Sadaka kwa Babu yafikia mil. 50/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sadaka kwa Babu yafikia mil. 50/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Mar 31, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Sadaka kwa Babu yafikia mil. 50/-


  *Yeye kupata mil 10/-, kanisa, wasaidizi mil. 20/- kila moja
  *Kanisa kujenga jengo la huduma la kukaa watu 700 kwa pamoja
  *Wanasayansi Kenya wathibitisha dawa yake kutibu maradhi mengi


  Na Said Njuki, Arusha

  KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati limetangaza kiwango cha
  fedha ambazo kimekusanywa kutoka kwa wagonjwa wanaokunywa kikombe cha dawa ya Mchungaji Ambilikile Masapila kuwa ni sh milioni 50.

  Akitangaza fedha hizo jana, Askofu wa kanisa hilo, Thomas Laizer alisema fedha hizo zimepatikana tangu kuanza kwa tiba hiyo mwishoni mwa mwaka jana, kutokana na mchango wa sh. 500 kwa kila mgonjwa.

  Kutokana na mgao wa fedha hizo kama alivyosema Babu ni kuwa yeye anabaki na sh 100 huku sh 200 zikienda kanisani na 200 kwa wasaidizi wake, yeye atapata sh milioni 10. Kanisa sh. milioni 20 na wasaidizi wake sh milioni 20.

  Wakati huo huo, Kanisa hilo limekamilisha mipango ya ujenzi wa banda kwa ajili ya tiba ya Mchungaji Ambilikile Masapila ‘Babu’ kijijini Samunge litakalogharimu sh. milioni 100 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya mchungaji huyo.

  Jengo hilo litakalohudumia watu 700 kwa wakati moja litakua la mviringo na litajengwa karibu kabisa na babu anakotolea tiba hiyo hivi sasa ambapo kutakuwa na viti vya watu zaidi ya 300, eneo la kutolea dawa, kuchemshia dawa hizo na sehemu ya kuhifadhia hiyo dawa.

  Askofu Laiser alisema jana kuwa uamuzi huo umekuja wakati ambao idadi kubwa ya watu wanateseka kumfikia mchungaji huo kwa kuwa katika jua kali, na wakati mwingine mvua wakisubiria tiba.

  Alisema ujenzi wa jengo hilo utaanza hivi karibuni huku akiwaomba au wengine wakiwemo serikali kutoa ushirikiano wa dhati katika kukamilisha malengo yaliyokusudiwa ili tiba hiyo ipatikane katika mazingira mazuri na yenye tija.

  “Kanisa limeona ni wakati sasa wa kujenga jengo hilo litakalochukua idadi hiyo ya watu na kutolewa huduma zingine bila ugumu wowote. Tangu kuanza kwa tiba hiyo watu na wagonjwa wanaotoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi walikuwa wakisimama kusubiri tiba hiyo,” alisema Askofu huyo.

  Sanjari na hiyo Kanisa hilo limefungua akaunti maalumu benki ya CRDB Na 0150036432600 na kuwaomba watu wenye mapenzi mema kuchangia huduma
  zinazotolewa na Mchungaji Masapila kupitia akaunti hiyo ama moja kwa moja kijijini kwa mchungaji huyo ambapo kutakuwa na utaratibu maalumu kwa ajili hiyo.

  Akizungumzia uchakachuaji wa barabara unaofanywa na baadhi ya madereva kwa kupitia Longido ili kuwahi kikombe cha babu bila kufuata foleni, Askofu alisema hiyo ni sawa na magendo mengine jambo ambalo halina baraka ndani yake.

  Alisema anaamini hata hao walipata kikombe hicho ni wazi wanakimbiza baraka zao kutoka kwa Mwenyezi Mungu hivyo hatima ya magonjwa yao ipo katika imani zao lakini si jambo zuri.

  Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Elias Wawa Lali kwa upande wake alisema kuwa foleni katika Kijiji cha Samunge imeanza kupungua kwa kiwango kikubwa hivyo kuwa na uhakika kwamba muda ulitolewa na mchungaji huyo utafikiwa.

  Pia alikiri kuwepo na madereva walikuwa wakichakachua njia ya Longido
  kupitia Ziwa Natron na kumfikia babu kirahisi na kwamba hali hiyo ilitokana na watu wa Longido kuchelewa kuweka kizuizi lakini sasa hakuna tena uchakachuaji huo.

  Wataka chumba cha maiti

  Serikali imetakiwa kujenga chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha Samunge Arusha ili wagonjwa wanaokufa njiani wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa Babu ili maiti zao zihifadhiwe.

  Pia imetakiwa kuwawajibisha polisi wanaochukua rushwa ili kuwaruhusu watu wanaoenda kwa babu wakati serikali imezuia watu wapya hadi waliotangulia wapungue.

  Bw. Edward Mtakimwa, aliyesema ametoka kwa babu kupata kikombe alisema kwenye ofisi za Majira kuwa serikali ijitahidi kumsaidia mchugaji huyo ili aweze kuendelea kutoa huduma ya uponyaji katika mazingira yanayostahili.

  "Polisi wanachukua rushwa kwa wagonjwa wanaoenda kwa babu ili waweze kuwarusu wakati serikali imetoa tamko la kuwazuia hadi waliotangulia wapungue," alisema.

  Bw. Mtakimwa aliiomba serikali kuendelea kuiruhusu helkopta ya Mbunge wa Moshi Mjini, Bw. Phillemon Ndesamburo ili iwawaishe wagonjwa mahututi, na iingilie kati bei ya vyakula ambapo sahamo moja inauzwa kati ya sh. 2,000 hadi 3,500, nyama kwa kilo ni sh 8,000 hadi 10,000, maji ya kunywa chupa nusu lita sh 1,500 na lita moja ni sh 5,000.

  Malori yapigwa marufuku

  Serikali mkoani Mwanza imepiga marufuku aina zote za malori kusafirisha wagonjwa wanaokwenda kupata kikombe cha babu katika kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro.

  Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abbas Kandoro kwenye kikao kilichowashirikisha wadau wa vyombo vya
  usafirishaji pamoja na vyombo vya habari.

  Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Babu kuomba msaada wa serikali kufuatia wagonjwa wengi kufariki wakiwa safarini na kwenye kufuata huduma yake.

  Imeandaliwa na Daud Magesa,Mwanza; Agnes Mwaijega, Dar na Said Njuki, Arusha
  [​IMG]


  5 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... HAYA KILLA LA KHERI NAONA HAPA KAMA KUNA UCHAKACHUAJI MAANA DATA ZILIZOKUWA ZINARIPOTIWA UMATI WA WATU KILA KUKICHA INA MAANA MPK SASA NI WATU LAKI MOJA TUU NDIO WALIOKUNYWA DAWA KWA BABU? MAANA LAKI 1 X 500=NDIO MIL.50.HONGERENI KKKT!!! NAONA MAKATO HAYA KAMA TFF NA KLABU ZA YANGA NA SIMBA MAANA MMHHHH!!
  March 31, 2011 12:03 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... babu hajafaidi lolote. Ni kazi ya Mungu. Mungu aendelee kumpa nguvu zaidi.
  Amen
  March 31, 2011 1:15 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... NAWASIWASI KUNA UCHAKACHUZI YAANI WATU WALIOKWENDA KWA BABU NI LAKI MMOJA TU???

  KWELI KKKT KANDA YA KASKAZINI NI WACHAGA HASWA DUU!
  March 31, 2011 2:30 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... IKIWA UWANJA MPYA WA MPIRA(NATIONAL STADIUM)UNA INGIZA WATU ELFU SITINI INA MAANA TOFAUTI NI WATU ELFU 40 NDIO IFIKIE UMATI WA KWA BABU AMBIKILE.KKKT ACHENI KURONGOFYA!

  NISHAANZA KUWA NA WASIWASI NA HIYO HUDUMA SASA! AU NI AINA MPYA YA UINJILISHAJI MPYA?
  March 31, 2011 2:38 AM [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Reggy's said... Jamani tuwe fair, wale wanaolinganisha na wanaoingia mpirani, mbona hawafikirii kuhusu viingilio? Mpira gani una viingilio vya 500 kwa wote? Lakini pia kumbuka mwanzoni hawakuwa wanakwenda watu wengi hivyo, maana taarifa zilisambaa kwa kusimuliana, hadi februari vyombo vya habari vilipomfahamu Babu. Hata hivyo, kama Babu angekuwa anatibu watu 2000 tangu mwanzo (let say kwa miezi 6 au siku 180 tangu Oktoba) angekuwa na watu 360,000. Honestly, mimi naona ni sahihi hakuna uchakachuaji, na kama upo si wa kupoteza muda kujadili.
  March 31, 2011 2:56 AM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Nimeitafuta habari hii ya wakenya kuthibitisha "kikomba" kinatibu maradhi mengi sikuiona..............where is it?

  PHP:
  *Wanasayansi Kenya wathibitisha dawa yake kutibu maradhi mengi
   
Loading...