SADC Hashim Mbita project: Southern African Liberation Struggles

SADC Hashim Mbita project: Southern African Liberation Struggles

Wakati wa awamu ya nne mambo ya udini yamepamba moto, ilikuwa ni faraja sana kumsikiliza Hashimu Mbita akiongea kwa uzalendo wa hali ya juu pamoja na uzee wake. Ni mtu ambaye ukimuangalia na kumsikiliza unatambua ndani na nje ya mwili wake ni mwafrika na mtanzania.

Sasa kuna watu wanataka kumtambulisha kwa label wanazounda wao wenyewe. Tuwakatae maana Mbita alikuwa:
  1. Mzalendo
  2. Mtanzania
  3. Mwafrika.
  4. ..rudia 1-3
Mtu akitaka kumvika vazi tofauti na hilo tumkatae na tumpe heshima mzalendo huyu.
 
SADC HASHIM MBITA PROJECT: SOUTHERN AFRICAN LIBERATION STRUGGLES
Br. Gr Hashim Mbita: Hero of the Liberation Struggle in Africa
​
Copy-of-Hayati-Hashim-Mbita.jpg

Author: Phyllis Johnson
 
Huku Mwanza kati kati ya jiji kuna mtaa unaitwa Mbita. Sasa nimegundua kwanini uliitwa hivyo.
 
Mzee said...sio tu bei ya vitabu ni msiba,lakini pia watu wengi hawapendi kusoma vitabu kàbisa....hilo ni janga kuu
 
RIP Hashim Mbita - the unsung hero of African Liberation struggle.
Asante mzee Said nilikua sijamsikia mtu huyu japo nilikuwa na fahamu zangu wakati wa miaka hiyo ya harakati za ukombozi.
 
Wakati wa awamu ya nne mambo ya udini yamepamba moto, ilikuwa ni faraja sana kumsikiliza Hashimu Mbita akiongea kwa uzalendo wa hali ya juu pamoja na uzee wake. Ni mtu ambaye ukimuangalia na kumsikiliza unatambua ndani na nje ya mwili wake ni mwafrika na mtanzania.

Sasa kuna watu wanataka kumtambulisha kwa label wanazounda wao wenyewe. Tuwakatae maana Mbita alikuwa:
  1. Mzalendo
  2. Mtanzania
  3. Mwafrika.
  4. ..rudia 1-3
Mtu akitaka kumvika vazi tofauti na hilo tumkatae na tumpe heshima mzalendo huyu.
Sooth,
Tatizo la udini halikuanza awamu ya nne.

Tatizo la usini limenza toka enzi ya Tanganyika na unaweza ukaligawa
katika sehemu tofauti.

Udini wakati wa ukoloni mtupu
Udini wakati Tanganyika inapigania uhuru wake, na
Udini baada ya Tanganyika kuwa huru.

Nikimjua vyema marehemu Hashim Mbita na msimamo wake.

Si kumjua tu niliwahi hata kufanya na yeye mjadala mkali tukiwa Madina
Saudi Arabia Hijja ya mwaka wa 1998.

Mjadala wetu ulisikilizwa na takriban Watanzania wote tuliokwenda hija
mwaka ule chini ya Tanzania Muslim Haj Trust.

Suala la udini katika nchi yetu si jepesi.
 
Huku Mwanza kati kati ya jiji kuna mtaa unaitwa Mbita. Sasa nimegundua kwanini uliitwa hivyo.
Sukari...
Majina ya mitaa kuwapa wazalendo imekuwa kitendawili kikubwa.

Kuna watu wamefanya makubwa sana kuikomboa Tanganyika toka
mikono ya wakoloni na hadi leo hawajaadhiishwa.

Nashukuru kuwa Hashim Mbita kapewa mtaa.
 
Sooth,
Tatizo la udini halikuanza awamu ya nne.

Tatizo la usini limenza toka enzi ya Tanganyika na unaweza ukaligawa
katika sehemu tofauti.

Udini wakati wa ukoloni mtupu
Udini wakati Tanganyika inapigania uhuru wake, na
Udini baada ya Tanganyika kuwa huru.

Nikimjua vyema marehemu Hashim Mbita na msimamo wake.

Si kumjua tu niliwahi hata kufanya na yeye mjadala mkali tukiwa Madina
Saudi Arabia Hijja ya mwaka wa 1998.

Mjadala wetu ulisikilizwa na takriban Watanzania wote tuliokwenda hija
mwaka ule chini ya Tanzania Muslim Haj Trust.

Suala la udini katika nchi yetu si jepesi.
Lakini basi tuseme lilifikia kilele wakati wa awamu ya nne. Toka lini watanzania wakagombea kuchinja wanyama? Kikwete alishindwa kuongoza, akaona ponapona yake ni kuwagombanisha watanzania.
 
Bramo,
Unajua mimi sasa ni mtu mzima.
Vijana mkinitania kama hivi nafarajika.

Uzee ni mgumu sana kama huna mbinu ya kukwepa upweke.
JF inanichangamsha kupita kiasi.

Nilikuwa nacheka peke yangu baada ya kukusoma.
Haya lete mnakasha tuchakarike.
SADC HASHIM MBITA PROJECT: SOUTHERN AFRICAN LIBERATION STRUGGLES
Br. Gr Hashim Mbita: Hero of the Liberation Struggle in Africa
​
Copy-of-Hayati-Hashim-Mbita.jpg

Hashim Mbita stood tall as a hero of the liberation struggle in Africa, and he was widely respected for his principles and dedication.His life touched every person who lives in the region, whether they know that or not.He died in Dar es Salaam, age 81, on Union Day, 26 April, the date that Tanganyika and Zanzibar were united in 1964 to create the United Republic of Tanzania. Unity is the message left behind. He was a proud Tanzanian who became a de facto southern African due to his role in the liberation of the region.

Brigadier-General Mbita (retired) was the Executive Secretary of the Liberation Committee for 22 years, from 1972 until his mission was accomplished in 1994 when the liberation of the subcontinent was completed with democratic elections in South Africa leading to majority rule.

He was honoured by the Southern African Development Community (SADC) with the Sir Seretse Khama medal, and by the African Union with its first “Son of Africa” award.

At the SADC Summit last year in Victoria Falls, Zimbabwe awarded Mbita the highest national honour that can be given to a foreigner, The Royal Order of Munhumutapa. He joined a list of only 6 recipients of that award, and all of the others were founding presidents of their respective countries – Angola, Botswana, Mozambique, Tanzania and Zambia.

The citation reads: “For the important role he played in regional liberation as well as integration during his 20-year tenure as the Executive Secretary of the Liberation Committee of the Organisation of African Unity (OAU) – precursor to the African Union (AU).”

The OAU Liberation Committee was hosted in Dar es Salaam by the government of Tanzania, at the invitation of the founding President, Mwalimu Julius Nyerere, who was Mbita’s mentor, teacher and commander.The Liberation Committee provided and coordinated material support for the African liberation movements who had to fight for independence during a 30-year period from 1963 to 1994, and without that support, most of southern Africa may not yet be independent.

He turned the tide of the liberation struggle in southern Africa when, soon after his appointment in 1972, he visited the liberated areas of northern Mozambique with the Mozambique Liberation Front (Frelimo).He wanted to see the situation on the ground for himself, and determine their needs. He was impressed with what he saw in the well-organized liberated zones, but he learned that they were subject to bombing by the Portuguese colonial forces.

His response was to organize anti-aircraft weaponry for Frelimo, and the rest is history.

Frelimo advanced and the Portuguese military officers soon realized they could not win the colonial wars in Africa. Their Movement of the Armed Forces seized power from the undemocratic and dictatorial regime in Lisbon, opened contacts through various third parties, and entered into negotiations with Frelimo for a transitional government that took office in 1974 and independence in June 1975.Angola gained independence a few months later, in November 1975, followed by Zimbabwe in 1980, Namibia in 1990, and finally, democratic elections in South Africa in 1994.

At a conference held in Arusha, Tanzania to close the liberation committee in August 1994, Mbita titled his statement “Mission Accomplished”.He dedicated the final report of the Liberation Committee to the “gallantry of Africa’s freedom fighters, especially to the memory of those who did not live to see the dawn of this era in Africa. This is a tribute to their courage, a salute to the heroes and heroines of African liberation.

“To Eduardo Mondlane, Amilcar Cabral, Herbert Chitepo, JZ Moyo, Josiah Tongogara, Steve Biko, David Sebeko, Duma Nokwe, Johnny Makatini, Peter Nanyemba, Solomon Mahlangu, and, most recently, Christ Hani and Oliver Tambo, as well as the numerous unknown combatants of the African Liberation Struggle.”

Mbita was born in 1933 in Tabora, in western Tanzania, where his father was a clerk at Tanganyika Railways and he got his son into the elite Tabora Boys School on academic performance, among whose alumni counted Julius Kambarage Nyerere, who became the founding president of Tanganyika and later Tanzania.

Young Mbita was active in the cooperative movement that gave Tanzania most of its early leadership, and joined the pro-independence party, the Tanganyika African Nation Union (TANU) in 1958. He moved to Dar es Salaam the year before independence, when young people, mainly men, were being recruited for in-service training in the colonial civil service in preparation for independence in December 1961.

He was assigned to the press section of the ministry of information, soon becoming press secretary to President Nyerere at State House, and hosting the media during official visits such as that of the then Chinese premier, Zhou Enlai, whom he greatly admired. Mbita rose through the ranks in party and government to become the Secretary-General of TANU before being sent by Nyerere to the Tanzania People’s Defense Force as political commissar. He went for military training in Tanzania, as well as Britain and elsewhere, and excelled, as he had with all of his other assignments.

By then, his president had prepared him for most important assignment of all, that of Executive Secretary of the OAU Liberation Committee. He resolved challenges and celebrated achievements, but he never took any credit for himself. He and his country believed that they were “just doing their duty” to the continent.In addition to his humility and all of his other attributes, one of his long-time close friends gave him the best accolade as “a great human being”

Author: Phyllis Johnson
Mohamed Said, Hashim Mbita alikuwa a celebrated hero na linkman aliyeifanya kazi yake kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Ila hujalitendea haki JWTZ kwani ilikuwa na vijana wengi (sasa majerali ) waliyoifanya kazi kubwa kulink JWTZ na mapambano huko Msumbiji, Rhodesia, South West Africa na nchi nyinginezo.

Sisi wengine tulibahatika sana kuishi enzi za ukombozi, na kina Mbita tumeishi nao Chang'ombe ikiwa ni pamoja na kina Samora Machel na Joachim Chissano,mtaa wa Maji Maji.
Unaweza kuniita mzee, ingawaje sipendi title hiyo lakini akiuwawa Eduardo Mondlane, pale Nkurumah, mwaka 1969 kwa bomu la kutegea, wengi wetu tulisikitika sana kama msiba unaotuhusu.

Miaka hiyo akiwa Major Hashim Mbita, alikuwa kiekelezo cha JWTZ kupeleka vijana wake fronline, wengi hawakurudi, makaburi yao huko Msumbiji ni ushahidi tosha.

Siyo siri, uzoefu wa JWTZ katika vita ya ukombozi ulikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa kulipa jeshi letu uzoefu ambao majeshi mengi hayakupitia hilo.
Walikuwepo makamanda kama kina Black Mamba, Mtimkavu, Radi walioutumia uzoefu huo with devastating effects wakati wa kumtwanga Nduli Iddi Amin.
Fuatilia Wakuu wengi jeshini sasa, walikuwa vijana kwenye kamati ya ukombozi, na walifanya kazizao kwa ustadi,uadilifu na uzalendo mkubwa, kama kiongozi wao Major Hashim Mbita.
Tatizo la watanzania hatupendi kuwaenzi mashujaa wetu hadi wamepotea.
 
Gwakisa,
Sijui kwa nini umesema ''sijalitendea haki JWTZ'' ilhali mimi nilichafanya hapa
Majlis ni kuweka hii mada na inatoka katika blog yangu:

Mohamed Said: SADC HASHIM MBITA PROJECT: SOUTHERN AFRICAN LIBERATION STRUGGLES

Mimi nimepita A Novel Idea Bookshop Slip Way, Masaki nikakuta hizo volume 9
basi nikaomba ruksa kwa mwenye duka nipige picha akaniruhusu bila shida.

Nilipofika nyumbani nikamuuliza Prof. Google na yeye akanipa hayo yote hapa.
Joka Kuu yeye kalaumu pia kuwa hatuthamini historia yetu.

Ngoja nikupe kisa cha mapenzi ya watu wa Msumbiji kwa Watanzania.
Mwaka wa 1990 mimi na wenzangu tulikwenda Msumbiji kwa ajili ya mafunzo.

Ndege ilotupeleka ni Royal Swazi.

Kwa mastaajabu tukakuta watu kutoka Wizara ya Nchi za Nje ya Msumbiji wako
uwanjani wanatusubiri kutupokea.

Sisi tulikuwa vijana kutoka Bandarini tunakwenda kusoma kozi fupi ya usafirishaji.
Hatukuwa na hadhi yoyote ya kupokelewa kiserikali.

Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wakawa wanagombana hawataki sisi
tupite Customs kwao wao ni sie Watanzania kuvunjiwa heshima na wao wako pale
kuhakikisha hadhi yetu inalindwa.

Ugomvi mkubwa ukatokea hadi mimi nilipofungua sanduku langu kwa khiyari yangu
na wenzangu wakafatia ndipo ikapatikana salama tukapita kwenda Hotel Cardoso.

Hii ndiyo ilikuwa hadhi yetu kwa hawa ndugu zetu wa Msumbiji.
Sijui leo mambo yakoje.

Kisa kingine nilikwenda kula chakula hoteli ambayo speciality yao ni samaki na beer.
Mimi hilo silijui kuwa hakuna vinywaji baridi hapo.

Kijana mmoja kuona vile akanyanyuka akaacha chakula akenda nje mtaa wa pili na
akarudi na chupa ya Coke akaniwekea mezani.

Akanambia wewe ni ndugu yetu.

Mmemwaga damu zenu kwa ajili ya uhuru wetu sisi na hadi leo ndugu zako wamelala
katika ardhi yetu.

Eduardo Mondlane aliuliwa nyumbani kwake Msasani kwa ''letter bomb.''

Marehemu Hamza Aziz amenambia kuwa mara kadhaa alikuwa
akimtahadharisha Mondlane kuhusu kufungua barua.

Hamza Aziz na Mondlane walikuwa majirani.

Mwaka 2011 nilialikwa Chuo Kikuu Cha Northwestern University, Chicago kufanya
mhadhara.

Hiki ndicho chuo alichosoma Mondlane na mkewe walifahamiana hapo.

Habari hizo ananieleza mwenyeji wangu Jonathon Glassman tukiwa kwenye
ukumbi ambao picha ya Mondlane imetundikwa pamoja na mapambo ya
vinyago vya Kimakonde kutoka Mozambique.

Katika ukumbi huu wa Mondlane ndipo nilipofanya mhadhara wangu.
Sina zaidi la kuongeza.

SAM_1630.JPG
 
Mkuu, mbona ukifungua hiyo link hakuna habari ya Nyerere, Kanisa Katoliki na Uislamu?
Kirikou,
Angalia hii:
Haiwezekani kuielewa ahadi ya Nyerere katika haki na usawa kwa raia wote kama alivyoahidi wakati wa kudai uhuru, hadi usome hotuba yake aliyoitoa tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakati Tanganyika inakua jamuhuri. Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo. Nyerere alifanya hivi labda akijua kuwa ingawa yeye alikuwa Rais Mkatoliki lakini waliomuweka madarakani kuitawala Tanganyika walikuwa Waislam. Nyerere alikuwa na haya ya kusema:

Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.[24]
​
Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema. Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo. Wakati Nyerere anatoa kauli hii ya kutia moyo, serikali iliyokuwa imejaa viongozi wa Kikristo na taasisi za Kikristo zilikuwa imejaa hofu wakiogopa harakati za Waislam za kujiletea maendeleo zilizokuwa zinatapakaa nchi nzima kwa kasi. Walifahamu fika nguvu na umoja wa Waislam ukitumiwa vyema hapana shaka Waislam watakuja juu. Kwa viongozi wa Kikristo waliokuwa wameshika madaraka ya serikali hii ilimaananisha kugawana madaraka sawa na Waislam, kwao wao harakati hizi mpya ziliashiria kuanguka kwa himaya yao katika madaraka kama viongozi.
Hii ilionekana kama harakati za pili za Waislam, safari hii kuchukua serikali kutoka kwa Wakristo. Harakati za kwanza zilikuwa zile za kumng’oa Mwingereza katika ardhi ya Tanganyika. Bila ya kutegemea, serikali ikajikuta inakabiliana ana kwa ana na na jumuiya ya Kiislam iliyokuwa na nguvu ambayo kwa dhahiri yake kila Muislam alikuwa ni mwanachama, na ndani yake imejumuisha wana-TANU shupavu pamoja na wapinzani wa TANU. Wakati huo huo Baraza la Wazee wa TANU katika nafasi yake ya ushauri likawa linaishinikiza serikali ifanye mabadiliko haraka kutokomeza mabaki ya ukoloni. Serikali ikaona harakati hizi ni sawasawa na kuendesha nchi katika misingi ya Uislam. Baraza la Wazee wa TANU lilikuwa sasa limejigeuza kutoka kundi dogo la wazalendo na kuwa kundi lililokuwa likishinikiza serikali ndani ya TANU. Serikali ilikuwa ama ikubali matakwa ya Waislam au ikatae na ipambane na upinzani kutoka kwao. Kuanzia hapa mambo yakaanza kwenda kwa kasi ya kushangaza...

Kama ilivyokwishaelezwa hapo mwanzoni kuwa mwaka 1963 ulikuwa mwaka wa mambo mazito. Ilikuwa ndiyo mwaka ambao Kanisa Katoliki liliteua wagombea wake wapambane na wagombea wa TANU waliokuwa Waislam katika uchaguzi wa serikali za mitaa kule Kigoma na Bukoba. Ulikuwa ndiyo mwaka ambao Rais wa TANU, Nyerere alipombana na EAMWS kupitia Bilali Rehani Waikela. Mwaka wa 1963 ndiyo ulikuwa mwaka ambao Halmashauri Kuu ya TANU ilivunja Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa limetawaliwa na Waislam kwa madai kuwa baraza hilo lilikuwa ‘likichanganya dini na siasa’. Mwaka 1963 ulikuwa mwaka muhimu kwa Halmashauri Kuu ya TANU kwa sababu ilikuwa mwaka ambao ilifanya maamuzi nyeti ya kidini. Mwaka ule Bibi Titi na Nyerere walishambuliana kwa maneno ndani ya Halmashauri Kuu yA TANU kuhusu jambo jingine tena la dini lililokuwa likihusu EAMWS...

Mwalimu Nyerere alikuwa anawaambia Tewa Said Tewa na Bibi Titi Mohamed uso kwa macho wajiandae kwa kile kilichokuwa dhahiri: vita ya msalaba dhidi ya umoja wa Waislam. Sheikh Suleiman Takadir aliyaona haya na aliiomba TANU toka mwaka wa 1958 pawepo na uhakika kuwa Wakristo ambao walikuwa wanapanda migongo ya Waislam na kuchukua uongozi hawatakuja kuwafanyia uadui Waislam pale Waislam watakapokuwa sasa wanataka kugawana madaraka ya kuongoza nchi sawa na Wakristo baada ya uhuru. Tewa Said Tewa, muasisi wa TANU, waziri katika serikali ya kwanza ya uhuru, balozi katika Jamuhuri ya watu wa China na Rais wa baraza la Tanzania la EAMWS, pamoja na Bibi Titi, mwanamke aliowakusanya wanawake wote nyuma ya Mwalimu Nyerere na TANU, walikuwa wakisemwa na Nyerere kama vile watoto wadogo wa shule waliokuwa watukutu kwa sababu tu, walikuja kumfahamisha Rais kuhusu kukiukwa kwa maadili ambayo ilihitaji yeye ashughulikie mara moja na kutoa uamuzi...

Kanisa Katoliki Bukoba lilikosa ujanja kwa hiyo njama zake zikaweza kugundulika mapema. Nguvu mpya dhidi ya Uislam na Waislam ilitumia ujanja na mbinu za hali ya juu na hivyo ikafanikiwa kuihujumu EAMWS na kuiweka BAKWATA kuwaongoza Waislam. Vipi serikali ambayo sifa yake ni kupinga ubaguzi wa rangi na kutetea umoja wa kitaifa, itawaruhusu kikundi kisichozidi watu watano kutumia magazeti ya TANU- The Nationalist, Uhuru, Radio Tanzania, polisi na Usalama wa Taifa, vyombo vilivyo chini ya vya dola kuamrisha utengano wa watu na kueneza siasa za ubaguzi wa rangi. Vipi itaundwa jumuiya ya Waislam ambayo licha kuwa haina ridhaa ya Waislam wenyewe vilevile haina ulamaa hata mmoja ndani ya uongozi wake. BAKWATA haikuundwa kwa maslahi ya kumtumikia Allah. Uongozi wa Kikristo uliokuwa madarakani ulikuwa na hofu ya hali yake ya baadae huku wakikabiliana na Waislam walio huru chini ya jumuiya yao wenyewe iliyo huru na mbali na serikali na Kanisa.

Kirikou,

Ulifanya haraka hukusoma.
Hayo yote nimekunyambulia humo...

Sasa soma kwa furaha.
 
Nani alimteua Hashim Mbita ? nani alimpatia hiyo nafasi hadi akaonekana ! Utashangaa Sheckh wa Tandamti atakwambia aliteuliwa na Msikiti wa Manyema.
 
Mzee Hashim Mbita alikuwa ni mtu wa kawaida sana ambaye ilkuwa sio rahisi kufahamu kuwa ndie yeye aliyekuwa ameshika nafasi nyingi sana za uongozi wa juu, kwani alikuwa mtu rahimu sana na mwanadiplomasia.

Hata hivyo ningependa kutoa taarifa ifuatayo kuhusu uongozi wa kamati ya ukombozi ya OAU. Katibu mtendaji wa kwanza wa kamati ya ukombozi ya OAU ambayo makao yake makuu yalikuwa Dares Salaam alikuwa marehemu George Magombe; ni baada ya marehemu Magombe ndio marehemu Mbita akateuliwa wadhifa huo!!
Babu George Magombe (rip) was the second, katibu wa kwanza wa liberation committee alikuwa Sebastian Chale (rip)
 
Sooth,
Bado hujajua kiini cha tatizo la udini.
Nakufungulia darsa kwako na kwa wana Majlis wengine:
Mohamed Said: MWL. JULIUS K. NYERERE, KANISA KATOLIKI NA UISLAM: DOLA NA TATIZO LA UDINI TANZANIA
Ndugu Mohamed Said,
Nimesoma sana maandiko yako mpaka msimamo wako kuhusu suala hili naujua. Pia nimesoma Mwembechai Killings (kitabu chote) na The Dark Side Of Nyerere Legacy.

Sina 'nguvu na msukumo' wa kubishana au kuelimishana nawe. Mimi nimeutafuta 'ukweli' wa jambo hili hata kabla ya wewe kuanza kuandika JF. Baada ya kujua kitabu cha Prof. Njozi kimezuiwa hapa Tanzania, nikakitafuta na kukisoma, tena with an open mind. Kabla ya hapo nilimsoma Mwijage na The Dark Side of Nyerere Legacy.Nimefika mahali, naamini ninachokiamini. Bila utafiti mpya wa 'independent' scholars, nitaendelea kuamini ninachokiamini.
 
Gwakisa,
Sijui kwa nini umesema ''sijalitendea haki JWTZ'' ilhali mimi nilichafanya hapa
Majlis ni kuweka hii mada na inatoka katika blog yangu:

Mohamed Said: SADC HASHIM MBITA PROJECT: SOUTHERN AFRICAN LIBERATION STRUGGLES

Mimi nimepita A Novel Idea Bookshop Slip Way, Masaki nikakuta hizo volume 9
basi nikaomba ruksa kwa mwenye duka nipige picha akaniruhusu bila shida.

Nilipofika nyumbani nikamuuliza Prof. Google na yeye akanipa hayo yote hapa.
Joka Kuu yeye kalaumu pia kuwa hatuthamini historia yetu.

Ngoja nikupe kisa cha mapenzi ya watu wa Msumbiji kwa Watanzania.
Mwaka wa 1990 mimi na wenzangu tulikwenda Msumbiji kwa ajili ya mafunzo.

Ndege ilotupeleka ni Royal Swazi.

Kwa mastaajabu tukakuta watu kutoka Wizara ya Nchi za Nje ya Msumbiji wako
uwanjani wanatusubiri kutupokea.

Sisi tulikuwa vijana kutoka Bandarini tunakwenda kusoma kozi fupi ya usafirishaji.
Hatukuwa na hadhi yoyote ya kupokelewa kiserikali.

Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wakawa wanagombana hawataki sisi
tupite Customs kwao wao ni sie Watanzania kuvunjiwa heshima na wao wako pale
kuhakikisha hadhi yetu inalindwa.

Ugomvi mkubwa ukatokea hadi mimi nilipofungua sanduku langu kwa khiyari yangu
na wenzangu wakafatia ndipo ikapatikana salama tukapita kwenda Hotel Cardoso.

Hii ndiyo ilikuwa hadhi yetu kwa hawa ndugu zetu wa Msumbiji.
Sijui leo mambo yakoje.

Kisa kingine nilikwenda kula chakula hoteli ambayo speciality yao ni samaki na beer.
Mimi hilo silijui kuwa hakuna vinywaji baridi hapo.

Kijana mmoja kuona vile akanyanyuka akaacha chakula akenda nje mtaa wa pili na
akarudi na chupa ya Coke akaniwekea mezani.

Akanambia wewe ni ndugu yetu.

Mmemwaga damu zenu kwa ajili ya uhuru wetu sisi na hadi leo ndugu zako wamelala
katika ardhi yetu.

Eduardo Mondlane aliuliwa nyumbani kwake Msasani kwa ''letter bomb.''

Marehemu Hamza Aziz amenambia kuwa mara kadhaa alikuwa
akimtahadharisha Mondlane kuhusu kufungua barua.

Hamza Aziz na Mondlane walikuwa majirani.

Mwaka 2011 nilialikwa Chuo Kikuu Cha Northwestern University, Chicago kufanya
mhadhara.

Hiki ndicho chuo alichosoma Mondlane na mkewe walifahamiana hapo.

Habari hizo ananieleza mwenyeji wangu Jonathon Glassman tukiwa kwenye
ukumbi ambao picha ya Mondlane imetundikwa pamoja na mapambo ya
vinyago vya Kimakonde kutoka Mozambique.

Katika ukumbi huu wa Mondlane ndipo nilipofanya mhadhara wangu.
Sina zaidi la kuongeza.

SAM_1630.JPG
Mohamed Said, nilichotaka kieleweke ni kwamba JWTZ imekulia katika vita vya ukombozi.
Na sisi wengine tumekua humo kwa kupitia familia zetu.
Hivyo historia hiyo tumeiishi, we've lived the history.
Na kwa masahihisho tu, Dr Eduardo Mondlane kweli aliuwawa na letter bomb, akiifungua hiyo barua OFISINI mwake pale Nkurumah st.

Walihusika katika vita ya ukombozi ni wengi sana hapa nchini, ila aliyejitokeza kwa vile alikuwa coordinator mzuri ni Major Hashim mbita(namwita Major kwa vile hiki cheo alikaa nacho muda mrefu sana).

Mimi kwa mawazo yangu, ni vema Wizara ya Ulinzi ikaruhusu memoirs za wapiganaji wetu, ambao wengi walifia nchi hii, na wengine walifia huko mstari wa mbele.

Kuna watu sasa hivi wanamnanga Mwalimu, lakini baada ya jaribio la mutiny ya askari wa kikoloni, 1964, miaka mbayo nilikuwepo na kuliona hilo, Mwalimu alitengeneza na kulisuka Jeshi ambalo halina mfanowe katika sehemu hizi za dunia.
I feel proud to have saw the history, na si kuhadithiwa.
 
Nani alimteua Hashim Mbita ? nani alimpatia hiyo nafasi hadi akaonekana ! Utashangaa Sheckh wa Tandamti atakwambia aliteuliwa na Msikiti wa Manyema.
Ngongo,
Ukitaka tufanye mjadala wa heshima tutaufanya na ukitaka tuondoe
staha itakuwa wewe ndiyo unawakaribisha watu ambao ni hodari wa
kejeli na matusi kukushinda.
 
Mohamed Said, nilichotaka kieleweke ni kwamba JWTZ imekulia katika vita vya ukombozi.
Na sisi wengine tumekua humo kwa kupitia familia zetu.
Hivyo historia hiyo tumeiishi, we've lived the history.
Na kwa masahihisho tu, Dr Eduardo Mondlane kweli aliuwawa na letter bomb, akiifungua hiyo barua OFISINI mwake pale Nkurumah st.

Walihusika katika vita ya ukombozi ni wengi sana hapa nchini, ila aliyejitokeza kwa vile alikuwa coordinator mzuri ni Major Hashim mbita(namwita Major kwa vile hiki cheo alikaa nacho muda mrefu sana).

Mimi kwa mawazo yangu, ni vema Wizara ya Ulinzi ikaruhusu memoirs za wapiganaji wetu, ambao wengi walifia nchi hii, na wengine walifia huko mstari wa mbele.

Kuna watu sasa hivi wanamnanga Mwalimu, lakini baada ya jaribio la mutiny ya askari wa kikoloni, 1964, miaka mbayo nilikuwepo na kuliona hilo, Mwalimu alitengeneza na kulisuka Jeshi ambalo halina mfanowe katika sehemu hizi za dunia.
I feel proud to have saw the history, na si kuhadithiwa.
Gwakisa,
Ahsante sana kwa maneno yako.
Hebu check tena hiyo letter bomb.

Ilikuwa nyumbani kwake kwenye ile beach house.
Picha zilitoka katika Tanganyika Standard.

Hebu tutafiti upya huenda kati yetu mmoja kasahau.
Mwenzangu wewe hutaki kuitwa mzee mie napenda.
 
Back
Top Bottom