Safari yangu ya Machimbo Msumbiji

Safari yangu ya Machimbo Msumbiji

habari zenu zinasisimua na kuhuzunisha hapohapo, hebu tupeni kamili kamili mnatuonjesha kidogo tu inatuachia maswali mengi

Uliza tu mkuu, tutakayoweza tutayajibu.
 
Maisha ni Safari iliyo jaa kila aina ya visa na mikasa
 
Wakasitisha lile zoezi la kuchana pasi wakanisogelea na kunyang'anya pasi yangu, wakaichana na yule bosi wao akanitemea mate usoni, bahati nilikuwa na PPV

.
Hili la kuchana pasi lipo sana hasa ukitumia zile za muda, nashukuru mkuu kwa kunikumbusha
kitu ambacho nilikisahau tabia hii wanayo sana askari wa NAMPULA.
 

Kutoka hicho kijiji niliweza kusafiri hadi PALMA, Palma nilikutana na fursa kadhaa ambazo zilinifanya nijaribu kuwashawishi wanaJF humu ndani kuweza kuchangamkia fursa hizo lakini kama kawaida wengi walionekana kutoniamini, nilijua ilikuwa ni vigumu kuniamini lakini ulikuwa ni mpango mzuri ambao wachache ambao walichangamkia Fursa hizo wamefanikiwa sana (sio niliowashawishi mimi)

Hii ndiyo ya muhimu zaidi katika stori nzima! Unaweza kuirejelea mkuu? au kama kuna thread uliwahi kuanzisha unaweza kunipoint ilipo.
 
Mengi aliyoandika mkuu hapa ni ukweli tupu.
Kule Mtepweshi (Monte Puez) ni kama ilivyo sehem yoyote yenye machimbo yasiyo rasmi, ni bahati tu! Jambo la usalama kule siku hizi liko vizuri kiasi, pamoja na chuki za wenyeji lakini watu wanaishi vizuri na wanapiga pesa, siku hizi watu wanakomaa na mamlaka zinasimamia sheria kiasi japo si sana. Ukienda kule siyo unazama shimoni, wewe nunua na kuuza mawe, Wathai wamejaa tele kule, changamoto ni ujambazi lakini sehemu yoyote yenye pesa njenje hhilo ni jambo la kawaida! siyo ajabu kumkuta mtu na bilini moja chumbani ni kawaida sana.
 
Sehemu zenye "purukushani za pata potea" ndo zinanifaa sana mimi. Nshahadithiwa sana ya huko Msumbiji, ipo siku ntajitosa huko liwalo na liwe potelea mbali hata nikiliwa na mamba wa mto ruvuma!
Mkuu GAZETI tafadhari ndg rejea huo uzi ndg yangu itakuwa jambo jema sana nikaenda na bidhaa pendwa huko hata roba la "mjani"
Ila hii mambo ya ulozi nimeisikia sana kama unataka upige hela kule machimbo.
Anyway nimekumbuka kitu hapa, ntapitia kwa mzee Jenga (mkuu wa kikosi cha jadi kinaitwa Mwano kule ukaguruni) anichanje dawa ya kuzuia risasi. Pia ntaenda Tanga nikachanjie "muku" ili ikitokea waasi wa LENAMO wamenibamba basi wakinikata mapanga yao yanadunda. Kisha ntaenda kwa "wanungule" wanipe ile dawa ya kujipaka usoni ili nisionekane na mtu yeyote yule popote nipitapo. Na hatimae ntamfuata mzee Bule anipe zile kucha za "muhanga" kwajl ya kuchimbia madini.
Oop mbona mzunguko mkubwa hivi ntaweza kweli!?
 
Last edited by a moderator:
Hii ndiyo ya muhimu zaidi katika stori nzima! Unaweza kuirejelea mkuu? au kama kuna thread uliwahi kuanzisha unaweza kunipoint ilipo.
Mkuu, kuna mambo niliwaelekeza wanajamvi ambayo yalihitaji pesa kidogo
ili kuweza kutengeneza fedha ya maana lakini nikaishia kuitwa tapeli ingawa
kuna waungwana wachache waliniuliza kiundani VIA PM lakini waliponiuliza
wao walikuwa wamekwishachelewa kwani mimi nilikuwa nimerudi kutoka eneo
husika hivyo Muamala wowote ambao ningeufanya muda huo ungekuwa ni utapeli.
 
Zilikuja taarifa kuwa Kuna madini yamegunduliwa Mozambique na watu wengi wanakimbilia huko, Rafiki zangu kadhaa na watu wengi ninao wafahamu waliacha shuguli zao na kuingia kwenye Mkumbo huo, wengi wao walirudi kimya kimya na kujikita kwenye shuguli zao bila hata kueleza kilichojiri huko.

Hiyo ilikuwa ni miaka kadhaa nyuma, Mwaka 2012 mwishoni kijana mmoja ambaye nilikuwa namtumia sana kwenye shuguli zangu za kusafisha Mabanda ya Kuku n.k aliniomba ruhusa ya kwenda Mozambique kujaribu bahati yake, hii ilikuwa ni baada ya tetesi za kugungulika madini ya RUBI katika eneo la MTIPWEZI. Safari hii utitiri wa Vijana ambao walikuwa wanamiminika kuelekea eneo hilo ulikuwa ni mkubwa zaidi. Tofauti na Mwanzo safari hii wengi walirudi na majibu mazuri, wengi walirudi wakiwa wamepata kati ya 5,000,000 mpaka milioni 50.

Yuko Mtu mmoja ambaye alielekea huko kama kuficha fedheha yake baada ya kufumaniwa na Mke wa Mkuu wa kituo cha polisi, yeye alirudi meno nje baada ya kuambulia dola15,000 huku akisahau yale yote ambayo yalimkuta, lakini kubwa ni kwa huyu aliyekuwa mfanyakazi wangu ambaye aliweza kupata kiasi cha Shilingi milioni 80. Aliporudi alikuja kunishukuru na kuniachia shilingi milioni 2. Kitendo cha kijana huyo ambaye alikuwa choka mbaya kurudi na mafanikio makubwa kiasi hicho kilimshawishi rafiki yangu wa karibu ambaye anamiliki Mashamba, mifugo, duka la spea za pikipiki na mashine ya kusaga naye kujaribu bahati yake.

Waliondoka watu wanne, ilimchukuwa wiki mbili tu naye kurudi akiwa na kiasi cha shilingi milioni 140 baada ya mgao wa watu watatu kufuatia kifo cha mwenzao mmoja ambaye alifia hukohuko akiwa shimoni.

Ikafika zamu yangu, Niliondoka mwezi wa kwanza 2014 kuelekea MTIPWEZI nilipitia Kilambo Mtwara pale tulivushwa na boti kwa Tsh 10,000 (ukivuka na pantoni ni tsh 500 (mia tano)) Tukafika eneo maarufu la uhamiaji la msumbiji linaloitwa NAMOTO, nikiwa na pasport yangu ya ujirani mwema lakini wewe kama unataka kwenda kwa kutokea huku Tanzania ni rahisi zaidi ukipitia Chikongo (uliza tu) nilipita vijiji kadhaa kama Kiyonga hadi kutokea wilaya ya Palma, hapo nilipumzika kwa siku moja kabla ya kuendelea na safari iliyonifikisha Musimbwa.

Nilipumzika Musimbwa kwa siku mbili kabla yakuendelea na safari, Nilikuwa peke yangu sikuongozana na yeyote yule, wenyeji wangu walinieleza ugumu wa ninakoenda lakini wakanipa moyo kuwa wengi hufanikiwa huko ingawa wao hakuna aliyejaribu bahati hiyo.

.Baada ya mapumziko hayo jiooni ya siku iliyofuata nikaingia Rasmi eneo la machimbo linalojulikana kama MTIPWEZI, Miongoni mwa vitu ambavyo vilinisisimua ni kukutana na rafiki yangu ambaye tuliachana mara ya mwisho baada ya kumaliza Darasa la saba, ni miaka mingi wengi walikuwa hawajui yuko wapi lakini nimemfuma huko, yeye alikuwa wa kwanza kunitambua na kustaajabu baada ya kuniona nikiwa na kitambi (Nimeanza kukiondoa) hakujua kuwa licha ya kitambi changu nina mazoezi ya kutosha kuweza kupiga kazi za kuchimba

Siku ya pili nikaanza kazi baada ya kujiunga na watu wanne ambao nilikutana nao huko, wawili walikuwa ni wa Msumbiji, mmoja Mtanzania na yule mwingine alikuwa anatoka Zimbabwe, miongoni mwa maswali niliyoulizwa ni kama nilikuja na dawa yoyote ya kunisaidia katika mashimo, nikawajibu kuwa sina walinicheka sana wakisema kuwa nimekuja kitoto, yule mmoja wa Mozambique alinionyesha Korodani za Binadamu alizodai kuwa ni za mjombaake na amekuja nazo ili ziweze Kumsaidia. Sikuuliza kama kamuua au ilikuwaje kwani nilishaingiwa na woga na kundi hili na wala sikutaka kuuliza hao wengine wamefanya nini.

Ilipofika saa mbili usiku tukiwa tuko eneo la machimbo ilisikika milio ya Risasi, Shimo letu halikuwa kubwa sana Hivyo tuliwahi kuchomoka na kukimbia. Watu walikuwa wanakimbia ovyo kunusuru maisha yao wengine walikamatwa na tulionusurika ndio hivyo tena tulijichanganya maporini. Ndugu yangu usifanye mchezo na njaa ya siku mbili. Kitu nilichoambiwa (sijathibitisha) Ni kuwa wale wanaokamatwa huuwawa na kutupwa kwenye mashimo ya madini.

Tulikutana na mambo mengi sana, nafasi haitoshi kusimulia yote hayo, ni katika kisa ambacho nimeshuhudia mwenzetu ambaye tulikimbia naye akiiaga dunia.

Tofauti na Wenzangu mimi nilikuwa na ile TEMPORARY PASPORT hivyo sikupata shida kuingia katika eneo lolote lile. Niliachana na wenzangu katika kijiji kimoja ambako Nyoka huwa wanaliwa sana, wanaitwa CHIDUDU ukisikia chidudu kama huli nyoka acha maana inafanana sana na Samaki.

Kutoka hicho kijiji niliweza kusafiri hadi PALMA, Palma nilikutana na fursa kadhaa ambazo zilinifanya nijaribu kuwashawishi wanaJF humu ndani kuweza kuchangamkia fursa hizo lakini kama kawaida wengi walionekana kutoniamini, nilijua ilikuwa ni vigumu kuniamini lakini ulikuwa ni mpango mzuri ambao wachache ambao walichangamkia Fursa hizo wamefanikiwa sana (sio niliowashawishi mimi)

Mwisho napenda niwaeleze kuwa mafanikio yana mapito yake ambayo ni magumu kweli kweli kwa yeyote ambaye atakutana na mikasa kama hiyo basi hatakiwi kukata tamaa bali azidi kukaza Buti.

NAWATAKIA ASUBUHI NJEMA.

Usije kuwa umefuata koro.da.ni za mjomba wako tafadhali hii shughuli waachie alshaabab
 
Ila kiukweli sijawahi fika huko lakin ilikuwa almanusra 2009 niende..
Jamaa yangu mmoja hapa Dar alinishauri tukajaribu bahati yamadini ama mbao. Lakin kwa bahati mbaya ama nzuri nikapata mchongo mwingine hapa hapa isipokuwa nina ndugu zangu naona wanatanua mmmno sasa hivi mijumba mikubwa lakini walikuwa hawatambuliki ukiuliza wanakwambie safari za Mozambique.
Kwahyo mimi nawapa moyo mwenye nia aende akajaribu bahati.
 
Umenikumbusha mbaaali sana mkuu GAZETI. Nakumbuka miaka hiyo nilikuwa maeneo ya huko na uchumi ulikuwa umevurugika sana watu walikuwa hawana pesa na matukio ya wizi

wa kuvamiwa usiku yalikuwa ya kawaida sana.jjj Ujio wa hayo machimbo ulikuwa ahueni kubwa sana kwani wimbi la watu mamia kwa maelfu walienda machimbo na wengine wengi walipita kila uchao na kuelekea machimbo huku wengi wakiwa na ndoto ya kubadilisha maisha yao wenyewe wakiita "kubongoa".


Na kweli kuna watu waliokuwa hoi kimaisha walibadilika baada ya kurudi toka huko machimbo. Kipindi hicho madini yalichimbwa upande wa Tanzania kabla hayajapungua na kulazimisha watu kuvuka msumbiji. Lakini kwa bahati mbaya sana na pengine kutokana na ugumu wa maisha au ulimbukeni wengi ya "wabongoaji" walirudi na msafara wa magari ya kukodi kama wafalme na kufunga mahoteli na baa huku wakiosha magari waliyoyakodi kwa bia (nimeshudia mwenyewe sijasimuliwa). Matokeo yake wengi wao walirejea hali duni kuliko hata walizokuwa hapo nazo mwanzo.
 
Kama kuna mtu alikua huko machimbo mwaka huu atujurishe hali ipo vp kwa sasa nataka niende hali mbaya umri unaenda pesa akuna wacha nijitoe

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mimi niko zangu huku rock city jamaa zangu wanahangaika migodi yote ccm wamejimilikisha sasa nitawashauri waende kule japo ni mbali sana toka huku
 
Usije kuwa umefuata koro.da.ni za mjomba wako tafadhali hii shughuli waachie alshaabab
Duh, hao wenyewe waliochukua wamekosa, wengine hawachukui chochote na wanapata
kuna wengine walienda mwezi uliopita wako watatu hawakuwa na uchawi wala nini lakini
wamebongoa 1.4 bilion.
 
Kama kuna mtu alikua huko machimbo mwaka huu atujurishe hali ipo vp kwa sasa nataka niende hali mbaya umri unaenda pesa akuna wacha nijitoe

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Sio mara zote kuwa kuna vurugu, huwa inatokea kwa muda mfupi tu na upatikanaji
wa madini ni rahisi kidogo kuliko Bongo maana kuna idadi ya watanzania wengi
walioambulia kati ya mil 50 mpaka 150 na wako wachache milioni 200 mpaka 900
 
mimi niko zangu huku rock city jamaa zangu wanahangaika migodi yote ccm wamejimilikisha sasa nitawashauri waende kule japo ni mbali sana toka huku

Kweli mkuu yaani mpaka Wanigeria wapo huko.
 
tuna wachimbaji wakitanzania wengi wametolewa kwa nguvu sehemu mbalimbali ndani ya tanzania kwa sababu mbalimbali za kisheria hadi kupelekea vifo vya baadhi ya wachimbaji.
Japo kuna ukweli wa matumizi ya nguvu kupita kiasi stahili kwa majeshi ya msumbiji, watanzania wanaofanya kazi kihalali wapo wengi katika majimbo mbalimbali ndani ya msumbiji na wanafanikiwa kwa kufuata tafatibu zilizowekwa.
Kuna msukuma mmoja nilikutana naye Katika sekeseke hilo akanifahamisha kuwa hizi Vurugu ninazoziona
huku Mozambique ni cha Mtoto ukilinganisha na hatari iliyopo kwa kuchimba TZ, alisema Tz ni ngumu sana
kupata fursa ya kuchimba kirahisi n kufanikiwa kama ilivyo Mocambique, Nilishangaa sana.
 
Kuna msukuma mmoja nilikutana naye Katika sekeseke hilo akanifahamisha kuwa hizi Vurugu ninazoziona
huku Mozambique ni cha Mtoto ukilinganisha na hatari iliyopo kwa kuchimba TZ, alisema Tz ni ngumu sana
kupata fursa ya kuchimba kirahisi n kufanikiwa kama ilivyo Mocambique, Nilishangaa sana.

mozambiq bado mbichi na tumaini kwa watafutaji, nikijaaliwa wepesi nitavuka robo ya mwaka ya kwanza mwakani ila nitegemea kujikita jimbo la tete.
 
Back
Top Bottom