Safari channel imeanza kuharibu mambo

Safari channel imeanza kuharibu mambo

nina star times ila hii channel sijawahi ipata hivi ni namba ngapi wadau nami nikaitafute
 
Kuna siku nakumbuka nilishuhudia wakirusha mkutano wa ccm...sikumbuki ilikua wapi....
 
Channel mpya ya Safari Channel ilipoanza ilionekana kama chaneli tishio kwa sababu watu wengi sana wanapenda kuangalia wanyama na matukio ya utamaduni wetu.Watu wengi awali walikuwa waking alia chaneli za wanyama za nje lakini baada ya kufunguliwa hii chaneli ya kwetu watu walihamia nyumbani.Baada ya muda mfupi tayari waandaji wa vipindi vya chaneli hii wameanza kuharibu kwa kasi ya ajabu na tayari watu wameanza kurudi kwenye chaneli zao za nje.Vipindi vingi vya Safari Chaneli vinarudiwa rudiwa mno hadi inakuwa chukuzi.Kuna makabila mengi Tanzania ambayo yote yana utamaduni wao lakini nafasi hayapewi.Mikanda ya wanyama iko mingi na mizuri mno lakini yote haioneshwi kamwe.Waandaji wanashindwa hata kumuenzi mzungu alietengeneza mkanda mashuhuri wa wanyama uliojulikana kwa jina la SERENGETI SHALL NEVER DIE.Huyu mzungu simkumbuki jina lakini katika harakati zake za kupiga picha za wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa kutumia helicopter yake binafsi alipata ajali baada ya ndege kugongwa na mapopo na kuanguka na yeye alifarika dunia.Baada ya ndugu zake kufika toka Ulaya waliamua azikwe Tanzania na kujengewa mnara wa kumbukumbu pale pale alipoangukia na ndege yake.Mtoto wake mkubwa katika kutoa neno kwa serikali ya Tanzania alitamka neno la ajabu na la kishujaa mno.Nanukuu alivyosema mtoto huyo, " Baba amekufa lakini Serengeti haitakufa.Alichukua mikoba ya baba yake na kumalizia kazi ya kupiga picha wanyama.Filamu yake aliita SERENGETI SHALL NOT DIE!!.Ni picha iliovutia mno watazamaji kipindi kile.Waandaji wa vipindi vya Safari Chaneli sidhani hata kama wanafahamu kumbukumbu hii muhimu na si ajabu hata nakala ya ya picha hawana.Ni aibu kufuta kumbukumbu ya jinsi hii.Nawasihi itafuteni ili vijana wa sasa waweze kujifunza kutoka kwenye mkanda huo wa kusisimua.Kwa sasa watu wamechoka mno na na mavipindi ya kurudia yale yale kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
unazungumzia TBC? ha ha ah, hawa wameweke li kmpyuta linajiendesha lenyewe, si channel inayoendeshwa na mtu, hata wewe unaeza enda youtube uka download .

Ryoba kaiua TBC na ni suala la mda tu, hataki JPM afanye ziara pale, siku JPM akijua kwamba DG huwa anamdanhganya mambo mengi na akijua TBC haitazamwi, wafanyakazi hawana vifaa, ma engineer wao hawasafiri, DG kaokota ndugu zake na kuwajaza pale, amekwenda mbali aidi sasa hata safari za kikazi badala wasafiri watu 5 anasafiri mmoja ndio maan KILA HOTUBA YA JPM RYOBA KWA maksudi hukata matangazo live, kuna watu wanasema huyu jamaa ni team membe, ataliwa kichwa.
 
Hivi hawa TBC hua wanapata hata wasaa kupitia mitandao ya kijamii ili waone wadau wanasema nini kuhusu huduma zao na pengine hata kuwajibu tu maoni yao kuwa ni mazuri na pengine watayafanyia kazi au vipi.Wamekaa kimya kama wamekufa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama serikali imeanzisha kitu alafu inashindwa kukiendesha si wabinafsishe tu hiyo channel apewe azam muone balaa lake watalii watadouble hapa tz ndani ya miaka mitatu tu.
Mambo mengine tutumie akili tu tbc safari ingieni mkataba na azam mbona zbc kule wameweza wamewapa azam zbc 2 na mambo yanaenda safi sahivi watanzania matukio muhimu mengi wanaangalia kupitia zbc 2..
Tunaweza kuanzisha project ila hatuwezi kuziendeleza.
 
wanachosha sana hao watu. wanategemea ruzuku kujiendesha hawana akili ya kujiongeza. Hawatafuti hata matangazo ya mahoteli? wanajua utalii ni Mbuga tu.
 
😀😀😀😀 siku wanazindua hii Chanel nilisema chonde chonde TBC msifanye upuuzi kama uliopo TBC1, upuuzi wakurudia rudia vipindi, ujinga sasa hiyo safari chanell ndio huo ukifungua utakuta mtwa mkwawa na familia yake kesho tena upuuzi huo huo kesho tena

Miye nashauri wapige nyimbo za bongo fleva tu Chanel imewashinda
 
Tatizo bajetii. Ishu za utalii zinahitaji hela ya kutosha ili uweze kusafiri kila mahali na kufanya coverage nyingi. Sasa hii ya kutegemea OC ndio upange safari, dah.. utarudia rudia mavipindi yaleyale asbh mpaka jioni..
Not true... Kama huna bajeti tafuta organizations zinazojihusisha na conservations watajitolea tuu kuandaa hizo documentaries.... Mfano Jane Gudall kule Kigoma Gombe na wengine hawawezi kushindwa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TBC si wabunifu ni kundi la wanasiasa watarajiwa, TBC ilikuwa na maktaba ya filamu iliyorithi Audio Visual Institute , picha hizo ingeweza kuzibadili ziweze kuoneshwa kwenye TV.
TBC wanapenda sana mambo ya siasa has a kuongozana na viongozi wa CCM, kwao ni fahari.
Ninawashauri waende mikoa ya Kusini na nyanda za huu Kusini, magharibi, Kagera na ya kati ambako kuna vitu vingi sana ambavyo hatuoneshwi zaidi ya wanyama!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ukweli kila niki tune hiyo channel hua inascratch, la sivyo na mie ningekua na povu la kutosha leo..
 
Not true... Kama huna bajeti tafuta organizations zinazojihusisha na conservations watajitolea tuu kuandaa hizo documentaries.... Mfano Jane Gudall kule Kigoma Gombe na wengine hawawezi kushindwa.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa mbona unajipinga mwenyewe, unasema “Not true” halafu unaendelea kusema kama huna bajeti. Au hukuelewa mantiki yangu kuhusu bajeti?
 
Sasa kama serikali imeanzisha kitu alafu inashindwa kukiendesha si wabinafsishe tu hiyo channel apewe azam muone balaa lake watalii watadouble hapa tz ndani ya miaka mitatu tu.

Mambo mengine tutumie akili tu tbc safari ingieni mkataba na azam mbona zbc kule wameweza wamewapa azam zbc 2 na mambo yanaenda safi sahivi watanzania matukio muhimu mengi wanaangalia kupitia zbc 2..
✓Na wakija wataliii waarabu itasema magaidi wanakuja. Mtu mweusi tupo kwy fungu la kukosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom