Safari njema...
Kuendesha usiku!
Kwanza hakikisha hauna usingizi. Kama una usingizi, paki gari pembeni ulale kama nusu saa. Tafuta kinywaji cha Azam/ Mo energy ujiboost kuondoa usingizi na uchovu.
Kwenye kuendesha gari, hakikisha hautembei spidi kubwa sana. Nenda themanini mwisho mia. Kwa sie wazoefu mimi huwa natembea hadi mia Dar-Moro, Mia hadi mia na kumi Moro hadi Dodoma na from there huwa natembea hadi mia thelasini usiku. Hii ni kutokana Dar Moro kuna magari mengi ya ku over take. Moro hadi Dodoma kwa kuwa lami ni mbaya na from there bara bara imetulia hivyo huwa napepea inangawa sometime Dom to Singida huwa kuna upepo mkali unaoyumbisha gari.
Unapopishana na gari likakupiga taaa full ukawa huoni mbele na wewe washa full alafu angalia mistari. Yani usiangalie mbele kwa kuwa huwezi kuona. Wewe angalia mstari wa kushoto ambao ni wa njano na wa kulia ambao ni mweupe. Hakikisha unacheza ndani ya chaki.
Pia kama ulikuwa umeshikilia usukani kabla ya kupishana, usikate kushoto wala kulia hadi upishane na gari lililokupiga taa full maana ukikata kushoto au kulia unaweza toka nje ya chaki na kuanguka au kulivaa gari unalopishana nalo. Mara nyingi bara bara za high way hazina kona za ghafla kwa hiyo kunyosha usukani kwa sekunde mbili tatu hakuwezi kuwa na madhara makubwa kwako...
Cha mwisho kuwa makini na matuta. Bara bara zetu zina matuta mengi kama shamba la viazi...