Safisha tu, mi nasema safisha tu!


C

Cisauti

Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
19
Likes
2
Points
5
C

Cisauti

Member
Joined Jan 31, 2012
19 2 5
Binafsi si mwanachama wa chama chochote cha siasa, japo ni kiri kuwa ni mpenda mabadiliko ktk nchi yetu. Nimekuwa nikifuatilia kinachoendelea ktk siasa za Tz na kugundua kama kuna mahali tulitereza na tuna endelea kutereza. Ni kweli kwa maoni ya 1992 80% ya wananchi (18+yrs wa enzi hizo) ktk Tume ya Jaji F. Nyalali hawakuunga mkono mfumo wa vyama vingi. Lakini kutokana na presha kutoka nje na sababu zingine nchi ilianzisha mfumo wa vyama vingi. Nimekuwa nikifuatilia mienendo ya vyama vya siasa, mfumo wa uchaguzi na namna siasa zinavyoendeshwa hapa nchini na kugundua kuna mahali hapakosawa. Miaka ya 1995 hadi 2010 nimekuwa nikishuhudia chama tawala kikitumia kila njia kushinda uchaguzi ikiwemo patrol za polisi (FFU) siku moja kabla ya uchaguzi na siku ya uchaguzi, kupandikiza wanachama wavurugaji, kubambikiza kesi wagombea au viongozi wa vyama vya upinzani na hata kutoa chochote ili waondoe majina yao kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi. Kwa ujumla naona kama chama tawala kikitumia mizizi yake ya hadi ngazi ya mtaa (mjumbe wa nyumba 10), kuwa na dola na uwezo wa kifedha, kimekuwa kikigandamiza kwa kila njia inayowezekana kufifisha uwepo au nguvu za vyama vya upinzani. Swali ninalo jiuliza kulikuwa na hata gani ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama chama tawala na dola havikuwa tayari na haviko tayari kuwa na mfumo wa vyama vingi? Kwanini wasipitishe sharia ya kufuta mfumo wa vyama vingi kutumia wingi wao bungeni? Nikisema kwamba serikali iliyopo madarakani imeshindwa kustawisha mfumo wa vyama vingi nitakosea? Hawaoni faida za kuwa na vyama vya upinzani vilivyo imara ktk kuwa kumbusha walipo tereza?
 

Forum statistics

Threads 1,252,123
Members 481,989
Posts 29,796,278