Safari channel imeanza kuharibu mambo

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
653
Channel mpya ya Safari Channel ilipoanza ilionekana kama chaneli tishio kwa sababu watu wengi sana wanapenda kuangalia wanyama na matukio ya utamaduni wetu.

Watu wengi awali walikuwa waking alia chaneli za wanyama za nje lakini baada ya kufunguliwa hii chaneli ya kwetu watu walihamia nyumbani.

Baada ya muda mfupi tayari waandaji wa vipindi vya chaneli hii wameanza kuharibu kwa kasi ya ajabu na tayari watu wameanza kurudi kwenye chaneli zao za nje.Vipindi vingi vya Safari Chaneli vinarudiwa rudiwa mno hadi inakuwa chukuzi.

Kuna makabila mengi Tanzania ambayo yote yana utamaduni wao lakini nafasi hayapewi.

Mikanda ya wanyama iko mingi na mizuri mno lakini yote haioneshwi kamwe.Waandaji wanashindwa hata kumuenzi mzungu alietengeneza mkanda mashuhuri wa wanyama uliojulikana kwa jina la SERENGETI SHALL NEVER DIE.

Huyu mzungu simkumbuki jina lakini katika harakati zake za kupiga picha za wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa kutumia helicopter yake binafsi alipata ajali baada ya ndege kugongwa na mapopo na kuanguka na yeye alifarika dunia.

Baada ya ndugu zake kufika toka Ulaya waliamua azikwe Tanzania na kujengewa mnara wa kumbukumbu pale pale alipoangukia na ndege yake.

Mtoto wake mkubwa katika kutoa neno kwa serikali ya Tanzania alitamka neno la ajabu na la kishujaa mno.

Nanukuu alivyosema mtoto huyo, " Baba amekufa lakini Serengeti haitakufa.Alichukua mikoba ya baba yake na kumalizia kazi ya kupiga picha wanyama.

Filamu yake aliita SERENGETI SHALL NOT DIE!!.Ni picha iliovutia mno watazamaji kipindi kile.Waandaji wa vipindi vya Safari Chaneli sidhani hata kama wanafahamu kumbukumbu hii muhimu na si ajabu hata nakala ya ya picha hawana.Ni aibu kufuta kumbukumbu ya jinsi hii.

Nawasihi itafuteni ili vijana wa sasa waweze kujifunza kutoka kwenye mkanda huo wa kusisimua.

Kwa sasa watu wamechoka mno na na mavipindi ya kurudia yale yale kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila siku wanarudia mahojiano na wahifadhi wale wale sijui shida Ni Nini ila watanzania Kuna tatizo sehemu sio bure maana haiwezekani kila kitu tunachokifanya kinakua hakina mvuto na unaweza shangaa mkuu wa Nchi siku akitembelea hapo na kuhoji kwa Nini wanarudia vipindi na Hali mikanda ya video ipo mingi au Mambo mengi ya kupromoti boss wa channel hiyo atatoa macho Kama kajamba ukweni akiwa Hana majibu safari channel mjirekebishe kiukweli mnaboa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila siku wanarudia mahojiano na wahifadhi wale wale sijui shida Ni Nini ila watanzania Kuna tatizo sehemu sio bure maana haiwezekani kila kitu tunachokifanya kinakua hakina mvuto na unaweza shangaa mkuu wa Nchi siku akitembelea hapo na kuhoji kwa Nini wanarudia vipindi na Hali mikanda ya video ipo mingi au Mambo mengi ya kupromoti boss wa channel hiyo atatoa macho Kama kajamba ukweni akiwa Hana majibu safari channel mjirekebishe kiukweli mnaboa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuuu. Sema tatizo lililopo ni bajeti tuuuuuuu. Videos nyingi zina Copy Right uwezi kurusha documentary ya mtu bila makubaliano na ni pesa kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuuu. Sema tatizo lililopo ni bajeti tuuuuuuu. Videos nyingi zina Copy Right uwezi kurusha documentary ya mtu bila makubaliano na ni pesa kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama serikali imeanzisha kitu alafu inashindwa kukiendesha si wabinafsishe tu hiyo channel apewe azam muone balaa lake watalii watadouble hapa tz ndani ya miaka mitatu tu.

Mambo mengine tutumie akili tu tbc safari ingieni mkataba na azam mbona zbc kule wameweza wamewapa azam zbc 2 na mambo yanaenda safi sahivi watanzania matukio muhimu mengi wanaangalia kupitia zbc 2..
 
Wanarudia vipindi vile vile wanavyovitoa Kwenye channel za nje hasa NAT Geo wild...!! Akati channel za nje zinaonyesha mbuga karibu **** za tanzania... Story za manyani...Kesho sijui katavi...Mara ngorongoro...!! jamaa wamekosa ubunifuu wanadhani vivutio ni Mbuga za wanyama tu na story ya mkawaa pekeee...Wanaboa balaaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TBC si wabunifu ni kundi la wanasiasa watarajiwa, TBC ilikuwa na maktaba ya filamu iliyorithi Audio Visual Institute , picha hizo ingeweza kuzibadili ziweze kuoneshwa kwenye TV.
TBC wanapenda sana mambo ya siasa has a kuongozana na viongozi wa CCM, kwao ni fahari.
Ninawashauri waende mikoa ya Kusini na nyanda za huu Kusini, magharibi, Kagera na ya kati ambako kuna vitu vingi sana ambavyo hatuoneshwi zaidi ya wanyama!
 
TBC si wabunifu ni kundi la wanasiasa watarajiwa, TBC ilikuwa na maktaba ya filamu iliyorithi Audio Visual Institute , picha hizo ingeweza kuzibadili ziweze kuoneshwa kwenye TV.
TBC wanapenda sana mambo ya siasa has a kuongozana na viongozi wa CCM, kwao ni fahari.
Ninawashauri waende mikoa ya Kusini na nyanda za huu Kusini, magharibi, Kagera na ya kati ambako kuna vitu vingi sana ambavyo hatuoneshwi zaidi ya wanyama!
Kumbe wengi mmeliona hilo, yaani kuna mikoa 26 sijui , makabila chungu nzima, vivutio kibao lakini kila siku utaon immagration ya nyumbu . ikibadilika sana tunaenda Kalenga kwa Chifu Mkwawa, mpak ina bore, badilikeni.
 
Sidhani kama wataelewa. wao wanadhani kila kitu ni siasa. Hayo mambo ya chama chao hawarudiii ila ya wanyama ,wanarudia hadi niliishaacha kuangalia hiyo chanel.
Kuna kipindi ulikuwa ukiweka hiyo channel unakutana na hifadhi ya rubondo wanarudia kitu kilekile cha jana
Nawashauri waingie makubaliano wawe wanaungana na chanel za nje angalau wapate vitu vipya
 
Channel mpya ya Safari Channel ilipoanza ilionekana kama chaneli tishio kwa sababu watu wengi sana wanapenda kuangalia wanyama na matukio ya utamaduni wetu.Watu wengi awali walikuwa waking alia chaneli za wanyama za nje lakini baada ya kufunguliwa hii chaneli ya kwetu watu walihamia nyumbani.Baada ya muda mfupi tayari waandaji wa vipindi vya chaneli hii wameanza kuharibu kwa kasi ya ajabu na tayari watu wameanza kurudi kwenye chaneli zao za nje.Vipindi vingi vya Safari Chaneli vinarudiwa rudiwa mno hadi inakuwa chukuzi.Kuna makabila mengi Tanzania ambayo yote yana utamaduni wao lakini nafasi hayapewi.Mikanda ya wanyama iko mingi na mizuri mno lakini yote haioneshwi kamwe.Waandaji wanashindwa hata kumuenzi mzungu alietengeneza mkanda mashuhuri wa wanyama uliojulikana kwa jina la SERENGETI SHALL NEVER DIE.Huyu mzungu simkumbuki jina lakini katika harakati zake za kupiga picha za wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa kutumia helicopter yake binafsi alipata ajali baada ya ndege kugongwa na mapopo na kuanguka na yeye alifarika dunia.Baada ya ndugu zake kufika toka Ulaya waliamua azikwe Tanzania na kujengewa mnara wa kumbukumbu pale pale alipoangukia na ndege yake.Mtoto wake mkubwa katika kutoa neno kwa serikali ya Tanzania alitamka neno la ajabu na la kishujaa mno.Nanukuu alivyosema mtoto huyo, " Baba amekufa lakini Serengeti haitakufa.Alichukua mikoba ya baba yake na kumalizia kazi ya kupiga picha wanyama.Filamu yake aliita SERENGETI SHALL NOT DIE!!.Ni picha iliovutia mno watazamaji kipindi kile.Waandaji wa vipindi vya Safari Chaneli sidhani hata kama wanafahamu kumbukumbu hii muhimu na si ajabu hata nakala ya ya picha hawana.Ni aibu kufuta kumbukumbu ya jinsi hii.Nawasihi itafuteni ili vijana wa sasa waweze kujifunza kutoka kwenye mkanda huo wa kusisimua.Kwa sasa time choke mno na na mavipindi ya kurudia yale yale kila siku.
Code:

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiachana na swala la baneti, pia uweledi ni tatiza kubwa sana sina uhakika kama watu wa tbc safari wanaweza kuandaa documentaries za kuvutia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom