Safari ya Kuzimu - Mwili hubaki duniani

Safari ya Kuzimu - Mwili hubaki duniani

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,507
Reaction score
45,129
Wanabodi,

Safari ya kuzimu haihitaji mwili wako, kinachokwenda kuzimu ni nafsi yako tu. sasa kama unakwenda huko moja kwa moja basi mwili wako huzikwa na ndugu zako kama msiba wa kawada, lakini kama unakwenda huko kwa lengo la kufanya kafara ama matambiko mbalimbali basi mwili wako hutunzwa hapa duniani na unaporudi unaukuta unauvaa na kuendelea na maisha yako. Count ya miaka ya kuzimu si sawa na ya hapa duniani, unaweza ukajiona umekaa kuzimu kwa wiki moja tu kumbe hapa duniani unakuwa haupo kwa miaka 10 na zaidi.

Ukitaka kuelewa sayansi ya ki-dunia kuhusu uumbaji wa mwanadamu ni lazima kwanza ujue namna ya kutenganisha Mwili na Nafsi. Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Mwili ni cover ya Nafsi ingawa Nafsi inaweza ku-exist yenyewe kama unajua namna ya kuitenganisha na mwili, Nafsi haionekani kwa macho lakini Mwili unaonekana. Unapozaliwa tu Nafsi yako huvishwa Mwili na ndipo unapotokea duniani na wazazi, ndugu na jamaa wanakushangilia.

Hata mchawi lazima atengue namna ya kuichota nafsi yako kwanza ili afanikishe azma yake, akishindwa basi anaweza kuroga ama kuudhuru mwili.

Sitaki kukuchanganya zaidi, lakini kumbuka kwamba safari ya Kuzimu haihitaji Mwili bali kinachohitajika ni nafsi, na unaweza kutenganisha Mwili na Nafsi na kinacho-control mfumo mzima wa maisha yako ni Nafsi.

Kwa hiyo nikishaikamata Nafsi yako basi naweza kukufanya wewe ukawa TV na mimi nikawa ndiyo Remote control yako na utafuata kila kitakacho mimi.
 
Haya mambo yana wenyewe aseee.Ngoja nipite mbali,afu unazo nafsi ngapi kwa sana unazozi control mkuu??
 
Blue Monday

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Hebu ajitolee mwana jf mmoja awe tv hlf jamaa awe remote.. hlf aje atuletee mrejesho
 
Haya masomo huwa ni magumu sana yanahitaji imani zaidi ya akili.. akili itakufanya ufanye tafiti kwa vitu vinavyoonekana na kushikika lakini hutapata jibu ya mambo hayo ya imani. Na kwenye issue ya nafsi hapo ndo mwisho wa kufikiria kwa mwanadamu.. Anafikiria anayoyaona na kuyashika unseen ni shida.
 
Haya masomo huwa ni maumu sana yanahitaji imani zaidi ya akili.. akili itakufanya ufanye tafiti kwa vitu vinavyoonekana na kushikika lakini hutapata jibu ya mambo hayo ya imani. Na kwenye issue ya nafsi hapo ndo mwisho wa kufikiria kwa mwanadamu.. Anafikiria anayoyaona na kuyashika unseen ni shida.
Mkuu siri ya uumbaji ndiyo ipo hapo, lazima ujifunze zaidi kwa kutumia vitu visivyoonekana. Kwa mfano wakristo huamini Roho mtakatifu lakini je walishamwona kwa macho huyo Roho mtakatifu? Je wakimwomba anawasaidia? jibu watakuambia "Yes"

Sasa kama binadamu wewe utangonja kuona kwanza ndipo usadiki aisee una kazi ngumu mno kujua wewe ni nani, je ni nguvu zipi ulizopewa na Mwenyezi Mungu lakini hujui kuzitumia na je ni kwa nini upo hapa duniani.

Elimu hii inafurahisha ukishaanza kujifunza.
 
Haya mambo yana wenyewe aseee.Ngoja nipite mbali,afu unazo nafsi ngapi kwa sana unazozi control mkuu??
wenyewe ndiyo wewe, usiogope haya ndiyo mambo makuu yanayokuzunguka kwenye maisha yako, lazima ujitahidi kuyafahamu.
 
Back
Top Bottom