Safarini Lindi/Mtwara


Hizo bei za bus ni za zamani, mpya ndo hizo 26,000 kwa luxury bus, machinga na Buti la Zungu, Usafiri wa ndege ni bora na cheap, Precision air na fly 540 nauli zake ni kati ya 90,000 mpaka 120,000, just 45 minutes upo Mtwara na ndege zipo deile asubuhi na jioni!! Kuhusu kulala namshauri aende Dolphin lodge akaenjoy raha za mtwara, kama hataona Mikindani ni mbali basi akapoe The Old Boma apate upepo wa bakhari na akatafune pweza! Mtwara raha ati!!
 

mwombe huyo rafiki yako akupe stori za Ngende ya Liwale hasa kule sehemu inayoitwa Mpigamiti!!
nadhani itakufaa sana!!
 

Naomba nikuongezee hii, kuna mtaa/kitongoji kinaitwa Mdenganamadi(Simply Mdenga), ni mtaa mzuri sana, wasela wote wa mji na wadada warembo huko ndo kwao, sasa ole wako upewe appointment ya kwenda huko kuanzia saa 12:30 jioni, ukikatiza tu ushakula ngeta!! hao wadada wanatumika, so ni muhimu uulize anaishi wapi, ukitajiwa hicho kitongoji fanya kila uwezalo kudivert hiyo appointment uende sehemu ingine, dont try it, ni hatari kwako!
 

Kuna hili bwana maarufu sana pale karibu na Idara ya maji linaitwa NABWADA, sijui bado lipo au wawekezaji washajenga kiwanda..
I really miss Mtwara sana
 
kuna moja pia iliitwa tinga tinga ya mama mmoja wa kizungu ipo karibia na baharini kule bei zake ni nzuri tu sijui kama bado ipo
 
mwombe huyo rafiki yako akupe stori za Ngende ya Liwale hasa kule sehemu inayoitwa Mpigamiti!!
nadhani itakufaa sana!!

Nimesikia kidogo stori za ngende, ni kule watu huenda kutafuta utajiri na kupimiwa kwa punje za mahindi ?
 
Wewe umesoma nauli kwenye mabango mimi nimepanda machinga ijumaa iliyopita 22,000/= . Hawajaanza kutoza nauli mpya mpaka siku naandika kumpa taarifa za nauli alizohitaji. Hiyo Dolphine ni nzuri sana ila kwa swala la location ni zero lodge kuwa uswazi that much tena ya kiwango kile sio kabisa .
 
Sawa mkuu, suala la nauli ni bora ajiandae kwa 26,000, ikiwa pungufu itamfaa mbele ya safari, hiyo 22,000 inategemea siku hiyo biashara ipoje, mimi nakumbuka kuna kipindi Novemba 2012 bei zilipanda sana hadi Tshs.28,000 sababu vyuo vilikuwa vimefungwa, so nauli ya 22,000 haitabiriki, Dolphin for sure ipo Uswazi, ila ipo katika kiwango!! Mkuu mia
 
Kuna hili bwana maarufu sana pale karibu na Idara ya maji linaitwa NABWADA, sijui bado lipo au wawekezaji washajenga kiwanda..
I really miss Mtwara sana

Idara ya maji ipi Mangamba? Pale kwa Lymo au wapi mkuu, sijakusoma bana! I Miss ming'oko na Chikandanga!! Mtwara raha kwa kweli!!
 
Maelekezo ndugu zangu.......nipo dom ila wiki ijayo nataka kwenda mtwara, kwa hapo dar booking za kwenda huko zinafanyikia wapi na kwa sasa nauli ni shilingi ngapi? Napenda kujua basi gani bora la kusafiri nalo toka dar mpaka mtwara.
 
Mkuu tafuta hiyo thread humu ipo tena haina hata mwezi mzima tangu ibandikwe. Na ina mengi kuhusu mtwara mpaka majina ya mabasi na kiwango cha nauli tena hizi mpya.

Karibu Mtwara Mkuu! Huku mgeni salamu ni.... Itatoka? Tafadhali jibu "haitoki" vinginevyo balaa litakupata. Kwa kifupi jaribu kujiepusha na mijadala ya kuhusu gesi hasa ukiwa mgeni hata kama msimamo wako ni kama wa kwao. Mpaka watakapokuwa na imani kuwa wewe si mamluki.
 
Booking either Ubungo au Tandika Sudan
 
Suala la usafiri wa Mtwara mkuu lilishajadiliwa humu jf,labda kama unaenda kuangalia uwezekano wa kutoka kwa gesi,maana hata hapo unapotokea nna mashaka umetumwa..NENDA KAMANDA,ITATOKA TU.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…