mwanamke akijua ni sumu mbaya sana kwenye mahusiano sababu atakuwa anakupelekesha anavyotaka na hatokuwa na nidham ikifika katika stage ya kutaka kumuacha uwezo huo hutokuwa nao na ukifikiria ataenda kwa mwingine wivu na tamaa vinawaka rohoni unaona solution kuu ni kufanya aliyofanya ili wote mkose. Wanawake ni urithi wetu, tuwapende kwa kiasi na muda mwingi tuishi nao kwa akili sio kimwili sana (mfano kumfanyia matendo hata yasiyo na ulazima na pengine ya kukuumiza kwa lengo la kumridhisha tu) pia usije ukaruhusu ajenge kujiamini kulikopitiliza kwako all in all maisha yanaendelea.
Ni wachache Sana ambao akiona unampenda zaidi atauthamini upendo wako kwake na atakueshimu kwa kumpenda.