Sadaka zimekuwa nyingi sana, dini imekuwa biashara

DR SANTOS

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
10,519
21,438
Habari za wakati huu Wana jamvi, mama yetu yupo Egypt kwa majukumu yake ya kikazi, niende moja kwa moja kwenye mada.

Ibada ni kitu muhimu Sana hasa kwa welfare ya kiroho, kwa sababu Vita ya kiroho ni Kubwa Sana Bora hata mtu akukimbize na panga unaweza ukajitetea kwa kukimbia au kupambana nae na ukashinda ila sio huko upande wa pili (spiritually)

Na laiti tungekua na uwezo wa kuona Vita iliyopo kiroho sidhani Kama tungetazamana mara mbili unakuta huyo huyo anaekupeleka hospitali ndie aliekuroga, ndugu zako wanakupiga juju ili usitoboe yaani Mambo ni mengi na ya hovyo tu.

Lakini ibada za siku hizi kwenye haya madhehebu yetu ni mara Mia ukakaa nyumbani ukasoma biblia na ukaenda kusaidia masikini moja kwa moja na ukabarikiwa.

Sadaka zimekua nyingi Sana mtu unakutana na zaidi ya vikapu vitano,baraka zitatoka wapi hapo? Mtu unaanza kugawa sadaka SI ndo yale yale ya kaini na habili?

Nawasilisha.
 
Navyozidi kutumia logic.. naona mapungufu mengi sana makanisani na mazuri mengi sana dini ya wenzetu waislamu..

Sadaka kwenye ukrito imekaa kipigaji pigaji sana hasa fungu la kumi na sadaka zingine kibao. Angalau waislam sadaka inasisitizwa itolewe kama zaka kwa maskini, wajane, wagonjwa, na makundi mengine yenye shida ,,katika nguzo zao za uislam.

Nimeshauguza sana mama yangu muhimbili na moi.. kila mara akilazwa nikienda asubuhi kumuona naona makundi ya waislam wanatembelea wagonjwa waliolazwa na kuwapa uji na vyakula asubuhi .. sio ndugu zao bali ni utaratibu wa dini yao wanasaidia wagonjwa ambao hawana wa kuwapa vyakula.. mimi ni mkristo sijawai kuona kundi la wakristo likifanya hivyo hata siku 1 katika siku zote nilizokuwa naenda moi na muhimbili kumuona mama.

Makanisani mahubiri yanasisitiza sadaka tu na hizo sadaka hazijulikani zinaenda wapi? Maana hata shule za kanisa zilizojengwa kwa sadaka zetu bila kulipa ada mwanao anafukuzwa
 
Navyozidi kutumia logic.. naona mapungufu mengi sana makanisani na mazuri mengi sana dini ya wenzetu waislamu..

Sadaka kwenye ukrito imekaa kipigaji pigaji sana hasa fungu la kumi na sadaka zingine kibao. Angalau waislam sadaka inasisitizwa itolewe kama zaka kwa maskini, wajane, wagonjwa, na makundi mengine yenye shida ,,katika nguzo zao za uislam.
Si kila kanisa ni kanisa,mengine ni mabehewa ya kusafirishia watu kuelekea kuzimu.
 
Nimebahatika kupita Roma a few weeks ago kucheki utaratibu ila dah nilichokutana nacho ni balaa!

1.Kapu la kwanza general sadaka ya misaa
2.Kapu la pili mtolee mungu kwa kibahasha cha kaki
3.Kapu la 3 kumuunga mkono baba paroko
4.Mchango wa ujenzi wa kanisa hapa ilikuwa inatakiwa laki 6 asubuhi sana na mapema. Mwenye elfu 10 yeyote alitakiwa anyooshe kidole na kufuatwa alipo.

Kwa hali hio sikuitarajia ndani ya kanisa takatifu kama Roma! Kumbe wahuni tu kama akina Gwajima🤩
 
Binafsi watumishi ninao wazikiliza na kutoa sadaka kwao, wapo Youtube.
mimi nimekua nikisali Lutheran, naishukuru sana kwa kunipa maziwa nikiwa mtoto mchanga, lakini kwa sasa chakula kigumu ninacho kitaka sikipati KKKT ni nje ya KKKT.

inshort Kanisani siendi, ibada yangu ni Nyumbani tu.
 
Jumapili iliyopita kulikuwa na michango minne..eti kapu la mama la redio maria,mara kusomesha wamisionari..yaani full mizengwe.

Kilichoniacha hoi zaidi ni kutaja jumuiya zilizotoa fedha kidogo kwenye zaka/fungu la kumi na exactly kiasi walichotoa..huku tukiambiwa kutoa unatoa ulichonacho,vipi kama hao wanajumuiya hawana?

RC mizengwe imezidi.
 
Nimebahatika kupita Roma a few weeks ago kucheki utaratibu ila dah nilichokutana nacho ni balaa!
1.Kapu la kwanza general sadaka ya misaa
2.Kapu la pili mtolee mungu kwa kibahasha cha kaki
3.Kapu la 3 kumuunga mkono baba paroko
4.Mchango wa ujenzi wa kanisa hapa ilikuwa inatakiwa laki 6 asubuhi sana na mapema. Mwenye elfu 10 yeyote alitakiwa anyooshe kidole na kufuatwa alipo.

Kwa hali hio sikuitarajia ndani ya kanisa takatifu kama Roma! Kumbe wahuni tu kama akina Gwajima
Imani yako itakuponya
 
Nendeni kwa mtumishi huyu, sadaka sio lazima🐒
download.jpeg
 
Back
Top Bottom