Sahau kuhusu Utajiri kama unafuatisha mifumo

BM X6

JF-Expert Member
Nov 24, 2020
1,360
4,149
Nimekuja kugundua kwenye hii Dunia hutakiwi kuwa mtepe mtepe, usifuatishe kila kitu kilivyopangwa utaishia kuishi kinyonge sana na Dunia ya Sasa inataka watu wakakamavu, walio serious na maisha haswa,

Labda kama umeridhika na maisha unayoishi lakini kama mawazo yako ni Utajiri au kupata pesa za kutosha basi ni lazima utoke Nje ya mfumo kidogo then ukishavuna unarudi ndani ya mfumo.

Ni lazima uvunje sheria ili kupata pesa, mfumo umeundwa ili kukuweka uwe masikini maisha yako yote na Sheria zinatungwa na matajiri ili kupata utajiri zaidi....Sounds wrong, but so right.

Matajiri wengi wamevuna pesa nje ya mfumo, na baada ya Kuvuna wamerudi ndani ya mfumo, Yani ni kama vile wote tunaenda Morogoro lakini foleni ni kubwa vibaya mno so uamuzi ni wako, upite na Service road uwahi kufika au ubaki Main road uchelewe au usifike kabsa

Na kumbuka anaepita Service road Kuna mawili, akutane na Police mbele huko au Asikutane nae kabisa na hata kama akikutana nae atajua jinsi ya kuchezesha then anarudi highway akiwa kashafika Moro


Caution

Kuwa Makini na uvunjaji wa sheria utakaoufanya, Sababu Kuvunja sheria ni rahisi kusema au kufanya lakini swali ni kwamba utaweza kukabiliana na matokeo?

Wakina Messi wanakwepa makodi kwenye ma nchi ya watu na badae wanajua jinsi ya kuchezesha,...hiyo ndio Kuvunja sheria na kukabiliana na matokeo, lakini mwisho wa siku kibunda kiko Bank, lakini pia ukivunja sheria in smart way mbona una peta tu

Nasisitiza tena, kuwa Makini, usichukue hatua za kimihemko mara baada ya kusoma huu Uzi, ni lazima udhamilie kweli kweli
Screenshot_20220624-150901.jpg
 
Mathalani familia na koo tajiri za kiarabu hapa bongo chanzo kikubwa cha utajiri wao ulianzia kwenye uwindaji haramu na uuzaji wa nyara za serikali.
Ndio mana wazee wao walianzia maisha pembezoni kwenye mbuga na hifadhi za wanyama pori na baada ya kupata mitaji mikubwa wakabadili biashara na kuhamisha makazi Dar es salaam.
 
Yote kwa yote kumbukeni tu kuwa kuna raha fulani anayopata mtu aliyeujenga utajiri wake upo msafi toka chini mpaka juu.

Kuna namna watapishana tu na mwenzake aliyeujenga kiuchafu katika wakati fulani hata kama kiviwango watakuwa na utajiri sawa.

Hata hivyo all hope is not lost, mwenye utajiri wenye uchafu anaweza kuusafisha kwa matendo ambayo yule mwenye utajiri msafi akiyafanya atapata raha maradufu.

Maana imagine huyu mchafu akaamua kutoa misaada kulipia 'deni' lake kwa jamii atakuwa analipa, lakini huyu mwenye nao msafi atakuwa simply ANATOA msaada.

Na itabaki ni kweli milele kwamba ; Ni heri zaidi kutoa kuliko kupokea............. Eternally true✔
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom