Safari ya India

MONA WA KYEN

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
340
271
habari za humu ndani wana jamii forum. ninaomba msaada kwenu kwani kuna ndugu yangu ameniomba nimsindikize kwa ajili ya matibabu hospitali inayoitwa APPOLO NEW DELH India. nimemkubalia kumsindikiza ana matatizo ya figo, kuna mtu tunaenda nae atakaempa figo wameshakubaliana ila naenda tu kama msindikizaji. kiukweli ndo mara yangu ya kwanza kusafiri kwenda india, na pia kutoka nje ya nchi. ninaomba mnieleweshe natakiwa kuwa na vitu gani, na nifanye vitu gani sasa hivi mana safari ni next week, na nikiwa kule kazi yangu kubwa itakuwa ipi kwa ambao mshaenda asanteni
 
passport naenda kuichukua jumatatu mungu akipenda
 
Jifunze kihindi na uchukue dola kidogo na pia ujue anuwani ya balozi watz.
Na pia jihadhari na wadokozi na usipoteze vitambulisho vyako. weka kopi.
 
Sasa hivi ni kipindi cha baridi. Uwe na mavazi stahiki kwa baridi.
2. Ni rahisi zaidi kufikia kwenye "guest houses", hizi ni apartments bei ni kati ya $20 - 50. Hotels are expensive.
3. Ukiwa guest house ni rahisi kupika chakula utakacho, hata ugali. Chakula cha kihindi pilipili usiseme.
4. Unaweza pia kubeba mchele na unga kiasi cha kutosha muda utakaokaa huko.
 
ahaa asante sana nashukuru. tax au wanatumia usafiri gani? wizi je?
 
Jifunze kihindi na uchukue dola kidogo na pia ujue anuwani ya balozi watz.
Na pia jihadhari na wadokozi na usipoteze vitambulisho vyako. weka kopi.
ahaa asante yanapatukana wapi mawasiliano yake? wadokozi mbinu zao ni zipi mkuu?
 
Culture shock! Utawakuta maskini kuliko maskini wa huku kwetu, kama una vijichenchi uwe unawatupia,pia utakutana na ubaguzi fulani lakini usijali.cha kuchunga zaidi ni hiyo figo yako.safari njema.
 
ahaa asante sana nashukuru. tax au wanatumia usafiri gani? wizi je?
Wanatumia taxi. Hata bajaji zipo.
Taxi ni nzuri zaidi na uwe unajua unapofikia. Hii ni muhimu. Ujanja wa kuongeza bei upo, lakini kama unajua unapofikia ni rahisi zaidi.
Inaweza kuwa Rupee 1,000 kama This.33,000/.
Safari zote nilizokwenda siku experience wizi.
Airport jitahidi kuwauliza na kupata maelekezo kwa askari. Wengi ni uniformed.
 
habari za humu ndani wana jamii forum. ninaomba msaada kwenu kwani kuna ndugu yangu ameniomba nimsindikize kwa ajili ya matibabu hospitali inayoitwa APPOLO NEW DELH India. nimemkubalia kumsindikiza ana matatizo ya figo, kuna mtu tunaenda nae atakaempa figo wameshakubaliana ila naenda tu kama msindikizaji. kiukweli ndo mara yangu ya kwanza kusafiri kwenda india, na pia kutoka nje ya nchi. ninaomba mnieleweshe natakiwa kuwa na vitu gani, na nifanye vitu gani sasa hivi mana safari ni next week, na nikiwa kule kazi yangu kubwa itakuwa ipi kwa ambao mshaenda asanteni

Pole kwa kuuguza na kujiandaa na hiyo safari,
1: Pesa ya India ilibadirishwa hivi karibuni hivyo kulikuwa na uhaba sana wa pesa za India, pia uwe makini sana wakati wa kufanya exchange rate, kuna uwezekano mkubwa wa kupewa pesa za kizamani ambazo hazitumiki, kama unaenda Kwenye Hospital kubwa kama hiyo basi unaweza kuwaomba wakufanyie change hapo Hospital, mwezi wa Nov change ilikuwa 1$= 63rupee, yaani $100 unapata 6300rupee

2: kuhusu tax ni gharama sana ukitumia tax za kawaida, tax cheap kabisa ni za UBER, hivyo kama unaweza download app ya Uber na ukifika Airport unaweza kutumia hiyo App kuita tax, kwa Tax za kawaida kutoka Airport Mpaka Maeneo ya Appolo ni Rupee700 lakini kwa Uber utalipa max ya 300rupee

3: gharama za malazi kama utatumia Hostel za hospital ni kubwa sana kuliko hata matibabu yenyewe, hapo karibu na Appolo kuna mji unaitwa Jasola, so kuna hotel ambazo zinakuwa na chumba kimoja Choo na jiko la gas, ni Rupee 1000 kwa siku au vyumba viwili vyoo viwili na jiko la gas kwa Rupee 1200, gas unajaza mwenyewe na kilo 1 ni 100 rupee hivyo kilo 4 size ya mitungi iliyopo inaweza kukutosha kwa wiki tatu au nne, chakula unanunua mwenyewe very cheap
Pia zingatia kuwa, kama matibabu yako sio ya dharura, basi usimpeleke mgonjwa kulazwa hospital, unaweza kukaa nae mtaani na siku ya operation ndio alazwe, yaani mtakuwa mnaenda kwenye vipomo na kurudi hotelini
Gharama za chumba, chakula kwa hospital ni kubwa sana

4: pia kuhusu dawa za kutumia baada ya kumaliza matibabu ya huko, msikubali kupewa za hospital ni gharama sana, wakikupa list ya dawa zinazotakiwa basi utaenda kwenye maduka ya wholeseller na utapata dawa kwa cheap sana na unaweza kununua dawa hata za miezi sita kwa bei nafuu kuliko za hospital

Kama kuna ziada plz niulize nikusaidie
 
Back
Top Bottom