Sadaka ya ajabu kuliko zote

Tumefika mahari ulimwengu usio onekana ( spiritual world ) uheshimiwe na utumiwe sana maana huo ndiyo utatufanya tuyumbe ktk maisha haya au la,ila kupanga ni kuchagua.
 
Sadaka toa mwenyewe kwa kuamua mwenyewe kwa jambo unalolipenda mwenyewe.

Kamaunapenda pombe, kuwanywesha rafiki zako pombe kwa kuwa moyo wakounafurahi ni sadaka kubwa kulikokusaidia masikini halafu roho yakoikasononeka.

Hayo mambo mengine ya asilimia kumi Mungu kasemani uongo tu, Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo angechapa noti zake mwenyewe asihitaji sadaka ya mtu.
 
MAkanisA waliyoleta wazungu yamewafanya mmekuwa wajinga
 
Ni kweli KABISA ila siyo kila penye msaraba unapeleka sadaka hutafanikiwa kwa kiwango kilicho kusudiwa na MUNGU BABA,soma kumbukumbu 12:5 na kumbukumbu 18:18-26
Tumia Agano Jipya kushawishi utoaji zaka.

Pia Mtoa mada. Maana wengi wanatumia Agano la kale ila tukiwaambia nguruwe haramu wanakimbilia agano jipya.
 
In short kama hutoi fungu la kumi huendi mbinguni, mbingu ni kwaajili ya watakatifu na sio kwaajili ya wezi soma Malaki 3:8-12.mbingu ni kwaajili ya wanaolitii neno la Mungu
Justify kwa kutumia agano Jipya.
 
Inaonekana "biashara" inakwenda mrama.
Nasikia na misamaha ya kodi kwa taasisi za dini imepunguzwa.
Nadhani hii no mbinu mbadala ya kupiga pesa za waumini.
Wanasiasa nao hawachangii mpaka itakapofika 2019
 
Ni kama unanunua ulinzi wako
Yaani unalipwa kwa KK security au makampuni mengine ya ulinzi.
Unataka utuaminishe kuwa nipe nikupe and virse versa
Sijaelewa hapa umeandika nini.
 
tatizo hilo fungu la kumi linaenda kuliwa na wengine....
Sadaka haikupasi ufikilie nani anakula iyo pesa wewe toa kwa moyo wote...nahatakama anakula si ndio kamba yake ina mruhusu..kama atakula bila mapenzi ya Mungu laana haita muacha salama
 
in a masonic world we call it rituals. kuna siri nyingi sana za ulimwengu ambazo si kila mtu anazijua, na ikitokea ukajua baadhi tu ya siri hizi unaweza kufanya mambo mengi na ya aajabu sana kwani unakuwa unafahamu principles za ulimwengu.

kati ya principle muhimu sana ni pamoja na kafara/sadaka. na in a masonic world kafara/ sadaka ni kati ya rituals zinazozingatiwa kwa umakini zaidi. fumbo la sadaka/kafara si jambo geni hata kwenye vitabu vya dini. na unaweza kuona katika kitabu cha mwanzo ambapo Cain na abel walitoa sadaka za mazao na mifugo.

kafara ili iwe na mafanikio lazma ikuume, na kafara kubwa zaidi ni ile ya damu hasa ya mtu wako wa karibu. tunaona katika biblia, Ibrahim alijaribisa imani kwa kuombwa kumtoa kafara mwanae wa pekee Isaka, au kwa wakristu, Mungu alitoa kafara ya damu ya mwanae Yesu kristu ili kushinda vita dhidi ya dhambi.

hizi zote hazitokei kama coincidence, bali kuna siri nzito ya ulimwengu iliyo nyuma ya kafara. dini zetu zimedodosa taratibu chache katika maswala ya kafara, na imerahisisha zaidi hata utaratibu wa kutoa kafara hizi kwa kuzipa thamani ya pesa. hivi sasa hutatakiwa kumtoa mwanao, ila utatoa pesa itakayokuuma kiasi. ....
 
Kutoa fungi la kumi ni sawa,, lakini tatizo ni huko zinakoenda,, ya ani mi nitoe fungu la kumi halafu"nabii" apeleke guest,, never ever
Sio lazima umpelekee yeye, ipeleke kwa watoto yatima au wajane au wagonjwa wasiojiweza Mungu atakubariki sana.
 
Nakubaliana nawewe mtoa Mada

Hilo ni la kweli kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…