Emekha Ikhe
Member
- Jul 14, 2021
- 52
- 84
SAFARI NDEFU YA KITAALUMA(LONG WALK TO ACADEMIC JUSTICE) NA NENO LA SHUKRANI KWA TAASISI, VYOMBO VYA HABARI NA WADAU MBALIMBALI 2011-2025.
Prof. Rwekaza Mkandala, Watawala Wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na Viongozi wote wa serikali Mlioshiriki kunifukuza Chuo Kikuu cha Taifa (UDSM) na kuniwekea vizuizi vingi katika safari yangu ya kitaaluma tangu mwaka 2012, Nichukue fursa hii kuwashukuru, na maana safari imekamilika kwa kupita mabonde na milima. Licha ya kwamba Kihistoria, Kufukuzwa kwangu kulinifanya nibadilishe taaluma, kutoka Shahada ya Uhasibu na kwenda Shahada ya Sheria, Lakini Mapito haya yote yamenisuka, Yameniimarisha na Yamenifunza kuwa imara Zaidi katika Kupigania haki za Binadamu.
Nimeshukuru kwa Kuwa, Maamuzi yenu yalichochea hatma ya mimi kubadili taaluma yangu ya Uhasibu na Kusomea Sheria badala ya kuendelea na Shahada yangu ya Uhasibu. MUNGU wa Nyakati ni Mwema sana, Amenishindia Vita tena ya Kitaaluma Mikononi Mwangu, Sifa na Utukufu virudi kwake.
Naomba aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mkandala na Wasaidizi Wake, Wakati wa Utawala wa Mstaafu Jakaya Kikwete, Walioshiriki Kunifukuza Chuo, Kunishtaki, kunifuta katika Mfumo wa Elimu na kuweka vizuizi mbalimbali, taarifa ziwafikie kwamba, wamesababisha hatma hii njema, MUNGU wa Nyakati ni Mwema, Kwa sasa amenipa utukufu Mwingine wa kuwa WAKILI wa Kutetea haki za binadamu.
Nimeamua kuandika hii Makala kama sehemu ya Ushuhuda na Kuwatia Moyo Vijana nchini Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika na Dunia kwa Ujumla Wake katika kupigania maono au ndoto wanazoziamini licha ya kupita katika giza na changamoto nzito kama ambavyo nimepitia, Binafsi, Nilibahatika kufukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam [UDSM] Mara mbili kwa nyakati tofauti, mwaka 2011 na mwaka 2017, Kwa sababu ya Kutetea Haki za Wanafunzi enzi nikiwa Mwanafunzi, Nakili kwamba ni bahati kufukuzwa kwa kuwa sikufukuzwa Chuo nikifanya uhalifu wowote, ila kwa Sababu ya Kutetea Haki za Wanafunzi Tanzania.
Mimi na wenzangu wa enzi hizo, tulitumia sana eneo maarufu liitwalo REVOLUTION SQUARE ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kuratibu na kuibua Mijadala mbalimbali inayogusa Haki za Wanafunzi na Maslahi ya Taifa, tulitumia eneo hili kufanya mijadala ya kitaifa juu ya Miswada mbalimbali ya Sheria, Kukemea Ufisadi, na kutafakari mambo mbalimbali yanayogusa Wanyonge nchini na kuyatolea tamko au kauli elekezi kama wasomi, Bahati Mbaya nimearifiwa kwamba eneo hili kwa sasa limefungwa na utamaduni wa Wanafunzi kukutana Kujadili mambo ya Nchi yao Umefungwa kama si kuzikwa kabisa.
Kwa Bahati Mbaya sana, Baada ya Watawala wa Vyuo Vikuu wakishirikiana na Serikali Pamoja na Vyombo Vya dola, Kufanikiwa kudhibiti fikra huru za Wanafunzi vyuo Vikuu, Vyuo Vya Kati na kuzika uhuru wa kitaaluma ndani ya Vyuo Vikuu, sasa Watawala wameamua kushughulika na kuzika Uhuru wa Kitaaluma (Academic Freedoms) ambao kwa sasa ni sehemu ya Haki za Binadamu kwa dunia ya sasa, Sasa kuna mashushushu kibao ambao wanapandikizwa Vyuoni kufuatilia mienendo ya Wahadhiri wanachofundisha kama hakiipendezi serikali wanakushughulikia. Kuna wahadhiri wameripotiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi, Chuo Kikuu Mzumbe na UDOM. Hii ni hatari katika taifa maana Uhuru wa Kitaaluma ni uhuru wa Taifa. Someni Kitabu Changu cha SAUTI YA WATETEZI WA HAKI VYUONI 1960’S-2017 kinapatikana softcopy kwa Mtandao wa GOOGLE, nimeeleza kwa kina.
Anyway, Kihistoria Nilifukuzwa kwa mara ya Kwanza, Mwaka 2011 Nikiwa Mwaka Wa tatu nikisomea Shahada ya Uhasibu (B.Com Accounting) kwa Sababu ya Kuongoza Mgomo na Maandamano ya Haki dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa Mstaafu, Jakaya Kikwete nikitetea Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza kutorudishwa nyumbani kwa sababu ya hoja ya Serikali kusema kwamba; Bajeti ya Mikopo haitoshi hivyo Wanafunzi wenye sifa ya kupewa mikopo, kukosa Mikopo na warudi nyumbani au Wajigharamie huku kukiwa na ufisadi Mkubwa ndani ya Serikali na Bodi ya Mikopo Yenyewe (HESLB) kwa mujibu wa Ripoti ya CAG
Tulishitakiwa Wanafunzi 51 lakini hatma yangu binsafsi; Nikafukuzwa, Nikafutwa Katika Mfumo wa Elimu, Sikuruhusiwa tena Kusoma Ndani ya Vyuo Vikuu Vya Umma Tanzania, Nikashitakiwa kwa jinai ya makosa Mawili (Criminal case No.270/ 2011); Kuongoza Maandamano yaliyokinyume na Sheria na Kukaidi amri ya Polisi iliyotutaka tutawanyike wakati wa Maandamno. Nikashinda kesi tar 30.08.2012 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini Sikurejeshwa Chuo huku baadhi ya Wenzangu walirejeshwa Chuo.
Mara baada ya Utawala wa Mstaafu Kikwete ambao ulitufukuza chuo kuisha, Nikamuandikia Barua Rais wa awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli yenye dhumuni la Kumuomba atengue Kifungo batili Walichokirasimisha watawala UDSM na Serikali ya wakati huo, Mhe, Rais Magufuli alielekeza Wasaidizi wake wa Sheria na Elimu IKULU kushughulikia hilo, ndipo Mwaka 2017 niliruhusiwa tena kusoma kwa mara ya pili, Chuo Kilekile [UDSM] Kwa Sharti ya kuanza Upya.
Niliamua Kuanza Kusoma shahada nyingine ya sheria, kwa sababu nilikuwa nimeonewa,hivyo nilitamani kutafuta nyenzo wezeshi ya kujitetea, Nimeshinda sana Katika korido za Mahakama kutafuta haki bila mafanikio na niliona kusoma Sheria ndio nyenzo wezeshi itayonisaidia mbeleni Kupigania haki zangu na kukutimiza Ndoto za kuwa WAKILI ili niwe na uwezo wa Kujitetea na Kutetea wengine, Vile vile niliamini kwamba, kuwa wakili, kutanifanya kuwa na weledi katika masuala yangu ya utetezi wa Haki za Binadamu.
Badlucky, Nikafukuzwa tena kwa mara ya pili, Nikiwa naendelea na ratiba za masomo chuoni ili kutimiza ndoto zangu za kuwa Mwanasheria na hatimaye baadaye kuwa Wakili, Ghafla Watawala UDSM walikatisha safari yangu Kikatili, Nikiwa katika ratiba ya kufanya Mitihani ya kumaliza mwaka wa Kwanza wa Shahada ya Sheria, Nikafukuzwa tena na Utawala wa UDSM (kwa Mara ya pili) Kwa kupewa barua ambayo ilitoa hoja kwamba; niliingia Chuoni na kudahiliwa kimakosa na kinyume na Sheria.
Nikafanya jitihada za kuwatafuta Wasaidizi wa Rais, Hayati John Pombe Magufuli waliopewa jukumu la kuhakikisha narudi Chuo, Nilipo wapigia wakaniambia kuna taarifa zangu mbaya zimepelekwa hivyo wanahitaji muda kuzichakata. Mpaka leo sijawahi fahamu ni taarifa gani zilizopelekwa ikulu ambazo zilitengua torati ya awali.
Baada ya hapo, MUNGU Mwema, Kuna padri wa Kanisa la Katoliki kwa huruma na jitihada zake alinitafuta, Nilisaidiwa na Padri husika [Jina Limehifadhiwa] Kwa Uharaka zaidi na kuunganishwa na Chuo binafsi (Private), TUMAINI University of Dar es Salaam ambako nilianza upya Shahada ya Sheria na Kumaliza shahada husika mwaka 2020. Wakati nasoma Chuo Kikuu cha Tumaini (TUDARCO) niliamua Kumshitaki Prof. Rwekaza Mkandala yeye kama yeye kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka ya Umakamu Mkuu wa Chuo na Pia Nikashitaki Taasisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa Kunifukuza chuo kinyume na Sheria. Kesi husika, haikuzaa Matunda
Baada ya safari ndefu ya Kitaaluma kama ambavyo Media ya The Chanzo, Gazeti la mwananchi na The Citizen zilivyoripoti katika Makala zake tofauti kwa Nyakati tofauti, kama ambavyo link zinavyojifafanua;
(Young Activist’s Twelve-Year Ordeal In Search Of Education - The Chanzo )
(Six years fruitless journey in search of education ).
Safari hii ndefu kitaaluma kwangu, ilinichukua takribani Miaka 12 kumaliza Shahada yangu ya Kwanza, Mpaka pale Chuo Kikuu cha Tumaini (TUDARCO) kuliponitunuku Shahada ya Sheria. Nilijiunga na Shule Ya Sheria [Law School of TANZANIA] 2021 na imenichukua miaka 4 kumaliza, Rasmi nimetunukiwa Uwakili wa Mahakama Kuu na Mahakama za Chini Yake. Huu sio Ushindi wangu bali MUNGU kanishindia vita hii ya Kitaaluma Mikononi Mwangu.
SHUKRANI KWA TAASISI MBALI MBALI ZILIZONISHIKA MKONO WAKATI WA SAFARI YANGU NDEU YA KITAALUMA
Licha ya ukweli kwamba Ninamshukuru MUNGU, ninawashukuru Wazazi Wangu, ndugu na jamaa wengi ambao wameshiriki kunishika mikono katika safari yangu ndefu ya Kitaaluma, pia Napende kushukuru taasisi zifuatazo;
MTANDAO WA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU (THRDC), KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) NA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)
Tangu nimefukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mashirika haya yasiyo ya kiserikali (NGOs) ya Kutetea Haki za Binadamu Mathalani, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) chini ya Uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji, Wakili, Onesmo Olenguruma, Legal Human Rights Center (LHRC) chini ya Uingozi wa Dr.Helen Kijobisimba, na Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS), Yalijitokeza katika Kutetea Haki yangu ya Kupata elimu Mahakamani.
LHRC Walinipa Wakili, Regnald Martin na Laetitia Petro Ntagazwa ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), THRDC walinipa wakili aliyeitwa Jones Sendodo, na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kilitoa Mawakili wawili, Wakili Mabere Nyaucho Marando na Wakili Mnyere.
Mawakili hawa wote kupitia taasisi zao, Wameshiriki katika Kuhakikisha Napata haki yangu ya elimu kwa njia ya Mahakama. Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilienda mbali Zaidi, kiliamua kuniajiri kama Mwangalizi Msaidizi wa Haki za Binadamu (Assistance Human Rights Monitor) ili niendelee kujifunza masuala ya Haki za Binadamu.
CHUO KIKUU CHA TUMAINI, DAR ES SALAAM (TUDARCO)
Katika Historia yangu ya machozi ya kutafuta Haki yangu ya Kitaaluma, Chuo Hiki kama Taasisi, kilinifuta machozi, Nakumbuka, baada ya Kufukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mara ya pili, Mwaka 2017, na baada ya Juhudi za Padri wa Kanisa la Katoliki (Jina Limehifadhiwa), nilifanikiwa Kudahiliwa chuo Kikuu cha Kanisa kiitwacho Tumaini University of Dar es Salaam (TUDARCO).
Kipekee, Nipende vile vile Kushukuru Waalimu wangu wote ambao walinifanikisha kumaliza Shahada yangu ya Kwanza ya Sheria TUDARCO, Asilimia Kubwa ya Waalimu walionifundisha tangu Mwaka wa Kwanza Mpaka wa Mwisho, Walijua mapito niliyopitia katika safari yangu ya Kitaaluma, Mwalimu Jangu na Mwalimu Kaunda, ni Miongoni mwa Walimu ambao walipenda kuona natimiza ndoto yangu ya kitaaluma baada ya Maswahibu niliyopitia. Kwa upendo wa Waalimu na kwa namna Chuo hiki kinavyolea Wanafunzi wake, Nilifanikiwa kupata shahada ya Sheria(LLB).
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM(UDSM) NA PROFESA RWEKAZA MKANDALA
Pamoja na ukweli kwamba, Chuo hiki kilinifukuza na Kunifuta katika Mfumo wa Elimu na kuniwekea Vikwazo mbalimbali kama ambavyo Tamko la Utawala wa UDSM lilivyohimiza kupitia link ifuatayo;
(Wanafunzi 43 wafukuzwa UDSM )
Siwezi kupuuza Mchango wa taasisi hii kwangu, Ni taasisi iliyonilea tangu mwaka wa kwanza mpaka pale nilipofukuzwa chuo, Mimi ni Zao la Chuo Kikuu cha Dar es Slaam katika Muktadha wa Kutetea Haki za Binadmu, Chemic hemi ya utetezi ilipandwa na kumea ndani yah ii taasisi. Bila taasisi hii huenda nisingezaliwa upya katika ulimwengu wa utetezi wa Haki za Binadamu.
Maamuzi ya kufukuzwa Chuo ni maamuzi mabaya machoni lakini baadae nimekuja kufahamu thawabu ya Mapito(Upande wa Pili wa Mapito) kwamba, bila haya mapito huenda nisingekuwa na hatma ya kuwa WAKILI (FATE WAS CALLING). Pia nimejengwa na kusukwa Misuli ya Imani katika Mapambano ya Kuetetea Utu na Haki za Bindamu kitaifa na Kimataifa.
Nakumbuka, Kitendo hiki cha kufukuzwa na kufutwa katika mfumo wa elimu ya umma kilinifanya niandike Waraka maalumu uliobeba hisia kali (Emotional Article) dhidi ya Prof.Rwekaza Mkandala na Watawala kama link inavyojieleza; WARAKA WA ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE KWAKO PROF. RWEKAZA MKANDALA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
(Waraka: Alphonce Lusako alias Emekha Ikhe kwako prof. Rwekaza Mkandala )
Sasa ni Ukurasa Mpya ambao nazika mambo yote ya Kale na Kuitazama kesho kishujaa, Nimesamehe yote niliyotendewa na watawala kwa miaka yote hii na nasemehe kwa ajili yangu pia, na kama kuna mahala niliwakosea katika harakati za kutimiza nia yangu njema ya Utetezi wa Haki za Watu, naomba vile vile nisameheke pia. (ITS NEW CHAPTER)
SEKA AND ASSOCIATE ADVOCATES
Hii ni Miongoni mwa Lawfirm ambayo inaongozwa na Wakili John Seka, Wakili John Seka kupitia hii Lawfirm, ilinisadia Kushikati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama taasisi na Prof. Rwekaza Mkandala kama yeye kwa matumizi mabaya ya Madaraka akiwa Makamu Mkuu wa UDSM. Link hapo chini inataarifa zaidi
(Court: Mukandala to stand trial for alleged unfair dismissal of a student )
VYOMBO VYA HABARI
Vyombo vya Habari vilifanya kazi kubwa ya kutafuta ukweli wa Sakata langu la kufukuzwa chuo na kupaza sauti, Vyombo Vya Habari vyote vilivyohusika vilifanya uonezi husika kufahamika hivyo sauti zao kuzifikia taasisi na wadau mbalimbali. Taasisi husika na wadau mbalimbali walijitokeza kunipa msaada wa namna moja au nyingine.
Gazeti la Mwananchi, Gazeti la The Citizen, Mwanahalisi, Media za The Chanzo na vyombo mbalimbali vya Habari vilitoa mchango Mkubwa katika safari yangu ndefu ya kitaaluma. Kuna waandishi wawili naomba niwataje kuwawakilisha wengine; KHALIFA SAID wa The Chanzo na JAMES MAGAI wa Gazeti la Mwananchi, Niwapongeze kipekee kwani tangu nafukuzwa UDSM, kwa nyakati tofauti waliandika Makala maalumu kuhusu tukio langu.
HITIMISHO
Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Nimeacha nyenzo wezeshi, Niliandika Kitabu kwa ajili yenu; SAUTI YA WATETEZI WA HAKI VYUONI 1960-2017, kilichohifadhi Mapambano ya Haki ndani ya Vyuo Vikuu na kuhusiha harakati za kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kitauluma na fikra huru za Wanafunzi Vyuoni kwa maslahi mapana ya Taifa. Someni, Kinapatikana bure ili mchote maarifa kupitia link;
(
View: https://www.scribd.com/document/354098670/Hali-Ya-Watetezi-Wa-Haki-Za-Binadamu-1. Kitabu hiki kinarejewa Upya na Toleo lake la Pili litatoka siku za usoni.
Historia yangu iwatie moyo Wapiganaji wote wenye ndoto kubwa wanaopitia Vikwazo katika kupigania ndoto na maono yao, Unaweza Kuzuiliwa na Mamlaka kwa namna yoyote inayotisha lakini Wakati wa MUNGU ukifika hakuna Mamlaka ya Kuzuia. Kuna nyakati za giza nene ambazo huenda ukadhani ndio mwisho wa Maono au ndoto zako, Usije ukakata tamaa maana, kukata tamaa ndio kifo cha ndoto na maono yako. Usikubali kushusha utu, Ubinadamu wako na misimamo yako ya haki eti kwa sababu ya Waovu, Wenye nguvu kutaka wakudogodeshe watakavyo.
Nimejifunza katika dunia hii, Watu wengi wanaofukuzwa au kuzuiliwa katika taasisi mbalimbali huwa ni hazina kwa Taifa, Ni watu Wema ambao wana kitu ndani yao kutimiza kusudi Fulani la MUNGU kwa watu wake. Sifa za watu waliochaguliwa na MUNGU (ChosenPeople), Njia zao sio nyepesi sana kwa kuwa hupigwa vita katika Ulimwengu wa Kiroho na kimwili. MUNGU hulinda watu wa aina hii kwa wivu mkubwa. Namshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kunishindia vita hii mikononi mwangu.
ALPHONCE LUSAKO
(WAKILI)