Sadifa: Sijawahi kuwa kichaa

Sadifa: Sijawahi kuwa kichaa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

APR162013




MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Khamis Sadifa Juma, amesema kuwa hajawahi kuugua ugonjwa wa akili (kichaa) kama anavyozushiwa na wapinzani wake.


Alisema kuna watu wameandaliwa na mafisadi ili wamchafue, ikiwezekana aachie ngazi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Yusuf Hamad Masauni.


Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu mwishoni mwa wiki, Sadifa alisema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya vurugu hizo kwa ajili ya kutaka kujipatia umaarufu kupitia mgogoro huo na kuwafurahisha wale wanaowafadhili kifedha.


Alisema miongoni mwa uchafu aliowahi kutupiwa na watu hao ni kuwa alighushi umri ili aweze kugombea nafasi hiyo.


"Najua nimewekwa kwenye kundi la Edward Lowassa na huyo wamemtaja tangu nagombea, ndiyo maana wananipiga vita kutoka mwanzo.


"Wamegonga ukuta, hao wanatapatapa tu ndugu yangu, hao si wanasiasa ni wana si hasa, watatulia wenyewe, mimi sina muda wa kujibizana na mtu magazetini," alisema.


Akizungumzia tuhuma hizo, Sadifa, alisema kuwa yeye alizaliwa mwaka 1982 na hivi karibuni ametimiza miaka 31, kwamba ambaye haamini anaweza kujiridhisha kwa kuingia kweye mtandao ataziona taarifa zake zote.


Kuhusu ugonjwa wa kichaa, alisema hizo ni taarifa za kitabibu, hivyo ni vema kwa wale wote wanaodai hivyo kuonesha ushahidi wa vyeti vya madaktari ambavyo vinathibitisha madai yao.


"Mimi ni mbunge sasa kama kuna mtu ananituhumu hivyo basi waende mahakamani kama alivyofanya Raila Odinga kwenda kupinga ushindi wa Uhuru na hatimaye haki ikapatikana," alisema.


Naye mmoja wa vijana wanaotuhumiwa kutaka kumwondoa madarakani mwenyekiti huyo alisema: "Wakati umefika Sadifa ni lazima aondoke."


Alisema ataondoka si kwa kuwa wana timu au mkakati uliosukwa wa kumwondoa bali suala la msingi hapo ni kanuni.


"Mimi ni mjumbe wa UVCCM najua kanuni zetu. Sadifa ataondoka si kwa kuwa hatumtaki, hatuutaki uwezo wake mdogo na kanuni alizovunja," alisema.


Alisema kuwa Sadifa ni mbunge tangu 2010 lakini akahoji ni wapi aliwahi kusikika akizungumzia hoja ya vijana kama vile ajira hata baada ya kuchaguliwa UVCCM?


"Wapi Sadifa amefanya mkutano na kuvutia vijana wajiunge na CCM? Huwezi kumlinganisha hata na John Heche, Mwenyekiti wa BAVICHA wa CHADEMA. Unategemea atasaidia chama, huyu ana uwezo mdogo," alisema kijana huyo.



CHANZO TANZANIA DAIMA
 
LOL... UVCCM hawapendi Wenyeviti toka Zanzibar?
 
Hata kina Stela Mwapamba na Jul Funza walivyokuwa vichaa tuliwatimua wakawa join wenzao
 
Wanaotuhumu na wanaotuhumiwa wote machizi,ndio maana wanakubali kutumiwa na mafisadi,kijana mwenye akili timamu hawezi kuwa ngazi ya mafisadi.
 
ngoja vijana wanaojirahisisha kwa njaa za buku 7 7 waje,

CC. LUMUMBA TEAM@7000/post
 
Kama sikosei hapo Chizi Mwenzake Riz1 ndio wanatupiana mawe.
 
CCM kwa majungu hamjambo, sasa huyo Sadifa anatakiwa kuthibitisha kama hajawahi kupungukiwa akili!
 
Kwani kuna kijana wa ccm ambaye si kichaa? Sadifa ndo mwenyekiti wa Umoja wa Vichaa CCM.
 
Watajibu kwani kichaa anajitambua?Hivi kwani kuna kijana yeyote mwenye akili timamu bado yupo CCM?Huko kutuhumiana hakunishangazi maanake ili uwe UVCCM mojawapo wa sifa kuu kuliko zote ni lazima uwe chizi.

Ben Kuwa makini na matamshi yako, acha propagannda. Mimi naamini kijana kutoka cdm kama wewe anatakiwa atowe mawazo ya kujenga ili watanzania wapte fursa ya kutambua mabaya ya watawala wao na waelekee kwenye UKOMBOZi but kama utaanza Prpopaganda utakuwa ni mwanzo wa kutoaminika kama kijana ktk Taifa
 
Watajibu kwani kichaa anajitambua?Hivi kwani kuna kijana yeyote mwenye akili timamu bado yupo CCM?Huko kutuhumiana hakunishangazi maanake ili uwe UVCCM mojawapo wa sifa kuu kuliko zote ni lazima uwe chizi.

Lakini gwanda lake la kijani limemtoa sana.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ben Kuwa makini na matamshi yako, acha propagannda. Mimi naamini kijana kutoka cdm kama wewe anatakiwa atowe mawazo ya kujenga ili watanzania wapte fursa ya kutambua mabaya ya watawala wao na waelekee kwenye UKOMBOZi but kama utaanza Prpopaganda utakuwa ni mwanzo wa kutoaminika kama kijana ktk Taifa

Asiaminike kwa kueleza ukweli?au wewe huoni ukichaa wa wao?kuwa wanashindana kwa maslahi yao kwa ajili ya mafisadi na si taifa!!!? Please open your eyes
 
Hivi wewe KAVYINABHUHIYE wanachama wenyewe wamekiri kwamba mwenyekiti wao ni kichaa, na kwa jinsi nchi inavyotafunwa ni mtu ambaye ni kichaa pake yake anayeweza kushabikia ccm kwa sasa. kama unaona maada ya saanane haiko sahihi basi na wewe ni kichaa pia.
 
CCm nao siku hizi wameacha kushona mashati kawaida nao wamehamia kwenye gwanda!!! Kweli chadema wanaongoza nchi indirect kwani kila kitu ccm wanaiga toka chadema. Angalia picha ya Sadifa hapo juu.
 
Back
Top Bottom