Safu ya Uongozi (CHADEMA) vyuo vikuu ni hii


Status
Not open for further replies.
TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Messages
1,619
Points
1,250
TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2010
1,619 1,250
============
Mjadala huu umefungwa kwa sasa (kwakuwa imebainika ni upotoshaji: Majibu ya CHADEMA yapo hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/356884-facts-juu-ya-uongozi-wa-chadema-vyuo-vikuu;-kusema-uongo-ni-kazi-wanayoiweza.html
============


Katika moja ya vitu ambavyo CHADEMA inatajwa sana ni juu ya upangaji wa safu zake za uongozi wa kukibeba na kukiendeleza chama hicho. Kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa hapa nchini CHADEMA nao wanapanga safu zao za uongozi katika sehemu mbalimbali nchini.,moja ya sehemu hizo ni uongozi katika matawi ya chama hicho katika vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu hapa nchini.

Hivi karibuni wamepanga safu za viongozi wao ambao watakisimamia chama hiko kwa kipindi cha miaka 5 ijayo. na safu ya Viongozi hao ni kama ifuatavyo;

(i) University of Dodoma maarufu kama UDOM ni ELISANTE MUSHI.,
(ii) Chuo Kishiriki cha MWENGE ni JAMES KIMARO.
(iii) Sokoine University of Agriculture (SUA) ni JOHN KIMARIO.
(iv) Chuo Kishiriki cha DUCE ni ELIBARIKI MUSHI.
(v) Chuo Kikuu cha MZUMBE ni FRANCIS TAIRO.
(vi) Chuo cha Teknolojia Dar es salaam (DIT) ni ABSOLOM TEMBA.
(vii) Chuo kikuu Cha Mtakatifu Joseph (ST JOSEPH) ni JAMES URIO.
(viii) Chuo Kikuu kishiriki cha JURDAN UNIVERSITY ni ESTER MASAWE.
(ix) Chuo kikuu Cha Mtakatifu John (ST JOHN) ni GEORGE KIMAMBO.

Hawa ni baadhi tu ya viongozi katika safu mpya ya viongozi wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo maarufu kama CHADEMA. Kwa majina tu ya viongozi hao mtu mwenye ufahamu wa watanzania na asili zao anaweza kung'amua mara moja kuwa Chama Hiki kimejikita katika Kukuza na kuimarisha Kabila fulani na kulipa nguvu katika uongozi wa Chama Hiko.

Hii inatafsiri nyingi lakini pia inasababu nyingi.,moja ya tafsiri ni kuwa watu wa kabila hili ndio pekee wenye kukipenda zaidi chama hiki hivyo hujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi na hivyo kuwafanya wengi kuwa wao katika safu za uongozi wa chama hicho, lakini pia inawezekana kabisa kuwa ni sura ya UKABILA iliyopo katika chama hicho ndio inayowapa nguvu watu wa kabila la wachaga katika kuwania na kushinda nafasi mbalimbali na kuongoza chama hicho. Jambo ambalo kwa muda mrefu sasa limekuwa likitajwa na kupigiwa kelele.

Ama juu ya sababu ya hili ni kuwa, waanzilishi waasisi wa Chama walikijenga chama chao katika mtazamo wa kikabila na kikanda zaidi.,Dhana ya Unafsi ilitawala wakati wa uanzilishi wa chama hiki na hivyo kuwapa nafasi watoto wa waanzilishi na jamaa zao kuona kuwa chama hicho ni chao. Wakajitoa kukipigania na kukitetea.

Lakini kwa lugha yeyote.,tafsiri yeyote ama sababu yeyote utakayoitoa haiwezi kujustify mambo haya kupewa nafasi katika Taifa lenye misingi ya Ujamaa na uzalendo. Misingi ambayo inakinzana na namna yeyote ile ya upendeleo ama ubaguzi.

Kwa hili mnalolifanya CHADEMA vyuo vikuu mnakaa vipi kuwa chama hiki si chama cha kikabila na kidini..,TAFAKARI CHUKUA HATUA...!
 
Nicole

Nicole

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2012
Messages
4,282
Points
0
Nicole

Nicole

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2012
4,282 0
Aseee hii ni hatari kwa ustawi wa chama
 
Kayabwe

Kayabwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2012
Messages
344
Points
195
Kayabwe

Kayabwe

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2012
344 195
Umetumwa na Magamba,nafasi zilikuwa za kugombea na kupigiwa kura.
 
M

Mndokanyi

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2012
Messages
629
Points
195
Age
42
M

Mndokanyi

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2012
629 195
Bado utafiti wako haujakamilika,nenda CCM leta majina ya watoto wa vigogo.Unajua wakati mwingine tumia akili zaidi,nenda uliza kwenye hivyo vyuo kama kuna mtu alichakachua kura akawapa hawa watu unaosema wa kabila moja.Sio kila mtu anapenda kuwa kada wa chama kwa sababu kwa upande wa CHADEMA hamna maslahi,ila CCM ni fujo kwa sababu kuna posho na utaweza kuunga kundi fulani kwa ajili ya kunufaika.
 
U

umla

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2012
Messages
1,174
Points
1,250
U

umla

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2012
1,174 1,250
mbona wote wachaga kama kimario,kimaro,massawe,mushi,temba na wengine au ndo tuamini CHADEMA ni chama cha wachaga,inamaana hakuna wengine
 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,050
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,050 1,225
Habari hii si ya kweli. Imechakachuliwa kwa maslahi ya mleta mada. Ngoja nikuletee full list ya uongozi. Wait
 
J

j joni

Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
90
Points
0
J

j joni

Member
Joined Apr 3, 2012
90 0
Bado utafiti wako haujakamilika,nenda CCM leta majina ya watoto wa vigogo.Unajua wakati mwingine tumia akili zaidi,nenda uliza kwenye hivyo vyuo kama kuna mtu alichakachua kura akawapa hawa watu unaosema wa kabila moja.Sio kila mtu anapenda kuwa kada wa chama kwa sababu kwa upande wa CHADEMA hamna maslahi,ila CCM ni fujo kwa sababu kuna posho na utaweza kuunga kundi fulani kwa ajili ya kunufaika.
Hapa kuna hoja inayotakiwa kujibiwa na hoja na siyo sophism
 
N

nyampanaga

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2012
Messages
344
Points
170
N

nyampanaga

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2012
344 170
Kama ni kweli hii haileti taswira nzuri...Jitihada zifanyike kwa makabila mengine za kuwaelimisha umuhimu wa kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama...ili wenye kijicho na cdm wasipate pa kupigia kelele kama hivi
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
31,456
Points
2,000
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
31,456 2,000
Nilipoangalia jina la mleta mada tu nikaishiwa hata hamu ya kuendelea kusoma....
 
T

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
1,367
Points
1,195
Age
45
T

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
1,367 1,195
Katika moja ya vitu ambavyo CHADEMA inatajwa sana ni juu ya upangaji wa safu zake za uongozi wa kukibeba na kukiendeleza chama hicho. Kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa hapa nchini CHADEMA nao wanapanga safu zao za uongozi katika sehemu mbalimbali nchini.,moja ya sehemu hizo ni uongozi katika matawi ya chama hicho katika vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu hapa nchini.

Hivi karibuni wamepanga safu za viongozi wao ambao watakisimamia chama hiko kwa kipindi cha miaka 5 ijayo. na safu ya Viongozi hao ni kama ifuatavyo;

(i) University of Dodoma maarufu kama UDOM ni ELISANTE MUSHI.,
(ii) Chuo Kishiriki cha MWENGE ni JAMES KIMARO.
ACHA UONGO,KAMANDA ANAYEONGOZA CHADEMA MWENGE NI LAYZER SIMON,SIJUI HUKO KWINGINE.KADHALIKA UONGOZI WA MATAWI YA CHADEMA HUPATIKANA KILA MWAKA NA SI MIAKA MITANO.YOU ARE A LAYER
 
chitambikwa

chitambikwa

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
3,938
Points
1,195
chitambikwa

chitambikwa

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
3,938 1,195
kumbe hii Cd inaendelea ,nadhani watu wa kasikazini waamue basi maana kuwasingizia imetosha
 
Mark Francis

Mark Francis

Verified Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
605
Points
195
Mark Francis

Mark Francis

Verified Member
Joined Nov 19, 2010
605 195
Kwa ni kura zilipigwa na watu wa ukanda huo tu? Au hao viongozi wameteuliwa na Mbowe? Kama ni hivyo, kweli tuna kila sababu ya kulaumu...!!
 
zethumb

zethumb

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
610
Points
225
zethumb

zethumb

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
610 225
we umetumwa na CUF wanaoona sasa hawana kitu katika siasa za Tanzania kueneza chuki za ukabila ndani ya CDM! kinacho nishangaza ni kwamba huko mnakotoka je uongozi ukoje ukianza kuangalia majina ya watu na kuconclude?!, kuna mtu anaitwa Kimaro na ni mjaluo, huyu unamweka wapi?! Mfano CJ aliepita miaka michache iliyopita wengi mlidhani ni wa Quran kumbe wa HOLY BIBLE!! kigezo cha mtu kuitwa jina fulan hakimaanishi anatokea pande hizo na ni wa kabila hilo au dini fulan...Waliokutuma au kama umejituma mwenyewe ni watu HATARI sana kwa ustawi wa Taifa letu....Fikra zako ni za kidini kabisaaaa (japo umekuja kwa gia za ukabila), ndo maana mnadai Haki Sawa na sehemu za kitaaluma, unataka kuwa DOCTA wakati umesoma Madrasa, si utamnyesha mgonjwa kahawa wewe!!?!.....WE NDO WA KUTAFAKARI ....watu makini hawana haja ya kufikiri upuuzi wako....
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,296,636
Members 498,713
Posts 31,254,578
Top