SIMBA mtoto
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 204
- 100
Natarajia kusafiri kwenda Newala, kusudi la safari yangu ni kufika kijiji cha Ngende kutafuta bahati ya kimaisha.
Taarifa za awali nilizozipata ni za kutisha sana, na hatari yake ni kubwa sana hadi ufike kwenye hicho kijiji.
Taarifa zinasema jaribio la kwanza ni muda utakaotumia hadi ufike kijijini na kutoka hicho kijiji ufike kwenye shimo wanakokaa hao waungwana, kuna umbali wa kilomita 12 lakini ukiwa ngangari sana itakuchukua siku tano kufika shimoni.
Jaribio la kwanza ni jinsi ya kuwapita simba luwala waliotapakaa njiani, jaribio la pili ni kumpata mwenyeji wa kukubali kukupeleka huko ukimpata dau lake ni kubwa na hatakufikisha atarudia njiani, jaribio la tatu baada ya kuwapita simba ni majoka ya kutisha utakayokutana nayo, ukiwapita hayo majoka utauona mlima mkubwa mbele yako na chini yake ndipo lilipo lango la kuingilia shimoni.
Taarifa zinasema, mara tu unapokaribia lango, huwa anajitokeza mwanamama mmoja mrefu sana, naye ana jicho moja, wanasema huyo mama ni mzee sana, lakini ana maguvu ya kumnyanyua tembo na kumtupa chini na ni mkali ajabu. Wanasema unaweza kukaa hapo mlangoni siku moja hadi mbili ukihojiwa na kufanyizwa kazi za usafi, kisha unapewa mashariti ya kuingia shimoni....
Jamani naenda Ngende, nimepigika kimaisha, maisha bora kwa kila mtu yamenipitia mbali, naenda Ngende, walioenda na kurudi na mafanikio nipeni maujanja wa kwenda Ngende.