Safari fupi ya kuzimu. Sijutii maisha yangu

Sehemu ya kwanza
Habari za wakati huu,

Niite Mark ni mtu mzima nilikuwa na mke na watoto 6. Nimzaliwa wa mkoani Kilimanjaro, moshi mjini Njoro. Elimu yangu ilikuwa ya kulenga kwa manati kutokana na nyumbani hali haikuwa nzuri sana kifedha.

Na hii ni stori yangu fuatana nami hadi mwisho utajifunza mengi.

Nyumbani kwetu tupo 10 wakiume 7 na wakike 3 wote hamna ambaye ananafuu kimaisha hali ni dhofu sana. Baada ya mzee kufariki na mama naye kufuatia, sisi kama ndugu tuliamua kuuza nyumba ya urithi ili kila mtu afe na chake mapema.

Ndipo nilipoamua kujiingiza kwenye biashara ya maparachichi, ambayo nilikuwa naenda vijijini moshi kukusanya mzigo na kuleta sokoni. Biashara sikuwahi kufanya mwanzo ndio mara ya kwanza.

Kiujumla biashara ilianza kuwa nzuri namimi nikaona hii sasa ndio yenyewe nilikuwa wapi sikuzote hizi? Soko likakuwa mpaka siku moja majira ya jioni nikiwa mitaa ya boma mbuzi pasua, nikiwa na mtaji wa kutosha nimetulia walipokuja wazee wa kazi nakunisafisha pesa zote nilizokuwa nazo.

Mvua inanyesha na kaubaridi na hela ya nyumba ya urithi ikawa imeenda hivyo. Sikuwa na lakufanya ila roho iliniuma sana kwasababu nilitakiwa nianze tena moja upya!

Nikajiingiza kwenye kazi za ufundi kwasababu nilikuwa nazijua, hizi za ujenzi na mzee pia alikuwa fundi. Kazi zikawa nazipata kwa kulenga kwa manati ila mafundi wengine naona wao wanapata( wanapeana kazi kwa kujuana).

Kila mja na riziki yake, nikapata kazi ya kujenga nyumba ya room 3, kuipiga plasta pamoja na kupaua. Nikaona hapa ndio penyewe nikaamua kugawa namimi riziki kwa mafundi wengine ili siku nao wakipata wanikumbuke.

Ile kazi ilikuwa nzuri na ilikuwa na hela kwa kweli, kazi ilianza na ilikuwa inaenda vizuri mpaka siku moja baada ya kula msosi wa mchana, kila nikinyanyua tofali nahisi kichomi nikilitua nakuwa freshi.

Nikasema acha niende geto niue siku ya leo. Njiani nikiwa naelekea magetoni niliteleza nikaanguka nikaumia mgongo. Ikabidi ile kazi nimuachie fundi mwingine kwa mapatano.

Baada ya wiki kuisha nikasema nirudi saiti namkuta tajiri kafura kwa hasira kazi chafu ukuta umepinda! Shughuli yangu ikaishia hapo akapewa mkataba fundi mwingine mmoja wa wale niliowaita. Maisha lazima yaendelee.
Nikapata kazi maeneo ya uhuru hostel kupiga plasta.

Tajiri kuleta material sio shida ila kukupa hela yako wewe kama fundi ndio utata unapoanzia. Mara atasema plasta mbona haijanyooka, mara ratio nyepesi sana, sijui umeniibia cement. Ilimradi tu asikupe hela.

Nlipoamua kumkomalia zaidi anipe pesa zangu, akanipa nusu nyingine akasema atanimalizia saiti inasimama kwanza, kumbe saiti haijasimama bali katafuta fundi mwingine namimi ndio kanichinjia baharini. Na hiyo nusu iliobaki hakuwahi kunilipa tena.

Haya maisha haya....... Usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Kumbe ni wewe ulitudhulumu zile mashine zetu keeling mangi sio mtu wa kumwamini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom