Safari yangu ya Machimbo Msumbiji

Safari yangu ya Machimbo Msumbiji

Ukweli ni uchimbaji kw mozambique kidogo afadhali kunat upatikanaji wa madini kuliko tz,huko huko monte puez kuna eneo linatoa dhahabu inaitwa malupa ipo karibu na inapopatikana ruby
 
Zilikuja taarifa kuwa Kuna madini yamegunduliwa Mozambique na watu wengi wanakimbilia huko, Rafiki zangu kadhaa na watu wengi ninao wafahamu waliacha shuguli zao na kuingia kwenye Mkumbo huo, wengi wao walirudi kimya kimya na kujikita kwenye shuguli zao bila hata kueleza kilichojiri huko.

Hiyo ilikuwa ni miaka kadhaa nyuma, Mwaka 2012 mwishoni kijana mmoja ambaye nilikuwa namtumia sana kwenye shuguli zangu za kusafisha Mabanda ya Kuku n.k aliniomba ruhusa ya kwenda Mozambique kujaribu bahati yake, hii ilikuwa ni baada ya tetesi za kugungulika madini ya RUBI katika eneo la MTIPWEZI. Safari hii utitiri wa Vijana ambao walikuwa wanamiminika kuelekea eneo hilo ulikuwa ni mkubwa zaidi. Tofauti na Mwanzo safari hii wengi walirudi na majibu mazuri, wengi walirudi wakiwa wamepata kati ya 5,000,000 mpaka milioni 50.

Yuko Mtu mmoja ambaye alielekea huko kama kuficha fedheha yake baada ya kufumaniwa na Mke wa Mkuu wa kituo cha polisi, yeye alirudi meno nje baada ya kuambulia dola15,000 huku akisahau yale yote ambayo yalimkuta, lakini kubwa ni kwa huyu aliyekuwa mfanyakazi wangu ambaye aliweza kupata kiasi cha Shilingi milioni 80. Aliporudi alikuja kunishukuru na kuniachia shilingi milioni 2. Kitendo cha kijana huyo ambaye alikuwa choka mbaya kurudi na mafanikio makubwa kiasi hicho kilimshawishi rafiki yangu wa karibu ambaye anamiliki Mashamba, mifugo, duka la spea za pikipiki na mashine ya kusaga naye kujaribu bahati yake.

Waliondoka watu wanne, ilimchukuwa wiki mbili tu naye kurudi akiwa na kiasi cha shilingi milioni 140 baada ya mgao wa watu watatu kufuatia kifo cha mwenzao mmoja ambaye alifia hukohuko akiwa shimoni.

Ikafika zamu yangu, Niliondoka mwezi wa kwanza 2014 kuelekea MTIPWEZI nilipitia Kilambo Mtwara pale tulivushwa na boti kwa Tsh 10,000 (ukivuka na pantoni ni tsh 500 (mia tano)) Tukafika eneo maarufu la uhamiaji la msumbiji linaloitwa NAMOTO, nikiwa na pasport yangu ya ujirani mwema lakini wewe kama unataka kwenda kwa kutokea huku Tanzania ni rahisi zaidi ukipitia Chikongo (uliza tu) nilipita vijiji kadhaa kama Kiyonga hadi kutokea wilaya ya Palma, hapo nilipumzika kwa siku moja kabla ya kuendelea na safari iliyonifikisha Musimbwa.

Nilipumzika Musimbwa kwa siku mbili kabla yakuendelea na safari, Nilikuwa peke yangu sikuongozana na yeyote yule, wenyeji wangu walinieleza ugumu wa ninakoenda lakini wakanipa moyo kuwa wengi hufanikiwa huko ingawa wao hakuna aliyejaribu bahati hiyo.

.Baada ya mapumziko hayo jiooni ya siku iliyofuata nikaingia Rasmi eneo la machimbo linalojulikana kama MTIPWEZI, Miongoni mwa vitu ambavyo vilinisisimua ni kukutana na rafiki yangu ambaye tuliachana mara ya mwisho baada ya kumaliza Darasa la saba, ni miaka mingi wengi walikuwa hawajui yuko wapi lakini nimemfuma huko, yeye alikuwa wa kwanza kunitambua na kustaajabu baada ya kuniona nikiwa na kitambi (Nimeanza kukiondoa) hakujua kuwa licha ya kitambi changu nina mazoezi ya kutosha kuweza kupiga kazi za kuchimba

Siku ya pili nikaanza kazi baada ya kujiunga na watu wanne ambao nilikutana nao huko, wawili walikuwa ni wa Msumbiji, mmoja Mtanzania na yule mwingine alikuwa anatoka Zimbabwe, miongoni mwa maswali niliyoulizwa ni kama nilikuja na dawa yoyote ya kunisaidia katika mashimo, nikawajibu kuwa sina walinicheka sana wakisema kuwa nimekuja kitoto, yule mmoja wa Mozambique alinionyesha Korodani za Binadamu alizodai kuwa ni za mjombaake na amekuja nazo ili ziweze Kumsaidia. Sikuuliza kama kamuua au ilikuwaje kwani nilishaingiwa na woga na kundi hili na wala sikutaka kuuliza hao wengine wamefanya nini.

Ilipofika saa mbili usiku tukiwa tuko eneo la machimbo ilisikika milio ya Risasi, Shimo letu halikuwa kubwa sana Hivyo tuliwahi kuchomoka na kukimbia. Watu walikuwa wanakimbia ovyo kunusuru maisha yao wengine walikamatwa na tulionusurika ndio hivyo tena tulijichanganya maporini. Ndugu yangu usifanye mchezo na njaa ya siku mbili. Kitu nilichoambiwa (sijathibitisha) Ni kuwa wale wanaokamatwa huuwawa na kutupwa kwenye mashimo ya madini.

Tulikutana na mambo mengi sana, nafasi haitoshi kusimulia yote hayo, ni katika kisa ambacho nimeshuhudia mwenzetu ambaye tulikimbia naye akiiaga dunia.

Tofauti na Wenzangu mimi nilikuwa na ile TEMPORARY PASPORT hivyo sikupata shida kuingia katika eneo lolote lile. Niliachana na wenzangu katika kijiji kimoja ambako Nyoka huwa wanaliwa sana, wanaitwa CHIDUDU ukisikia chidudu kama huli nyoka acha maana inafanana sana na Samaki.

Kutoka hicho kijiji niliweza kusafiri hadi PALMA, Palma nilikutana na fursa kadhaa ambazo zilinifanya nijaribu kuwashawishi wanaJF humu ndani kuweza kuchangamkia fursa hizo lakini kama kawaida wengi walionekana kutoniamini, nilijua ilikuwa ni vigumu kuniamini lakini ulikuwa ni mpango mzuri ambao wachache ambao walichangamkia Fursa hizo wamefanikiwa sana (sio niliowashawishi mimi)

Mwisho napenda niwaeleze kuwa mafanikio yana mapito yake ambayo ni magumu kweli kweli kwa yeyote ambaye atakutana na mikasa kama hiyo basi hatakiwi kukata tamaa bali azidi kukaza Buti.

NAWATAKIA ASUBUHI NJEMA.

Fursa zipi izo???
 
Kutoka boda mt.hd msimbwa panaumbali gan kama ukiwa bongo? Kiasi gani cha nauli in tz shs.
 
Sio mara zote kuwa kuna vurugu, huwa inatokea kwa muda mfupi tu na upatikanaji
wa madini ni rahisi kidogo kuliko Bongo maana kuna idadi ya watanzania wengi
walioambulia kati ya mil 50 mpaka 150 na wako wachache milioni 200 mpaka 900

Mkuu nipe ramani nzima nataka niende mwezi ujayo au kama kuna mtu anaenda niunganishe naye njoo Pm zaidi nipo tayari kwa lolote

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ingekuwa hollywood wangeshatengenezea muvie
 
Duh, hao wenyewe waliochukua wamekosa, wengine hawachukui chochote na wanapata
kuna wengine walienda mwezi uliopita wako watatu hawakuwa na uchawi wala nini lakini
wamebongoa 1.4 bilion.

Je unajua walienda na sh.ngap mpaka wakapiga pesa ndefu hivo?
 
mkuu nipe ramani nzima nataka niende mwezi ujayo au kama kuna mtu anaenda niunganishe naye njoo pm zaidi nipo tayari kwa lolote

sent from my blackberry 8520 using jamiiforums

sahvi bdo uende mwezi wa kumi namoja kipindi cha mvua ndyo kuna unafuu sbb ya maji shv maji hayapo utapata shda.chamuhimu tegea kipindi cha mvua.hata na hvyo dili sahvi haiko km zamani sahvi hela ni ya bahati nahakuna prukushani km awali.wengi wamekimbilia malupa kwenye dhahabu.
 
Je walikudokeza wameenda na mtaji wa sh.ngap?

HAKUNA MTAJI WATU WANAENDA KWA BAHATI,WAPO WALIOENDA WAKUKUTANA NA BAHATI KUBWA,KWAWALE WAZOEFU KUNA MTU KM ndaki jina kubwa huko alipiga bilion2 yupo male naye alipiga milion 900.huyu male alitoka songea na usafiri wa kudandia kwa side mpare mnunuzi wa madini maurufu pale songea.NIMETAJA MAJINA YAWATU JAPO CYO USTAARABU ILA NI WATU WENYE MAJINA MAKUBWA KWA WACHMBAJI
 
wewe ulikuwepo kipindi gani huko mimi nilikuwepo huko mwaka juzi....ila nilipashindwa kutokana na mfumo mzims ws biashara, elewa msumbiji hawatoi vibali vya kuchimba madini maeneo yote mliyokuwa mnaenda kusaka ruby ni maeneo ya ma branco....ndomana ukidakwa wana kutemesha hela na mawe.mtoa mada unamkumbuka rambo (r.I.p)
 
arola54@.......gemstones haina formula....unaweza ukanunua jiwe la 2mln ukaenda liuzaaaa 30mln, au pia ukaliyza laki mbili.kikubwa ni kujua nunua jiwe na kuchagua na kijua uza basi
 
Biashara ya madini hasa hayo ya wachimbaji wadogo . Story zake hazina tofauti na biashara yeyote haramu kama drugs....etc. Mfanyabiashara wa madini hata kama angekuwa baba yako mzazi hakuna siku atakuambia full story ya ukweli. Atakupiga blah blah tu.......kifupi usiamini story yeyote ya mtu wa madini. Ukitaka kupoteza hela au ku risk maisha yako msikilize. Ila hatakuja kukueleza ukweli kamwe .
 
Bonge la story !

... la muhimu nawe GAZETI uliambulia 2M za dogo
 
Last edited by a moderator:
wewe ulikuwepo kipindi gani huko mimi nilikuwepo huko mwaka juzi....ila nilipashindwa kutokana na mfumo mzims ws biashara, elewa msumbiji hawatoi vibali vya kuchimba madini maeneo yote mliyokuwa mnaenda kusaka ruby ni maeneo ya ma branco....ndomana ukidakwa wana kutemesha hela na mawe.mtoa mada unamkumbuka rambo (r.I.p)
No ninayemkumbua sana ni yule askari anaitwa Tomas, anapiga watu kwa mianzi
si mchezo.
 
Mimi nishaenda sana kule tena naona watu wa kule au serekali yao ni nzuri ingekuwa machimbo yale yako hapa tz mpaka sasa yangekuwa chini ya kampuni moja ya kigeni na asingesubutu kufika mtu lakini kule robo tatu ya wachimbaji na wanaonunua na kuuzia wathailand na wasirlanka ni wageni wabongo na watu wa afrika magharibi tena bila vibali vyovyote na machimbo yale yana mwaka wa tano sasa, yaan ukifika hapo montepuez utafikiri uko tz watanzania wako wengi sana na polis wanaoleta fujo ni wale wakutoka mkoani pemba na wanakuja mara mojamoja ila kama ni mgeni ukiwakuta hao wa pemba utatamani siku hiyohiyo urudi tz.
 
Mimi nishaenda sana kule tena naona watu wa kule au serekali yao ni nzuri ingekuwa machimbo yale yako hapa tz mpaka sasa yangekuwa chini ya kampuni moja ya kigeni na asingesubutu kufika mtu lakini kule robo tatu ya wachimbaji na wanaonunua na kuuzia wathailand na wasirlanka ni wageni wabongo na watu wa afrika magharibi tena bila vibali vyovyote na machimbo yale yana mwaka wa tano sasa, yaan ukifika hapo montepuez utafikiri uko tz watanzania wako wengi sana na polis wanaoleta fujo ni wale wakutoka mkoani pemba na wanakuja mara mojamoja ila kama ni mgeni ukiwakuta hao wa pemba utatamani siku hiyohiyo urudi tz.

gemstones kule hawatowi kibali kuchimba...mimi nishakwenda na mthailand mmoja alifikia huku tz kwa prayun ..basi aliposkia mazingira ya kule danger ah hakuvuka bordet kabisa...tz ndiyo wageni wanajiachia wanavyotaka
 
sahvi bdo uende mwezi wa kumi namoja kipindi cha mvua ndyo kuna unafuu sbb ya maji shv maji hayapo utapata shda.chamuhimu tegea kipindi cha mvua.hata na hvyo dili sahvi haiko km zamani sahvi hela ni ya bahati nahakuna prukushani km awali.wengi wamekimbilia malupa kwenye dhahabu.

Juzi nilikuwa TANDAHIMBA kuna jamaa yangu 1 Pale amenipa hizo Stori akanithibitishia kwamba nikweli watu wanapiga NOTI sana nasio madini tu anasema kwa jins wabongo tulivyo wajanja Pesa iko Nje..!Alichonambia Mwishoni mwa Mwaka huu wanauchaguzi sasa kiusalama sio kuzuri Kwenda Huyo jamaa yangu yy ni mwenyeji sana wakule so Amenambia nikiwa tayari atanipeleka hadi Kwenye Serikalo ya mtaa kunitambulisha wanasema MFUNGWA hachagui Gereza pambana kila iwezekanavyo ili hata cku unazimika Watt wako wawe na Sababu yakukulilia kuwa wamepoza kifaa sio wakulilie km ilivyokawaida Manake watakusahau mapema...
 
Ipo siku nitatembelea huko.
Ngoja nijipange.
cc Gemmy
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom