Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 5,581
- 10,110
Nsekela alianza kazi benki ya CRDB mwaka 1997 akiwa afisa mdogo, lakini mwenye kiu ya maarifa na bidii ya kazi.
Hakusimama. Alijifunza kwa vitendo, akaelewa mteja, akaelewa mifumo, na akaelewa taswira pana ya taasisi hiyo. Ndani ya miaka michache tu, alipanda ngazi kuwa Meneja Uhusiano, kisha Meneja Uhusiano Mwandamizi.
Mwaka 2008, alihama na kujiunga na NMB, ambako aliimarika zaidi kitaaluma. Alisimamia miradi mikubwa, alibuni huduma rafiki kwa wateja, na kuonesha uwezo wa kuliongoza soko lenye ushindani. ?
Huko, alijijengea heshima kama mmoja wa wasomi na watendaji bora wa sekta ya benki.Miaka ilipita, na Juni 2018, CRDB ilimrudisha tena lakini safari hii si kama afisa, bali kama Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.
Hatua hii ilikuwa ya kihistoria, kwani alirithi nafasi ya Dkt. Charles Kimei, mtu aliyewahi kumpa cheti miaka mingi nyuma.Leo, chini ya usukani wa Nsekela, CRDB imeendelea kustawi, kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi, na kukumbatia teknolojia ya kisasa. Safari yake ni ushuhuda wa jinsi mtu mwenye maono, nidhamu, na uvumilivu anaweza kupanda kutoka ngazi ya chini hadi uongozi wa kilele.
Kwa mafanikio yake, unyenyekevu wake, na ujasiri wake wa kuchukua hatua kubwa katika maisha Abdulmajid Nsekela si tu kiongozi bora, bali pia ni kielelezo cha kuigwa kwangu. Yeye ni role model wangu wa kweli.
c&p Mkongo