Sahau kuhusu Utajiri kama unafuatisha mifumo

Sahau kuhusu Utajiri kama unafuatisha mifumo

Unamwambiaje tunaeenda nae Moro na yuko ndani ya Bus,,,na Dereva hataki kupita hio Service Road..???

Sasa wengi ni Wanaenda Morogoro,,,lakini wapo ndani ya Bus,,,so akili ya Dereva ndio inawaongoza,,,wao wametulia tu..,,na wana amini wakitoka nje ya Bus watachelewa zaidi.,,,hawafikirii hata kushuka na kuomba Lift kwa wanaopita Service Road...

Ili utoke ndani ya Mfumo inahitaji ukubali kulipa Gharama zote na kukabiliana nazo,,Wengi wamefungwa na mifumo ya UOGA,,,UVIVU,,na mitazamo Hasi,,,,MUHIMU waanze kujitoa humo ndio waingie kwenye mifumo ya Nje..

Msomaji ambaye hujanielewa,,,,Relax,,Jipe Muda,,, Nakuja na Summary hivi punde...
Paragraph ya kwanza inawahusu watu walioajiriwa zaidi, Boss wake ndiye Dereva wake....ww mara ngapi ushawahi kuona watu wanashuka kwenye Daladala juu ya jam? Sasa mahesabu yanayotumika pale ndio inabidi yatumike pia kwenye ulimwengu wa kutafuta pesa.

Ukishuka utaumiza akili yako kujua utafikaje mahala unapotakiwa kufika, ukibaki kwenye basi utasubiri muongozo wa Dereva wako ambaye naye anafuata miongozo iliyowekwa Barabarani inayolindwa na mifumo

Na kumbuka mkifika Destination aliyefanikiwa hapo ni Dereva/Boss kwa juhudi za abiria, Sasa kwanini usishuke ukawa Dereva wa chombo chako mwenyewe hata kama utakumbana na changamoto za kutosha mbele ya Safari utakutana na waoga wengine wataunga taller kukurahisishia safari, Kikubwa na jambo la msingi ni kwamba ukifiki ni umefika hiyo, hujamsindikiza mtu kwenye mafanikio.
 
HUU NI UKWELI USIO DHAHIRI ILA NDIO UKWELI.
NI UKWELI AMBAO UNAFICHWA NA HUTAKIWI KUFIKIRIWA HATA CHEMBE ILA NDIO UKWELI.

UKWELI WENYE KIOO CHA TINTED ILA NDIO UKWELI.
VIONGOZI NA MATAJIRI WOOOTE WANATUMIA UKWELI HUU KUFANIKISHA MALENGO YAO YA KISIASA NA KIMAISHA.

NJIA NI MBILI TU ZA KUFANIKISHA MALENGO YAKO.
1. UWE MSHIRIKINA.
2. UTOKE NJE YA MFUMO.
 
Nimekuja kugundua kwenye hii Dunia hutakiwi kuwa mtepe mtepe, usifuatishe kila kitu kilivyopangwa utaishia kuishi kinyonge sana na Dunia ya Sasa inataka watu wakakamavu, walio serious na maisha haswa,

Labda kama umeridhika na maisha unayoishi lakini kama mawazo yako ni Utajiri au kupata pesa za kutosha basi ni lazima utoke Nje ya mfumo kidogo then ukishavuna unarudi ndani ya mfumo.

Ni lazima uvunje sheria ili kupata pesa, mfumo umeundwa ili kukuweka uwe masikini maisha yako yote na Sheria zinatungwa na matajiri ili kupata utajiri zaidi....Sounds wrong, but so right.

Matajiri wengi wamevuna pesa nje ya mfumo, na baada ya Kuvuna wamerudi ndani ya mfumo, Yani ni kama vile wote tunaenda Morogoro lakini foleni ni kubwa vibaya mno so uamuzi ni wako, upite na Service road uwahi kufika au ubaki Main road uchelewe au usifike kabsa

Na kumbuka anaepita Service road Kuna mawili, akutane na Police mbele huko au Asikutane nae kabisa na hata kama akikutana nae atajua jinsi ya kuchezesha then anarudi highway akiwa kashafika Moro


Caution[emoji3544]

Kuwa Makini na uvunjaji wa sheria utakaoufanya, Sababu Kuvunja sheria ni rahisi kusema au kufanya lakini swali ni kwamba utaweza kukabiliana na matokeo?

Wakina Messi wanakwepa makodi kwenye ma nchi ya watu na badae wanajua jinsi ya kuchezesha,...hiyo ndio Kuvunja sheria na kukabiliana na matokeo, lakini mwisho wa siku kibunda kiko Bank, lakini pia ukivunja sheria in smart way mbona una peta tu

Nasisitiza tena, kuwa Makini, usichukue hatua za kimihemko mara baada ya kusoma huu Uzi, ni lazima udhamilie kweli kweliView attachment 2270690
You are right nimesubiri thread kama hii miaka mingi sana at last imekuja......
is all about taking risk.
get rich or dying trying
 
Mathalani familia na koo tajiri za kiarabu hapa bongo chanzo kikubwa cha utajiri wao ulianzia kwenye uwindaji haramu na uuzaji wa nyara za serikali.
Ndio mana wazee wao walianzia maisha pembezoni kwenye mbuga na hifadhi za wanyama pori na baada ya kupata mitaji mikubwa wakabadili biashara na kuhamisha makazi Dar es salaam.
Hii kitu Ina ukweli ndani yake aisee

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mathalani familia na koo tajiri za kiarabu hapa bongo chanzo kikubwa cha utajiri wao ulianzia kwenye uwindaji haramu na uuzaji wa nyara za serikali.
Ndio mana wazee wao walianzia maisha pembezoni kwenye mbuga na hifadhi za wanyama pori na baada ya kupata mitaji mikubwa wakabadili biashara na kuhamisha makazi Dar es salaam.
Tafuta hela, acha hekaya za abunuwasi
 
Kwamba niende bariadi nikapge ndagu(kafara ya mtoto au mzazi). Mambo yakitiki naludi kwenye mfumo ikiwemo kwenda kanisani.
 
Back
Top Bottom