Selle Milao
Member
- Mar 30, 2016
- 32
- 30
Mimi mwana Dar es salaam mzaliwa wa Amana Hospital kabila Mkwele na Uzaramo mchanganyiko.
Nimekuwa na kawaida kutembelea maeneo tofauti kitika nchi yangu ninapopata nafasi baadhi ya maeneo niliofika Gombe na Mahale, Rubondo, Mikumi, Saadan, Tarangire na baadhi hifadhi list ndefu.
Kondoa hapa nilipapenda kutokana na ukalimu na mgeni wanakufanya ujione mwenyeji.
Baadhi ya maeneo niliotembelea Kolo hapa kuna michoro ya mapangoni ina zaidi ya miaka 1500 pia kabla ujaenda huko kuna Makumbusho ndogo hapa utajifunza mila na tamaduni za wenyeji wa Kondoa nimebatika kufika kwenye Nyumba ya mtemi Kimolo kitu cha ajabu kwenye hii nyumba kuna mlango ulijifunga wenyewe siku ya mazishi ya Mtemi hadi leo ujafunguliwa
Nimezunguka sehemu nyingi Baadhi ni Haubi, Masange, Bereko,Itololo, Kisese, Sambwa, Busi na mengineo

