GE2025 Sagini akutana na balaa zito Butiama, wajumbe wamkataa!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Sagini Jumanne Abdallah amakutana na balaa zito kwa wananchi wa Butiama, baada ya ya baadhi ya wananchi kuonyesha kutomtaka kuendelea kujinadi mbele ya wajumbe

Hakika kweli wananchi mwaka huu wanalao jambo kwa viongozi waliwakimbia kuwaletea maendeleo

Nataman wabunge wote ambao walikwepo wasirudi ili waje wengine wapya nao wapate ajira maana akina kigwangallah wametuambia tujiajiri
 
na hii inapeleka ujumbe mzuri sana kwa viongozi wasiowajibika katika kuwatumikia wananchi waliowachagua, tatizo linapokuja box la kura wanashinda.
 
Mibunge yote ambayo huwa inapata bahati ya Kuwa mawaziri kutokea Mkoa wa Mara,huwa ni hovyo!

1.STEVEN MASATU WASIRA

Huyu yeye amekuwa Mbunge wa Bunda Miaka ya kutosha,Aliwahi Kuwa Waziri wa Kilimo & Maji

Tulitegemea watu wa Mara hakikishe anasaidiana na wadau wa maendeleo,wawekezaji na kuibana serikali ili kufufua viwanda vilivyokufa Ili watu na Vijana wa Mkoa wa Mara wapate Ajira,Ajabu viwanda vyote vya kuchakata Pamba (Jineri),Viwanda vya Samaki,Viwanda vya nguo (Mutex) amevikuta kama vilivyo na kaondoka kaviacha kama vilivyo!

Akiwa Waziri wa maji,Bunda haikuwahi Kuwa na maji hadi Leo,angalau kipindi Cha Esther Bulaya akiwa Mbunge watu wa Bunda waliopata maji ijapokuwa nayo yanatoka mara moja Kwa mwezi na wakati ziwa liko umbali WA km 5 tu !

Kazi ya WASIRA muda wote imekuwa kuisema CHADEMA kuliko kuwasemea watu wa Mara ambao wamezungukwa na Utajiri usiowanufaisha !

2.KANGI LUGOLA KANGI

Huyu yeye alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara,Mwibara ni Jimbo ambalo liko ndani ya wilaya ya Bunda,lakini pamoja na fursa hiyo ya uwaziri aliyoipata,Mwibara Iko ziwani kabisa lakini wananchi wake wanayaangalia maji Kwa macho tu !

Alichotumwa na wananchi hakukifanya ila akafanya asichotumwa na wananchi,Alikuwa mjuzi wa kukata viuno stejini huku waliopaswa kukata viuno wakimshangaa !,Haikuchukua muda Magufuli naye akamla kichwa,nadhani aliona hamna shughuli !

3.SOSPETER MUHONGO

Huyu yeye amekuwa Mbunge wa Musoma vijijini Kwa kipindi Cha miaka takribani 10,Pia Kwa kipindi hicho amekuwa Waziri ,Ajabu ni kwamba,ukienda Musoma vijijini Kuna Nuka shida,Jimbo la Musoma Vijijini ni Jimbo ambalo linazungukwa na ziwa lakini watu wake hawana maji safi na salama,Kuna migodi lakini wananchi wanauishi umasikini Kwa Vitendo,barabara kutoka Musoma mjini kuelekea Musoma Vijijini (Majita road) ni vumbi mwanzo mwisho !

4.JUMANNE SAGINI ABDALLAH

Huyu yeye hakuna alichofanya hapo Butiama zaidi ya kulembua uso,Aliyekuwa Mbunge wa Butiama ambaye Sasa ni Marehemu (Nimrod Mkono) amefanya mambo makubwa sana hapo Butiama enzi zake ukilinganisha na Hawa ambao wamepewa na uwaziri kabisa,Nimrod alikuwa Mbunge wa kawaida tu lakini aliibadili Butiama kuliko huyo SAGINI !

Mkoa wa Mara una bahati ya kupata mawaziri lakini tatizo hawaelewi wanachopaswa kufanya !

Mkoa wa Mara umezungukwa na mbuga maarufu ya Serengeti ,ajabu ni kwamba,watu wa Arusha na Viunga vyake ndio wanaonufaika na Serengeti kuliko Wana Mara wenye mbuga yao!

Kutoka Arusha to Serengeti ni umbali wa km 383

Kutoka Musoma Mjini to Serengeti Via Butiama ni km 129 (Kupitia gate la Natta/fort ikoma)

Kutoka Musoma mjini to Serengeti Via Bunda ni Km 87 (Ndabaka gate)

Musoma Kuna uwanja wa ndege ambao umekuwa ukitumika miaka yote,Ajabu ni Kuwa hao mawaziri mizigo wao kukaa chini na wadau wa utalii kushirikiana na wafanya biashara Ili Kuja na mkakati wa pamoja wa kukuza utalii ndani ya Mkoa wa Mara,wameshindwa!

Mtu kama WASIRA hajawahi kusikika mahali popote akiuongelea Mkoa wa Mara na kuzieleza fursa za kiuwekezaji!

Kazi yake kubwa ukimsikia ni kuiongelea CHADEMA tu na kuipiga Vijembe !,Anasahau kazi anayopaswa kuifanya Kwa ajili ya Wana Mara!
 
Piga chini sagini hakuna alichofanya, kamati kuu waheshimu uamuzi wa wajumbe
 
Sajini ni mzigo!
 
Nimeishi Butiama, kwangu mimi ndio sehemu ya hovyo zaidi niliyowahi kuishi.
 
Sagini Jumanne Abdallah amakutana na balaa zito kwa wananchi wa Butiama, baada ya ya baadhi ya wananchi kuonyesha kutomtaka kuendelea kujinadi mbele ya wajumbe

Hakika kweli wananchi mwaka huu wanalao jambo kwa viongozi waliwakimbia kuwaletea maendeleo

Huko siyo kwa akina Lucas Mwashambwa na Choicevariable kwamba utawadanganya na vijitakwimu vya kipuuzi tu.
 
Back
Top Bottom