Safi sana Dr Magufuli, Tanzania inaliwa na watu kama bosi wa EWURA!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,109
26,000
Ni jambo la kushangaza, kana si kusikitisha, ati kuna watu serikalini hawana habari kabisa juu ya kuibiwa mali za nchi kwa mikataba mibovu kama huu wa IPTL.

Kuna watendaji serikali, si tu hawana uchungu, lakini kwao ni business as usual.

Wao ni wasukuma mafaili tu, wakikodolea sheria tu inayowalinda kazini.

Hawa ni maadui wakubwa wa rasilmali za nchi na si ajabu utendaji wao kuna msukumo wa kufaidika kimaslahi, dhidi ya msimamo makini kama wa Rais Magufuli.

Wazo langu si kutumbuliwa tu hawa watu, tutazami na rushwa inayotembea nyuma ya pazia, kuendekeza mikataba mibovu kama huu wa IPTL.
 
Kwani huo mkataba aliingia yy au serikali?saiv ni kurushiana majanga,kila mtu anatafuta mnyonge wake
 
Sera zetu ndio mbovu,kwani kuna mahali kavunja sheria.Wampeleke mahakamani kama kuna sheria zimevunjwa yeye amefuata taratibu zote
 
Ni wendawazimu kufikiria mfanyakazi anaweza kusimamia au kuendesha ofisi kwa utashi wake bila ya kufuata sheria. Kama kuna tatizo la mikataba, kosa ni la mwajiriwa au serikali yenyewe ambayo ilitia saini mikataba hiyo? Ofisi za umma zinatakiwa kusimamiwa na sheria na kanuni za kazi na siyo utashi binafsi.
 
najiuliza tu, mbali na tambo zote hizi za tumbua tumbua;
mbona majipu na chunusi haziishi kwenye shamba hili la bibi?
nahisi kitu.
 
Sera zetu ndio mbovu,kwani kuna mahali kavunja sheria.Wampeleke mahakamani kama kuna sheria zimevunjwa yeye amefuata taratibu zote
Mkuu maamuzi mengine yanahitaji uzalendo wa hali ya juu.
Watendaji wengi serikalini wanajificha nyuma ya sheria zabutendaji na sheria za kazi huku wakipokea rushwa ili watoe maamuzi kwa maslahi yao na wafaidika dhidi ya serikali na wananchi.

Siyo bure, yule mhindi Singh katoa kitu kidogo ili EWURA wafanye maamuzi mabovu.
 
Watu wanatolewa kafara kwa kuwalinda wezi na bado unashabikia...
 
Sera zetu ndio mbovu,kwani kuna mahali kavunja sheria.Wampeleke mahakamani kama kuna sheria zimevunjwa yeye amefuata taratibu zote
Wewe kweli una upopo!
Kwani inahitaji akili gani kumfungia mlango mtu unayejua ni mwizi?

Tunalia mkataba wa IPTL ni mkataba mbovu, halafu mtu anapopata mwanya wa kumfungia kwa kumnyima leseni kwa maslahi ya nchi, anaamua kuuliza tumfugie au la?

Tumweleweje huyo mtu!
 
Ni jambo la kushangaza, kana si kusikitisha, ati kuna watu serikalini hawana habari kabisa juu ya kuibiwa mali za nchi kwa mikataba mibovu kama huu wa IPTL.

Kuna watendaji serikali, si tu hawana uchungu, lakini kwao ni business as usual.

Wao ni wasukuma mafaili tu, wakikodolea sheria tu inayowalinda kazini.

Hawa ni maadui wakubwa wa rasilmali za nchi na si ajabu utendaji wao kuna msukumo wa kufaidika kimaslahi, dhidi ya msimamo makini kama wa Rais Magufuli.

Wazo langu si kutumbuliwa tu hawa watu, tutazami na rushwa inayotembea nyuma ya pazia, kuendekeza mikataba mibovu kama huu wa IPTL.
Ripoti ya Makenikia Part II, inadhihiri ukweli wa mada hii!
 
Wewe kweli una upopo!
Kwani inahitaji akili gani kumfungia mlango mtu unayejua ni mwizi?

Tunalia mkataba wa IPTL ni mkataba mbovu, halafu mtu anapopata mwanya wa kumfungia kwa kumnyima leseni kwa maslahi ya nchi, anaamua kuuliza tumfugie au la?

Tumweleweje huyo mtu!

Wakati walioingia mikataba ya kishenzi bado mnawalipa pesi eti wastaafu,kazi mnawaachisha hawa mbuzi tu.
 
Sikiliza vizuri hitimisho na mapendekezo ya mwenyekiti wa kamati ni 2 ya madini.

Wanasheria wakuu, mawaziri wa madini, kamishna wa madini wote kuchukuliwa hatua!
 
Na Wastaafu wetu je?Si ndiyo waliotoa zile yellow stickers au??Kaka yangu mpendwa huwezi kumgusa Kalemani kama huwezi kumgusa Mkapa,upo??Yaani popote utakapowapeleka utagota tu.Issue ni hilo likatiba.
 
Katiba mwaisingizia.
Sasa nafikiri umesikia mapendekezo ya kamati ya madini II, mikataba inarudi bungeni.
Na wahusika wa mikataba mibovu kuhojiwa!
 
Mkuu mtani wangu mpendwa sijui kama litatekelezeka kwa maana waliokwapua ni WAKUBWA wa NCHI,tuliowapa madaraka makubwa mno kumbe hatukujua ni MAJAMBAZI.

Kuyakamata haya si rahisi,ni bora kusema adhabu yao ni kusimamisha mafao yao ya uzeeni maana wameshajilipa.!
 
Kuwatambua ni nusu tu ya kuwachukulia hatua!
 
Unawatambua halafu wanaendelea kuenjoy life,Mtani kweli unajua nitakurudisha milimani maana hapa mjini bado hujajua nini maana ya wekundu wa msimbazi.

Hao akina Mkapa na JK walitakiwa leo hii pamoja na waandamizi wao na familia zao wawe Lupango,mmeshindwa hakuna kuwapa vinunua mgongo period
 
Hivi Magu hajui kweli kwamba wanao hujumu na kuifilisi hii nchi ni ccm aka magambas pamoja na yeye akiwamo, ok ngoja tuone mwisho wake kama starling atakufa mwishoni au vp.
 
Mkuu maamuzi mengine yanahitaji uzalendo wa hali ya juu.
Watendaji wengi serikalini wanajificha nyuma ya sheria zabutendaji na sheria za kazi huku wakipokea rushwa ili watoe maamuzi kwa maslahi yao na wafaidika dhidi ya serikali na wananchi.

Siyo bure, yule mhindi Singh katoa kitu kidogo ili EWURA wafanye maamuzi mabovu.
Maamuzi magumu hayajawahi kumwacha mtu salama!ila tujiandae na matatizo makubwa ya uchumi.Hii kitu haitatuacha salama kwani Tanzania sio kisiwa tena.Watanzania tujiandae kisaikolojia kwani maisha yatapanda mara dufu hawa wenzetu wanaushirikiano kuliko sisi watanzania.Mungu naomba utusaidie.
 
Back
Top Bottom